JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Watu wa humu ndani nimewashindwa tabia yaani mkiwa na kesi mnapotea, mkiombwa kitu mnapotea kwanini mwalia gizani kwa kumwogopa jirani?

Neybright kukuomba uniazimishe baby wako ndo umekimbia kabisa jukwaa?

Kichwa Kichafu kukuomba twende wote mpirani ndo umepotea mazima?

Manga ML kukuomba unifundishe kubet umeacha na kukesha?

Nleterewa Nganengo Kukuomba dawa ya kupunguza wivu ndo umebadilisha na njia hupiti tena huku?

Samaritan kukuuliza swali ndo ukapotea mazima?

Joseverest kukwambia nitakuja uninunulie bombadia ndo hata nafasi yako ya 2 umeiacha kweli?

jje's kukukwambia naomba usiku mmoja tu na KK ndo ukaaga kabisa hapa jukwaani?

Maserati kukuomba blanket nijifunike kupunguza hili baridi ndo huonekani tena?

Jamani sio vizuri hivyo, mimi nilikuwa nawatania tu....kwanza MOYO WANGU SULTAN CHA MTU SITAMANI [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
Ahahahaaaaaa wewe ni kiboko [emoji119] [emoji119] [emoji119] Aiseeh mie sikuwez ujue, umejua kunichekesha leo
 
Back
Top Bottom