TUSHIRIKISHANE JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

ila ujenzi wa kituo cha afya NHOBORA ukikamilika pasipo kujenga hili daraja linalounganisha kijiji cha cha NHOBORA na kijiji cha MBOGWE ni sawa na bure tu

kwani wagonjwa watakaohitaji kupewa rufaaa kuja hospitali ya wilaya nzega kwa haraka ni vigumu kwani miundombinu si rafiki huo mfereji wa NHOBORA marufu kama daraja la NHOBORA kipindi cha mvua hujaa maji na kukatisha mawasiano kwa watembea kwa miguu, baiskeli, magari ndio hayafiki katika hivyo wakiwa wanamalizia kituo cha afya wakumbuke na hili daraja alimarufu kama daraja la NHOBORA
 
HONGERA SANA KAKA MAX NA JF-MUNGU AWAPE AFYA NJEMA, ILI MALENGO HAYA MEMA YATIMIE KWA MAJIMBO TISA NA WIGO MTAKAOUTANUA BAADAE.

KWA HAZINA YA BRAIN ZILIZOKO HUMU NAAMINI JF ITAISHANGAZA DUNIA KWA AINA YA MIRADI MTAKAYOIBUKA NAYO KWA JAMII.

KARIBUNI SANA NA KWETU.
 
kitu kingine wana nzega tunahoji umaliziaji wa kituo kipya cha mabasi hivi lini hiki kituo kitaisha ujenzi wake

Na ikiwa hakikamiliki leo wala kesho je tatizo nini wananzega tuna hamu ya kujua kwani tumesubilia kwa mda mrefu sana kupata kituo kipya cha kisasa cha mabasi kwani uwepo wake ni chachu ya maendeleo yetu sisi wakazi wa nzega na halmashauri kwa ujumla
 
Hilo Daraja la Nhobola lipo kwenye bajeti ya 2016/2017 pamoja na lile Daraja la Butandula kata ya Ijanija.
Infact Mh Mbunge alipewa option mbili kwa mwaka huu wa fedha.

1. Kilomita 10 za lami Nzega Mjini,

2. Madaraja mawili ya Butandula na Nhobola.

Kwahiyo Mh alichagua hayo madaraja mawili. Nikutoe hofu kazi hiyo tayari ipo kwenye pipeline.
 
Umenielewa vizuri kabisa.
 
Kituo hichi sasa hivi Mkandarasi yupo site na nimoja kati ya maazimio ambayo tumejiwekea kuyakamilisha ndani ya miezi 9 kuanzia sasa ndani ya miradi 4 ya Tushirikishane.
Tumeshapata pp kwahiyo wananchi watakodishiwa maeneo na kujenga na watakatana na Halmashauri kwenye kodi.
Ujenzi huu utakua chini ya usimamizi wa ma Engineer wa mji.
 
Mkuu Maxence Melo majibu mazuri ya aina hii ndio tunatarajia kuyakuta kwenye "chumba cha mkutano na mbunge" na kwa maana hii ama mbunge mwenyewe au katibu wake kwa ruhusa ya mbunge angewajibu wapigakura wake hivi.

Lakini pia angetoa nafasi ya mjadala na wapiga kura wake pale alipopewa option mbili, yaani madaraja au lami.
 
Mh Mbunge aliangalia maslahi mapana ya uhalisia wa tatizo.
Nzega mjini tayari kuna lami japo haijitoshelezi kwa kiwango kikubwa ila kwa Daraja la Nhobola umuhimu wake ulikua ni mkubwa sana na watoto wengi pamoja na wananchi walikua wanatengwa na kipindi cha masika. Wanafunzi walikua wanashindwa kwenda shule na shughuli za kiuchumi nyingi zilikua zinakwama kutokana na kutokuwepo kwa daraja ili.
Kwahiyo ni busara ndio iliyompelekea Mh Mbunge kuchagua Daraja hilo badala ya lami ya mjini.
Hata hivyo tunachukua ushauri wako.
 
View attachment 380549
Ujenzi wa nyumba ya muuguzi katika kituo cha NHOBORA tutafurahi sana ujenzi wake ukikamilika.

Asanteni Jamii Media kutuletea huu mradi wa TUSHIRIKIANE, tuna imani utasaidia ondoa hii changamoto
Mh
Mbunge Hussein Bashe akimkabidhi mtendaji wa Kata ya Mbogwe hundi ya million 9 kwaajili ya ukamilishaji wa nyumba ya Mganga mkuu katika kituo cha afya cha Nhobola
 
Nakushukuru kwa jinsi umeendelea kutoa "madini" ambayo jamii inafaidika nayo.

Nilipenda somo la post yangu lieleweke vizuri zaidi.
Tunapenda mbunge wetu awe na busara, busara hii imuelekeze kuwa ni afya kwa maendeleo kunapokuwa na majadiliano kabla ya kutoa uamuzi.

Na utekelezaji wake sii mgumu, tunakutania kwenye "chumba cha mkutano na mbunge"
Chumba hiki kiwepo kwa kila jimbo ndani ya Jamiiforums
 
Tuko pamoja mdau.
 
Serikali imeshatenga fedha hizo na ujenzi utaanza muda si mrefu
 
KIPITA SHOTO MJINI NZEGA


Nikiwa kama mwananzego(mkazi) wa mji wa nzega nimefurahi sana kupata majibu kutoka kwa mwanachama mwenzetu hapa jamii Forum anajiita GIDEON ANYONA safi ila na swali

Leo hii jamii Forum wamekuja na huu mradi katika jimbo la nzega wameanzisha huu mjadala tumeweza yasema tunayoona kero na Gideon amajibu niwapongeze jamii Forum kwa hili kwani tumepata pakusemea

Swali langu kwa huyu Gideon taminije usemayo ni tarifa sahihi?

Pili ikiwa usemayo ni tarifa sahihi je ni wapi mwananzego asiyejua tumia jamii Forum akaona tunayoyajadili hapa anaweza kwenda nakuzikuta hizi tarifa sahihi?

Tatu unaweza kuwa msaad kwangu na wananzega wengine watumiao hii mitandao ya kijamii tunaomba utupatie tofuti ya halmashauri ya mji nzega ili tuingie tuone yaliyomo maaana nimehangaika sana kutafuta tarifa za ulichonijibu sijaona

Asante
 
Asante sana mwanazengo.

Taarifa ninazo zitoa ni sahii na zinapatikana Halmashauri ya mji na ofisi ya Mbunge.
Moja kati ya changamoto ambazo tukonazo na ambayo Tushirikishane imetusaidia ni swala la kutoa taarifa sahii na kwa wakati muafaka.
Kwa kupitia platform hii nitakua natoa taarifa sahii humu.
Swala la mradi wa daraja la Nhobola nimetoa evidence hapa Mh Mbunge akijibiwa bungeni.
Kuhusu pesa na hundi zilizotolewa picha zipo na taarifa hizi zipo Halmashauri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…