JAMVI LA WANAWAKE: Baada ya kumuoa anataka wawe wanafanya mapenzi kinyume na maumbile, afanyaje?

JAMVI LA WANAWAKE: Baada ya kumuoa anataka wawe wanafanya mapenzi kinyume na maumbile, afanyaje?

Acha tu, mimi ni mama wa ushauri nasaha. Huwa naletewa visa huko mtaani nachoka kabisa na wakati mwingine naingiwa uoga dhidi ya binadamu. Visa vingine ndiyo hivi, nawaletea na nyinyi humu JF mchangie mawazo

Jamvi haliwezi kuchanika, ndiyo mahali pa kuanzisha mazungumzo.
So far I'm proud of you elimisha hawa wajinga wanaotuita mbwa halafu ikifika visikukuu vya kijinga kama valentine wanataka gifts
 
Kichwa cha uzi kinasema Jamvi la wanawake nashangaa kuona wanaume ndo wa kwanza kuchangia.
 
Nimeshirikishwa mkasa wa binti mdogo wa miaka 23 ambaye ameingia kwenye ndoa wiki kadhaa zilizopita. Baada ya ndoa, mumewe ameanza kumuomba wafanye mapenzi kinyume na maumbile, jambo ambalo hakuwahi kufanya hapo kabla. Ilipotokea siku ya kwanza hakusema moja kwa moja, ila katikati ya kushiriki tendo alijifanya kama kakosea na kutaka kumuingilia kinyume, alivyoona binti hatoi ushirikiano hakuendelea ila siku inayofuata akamwambia live kwamba atafurahi zaidi akiwa anampa unyumba pia ampe Yas.

Binti yuko njia panda, ndoa bado changa sana, hataki kupeleka hili tatizo kwa wazazi maana ni aibu ila pia anahofia asipomkubalia mumewe ataenda kutafuta anachokikosa kwa mtu mwingine.

Tusaidiane kumshauri (kwa hekima na siyo kumkebehi, kumchamba au kuandika maneno yasiyofaa ya kumdhihaki) nitamtumia replies zenu!

View attachment 3237530
Asikubali huo ushetani. Huyo mume tayari ana wahuni wanaompa anayotaka. Ashikilie msinamo wake. Yeye ni mke. Sio mhuni. Full stop atakuheshimu. Labda alisikia kwa wahuni wengine kuwa unatoa. Kama sivyo afadhali ndoa iishe kwa sababu hiyo. Hajielewi bado. Shida vijana wengi wameingia ktk mtego huu. Hasa wasichana kwa kuogopa kupata uja uzito.
 
Yeye ana 23, jamaa ana ngapi?

Aanze yeye kukaa chini, aelewe kwanza anachoambiwa kufanya, afanye upembuzi wa side effects kama zipo...baada hapo;
  • Kama ameingia kwenye ndoa rasmi ya kidini/kiimani, basi achunguze kwenye dini yake wanasemaje kuhusu hilo swala.
  • Jamii yake, ina muelekeo gani kuhusu hilo, lazima kuna wamama watu wazima ambao ni wa kabila, ukoo na hata jamii iliyomzunguka, azungumze naye kana kwamba yeye ndo anawaza kufanya hivyo ili kumdhibiti mume, atapewa a,b,c tu.

Atakuwa amejiweka kwenye nafasi nzuri sasa kiimani, kijamii na nafsi yake, kuona afanye nini!

Mwisho, za kuambiwa achanganye na zake baada ya kupata maarifa hayo.
Asante sana Ndalilo, ushauri utamfikia.
 
Nimeshirikishwa mkasa wa binti mdogo wa miaka 23 ambaye ameingia kwenye ndoa wiki kadhaa zilizopita. Baada ya ndoa, mumewe ameanza kumuomba wafanye mapenzi kinyume na maumbile, jambo ambalo hakuwahi kufanya hapo kabla. Ilipotokea siku ya kwanza hakusema moja kwa moja, ila katikati ya kushiriki tendo alijifanya kama kakosea na kutaka kumuingilia kinyume, alivyoona binti hatoi ushirikiano hakuendelea ila siku inayofuata akamwambia live kwamba atafurahi zaidi akiwa anampa unyumba pia ampe Yas.

Binti yuko njia panda, ndoa bado changa sana, hataki kupeleka hili tatizo kwa wazazi maana ni aibu ila pia anahofia asipomkubalia mumewe ataenda kutafuta anachokikosa kwa mtu mwingine.

Tusaidiane kumshauri (kwa hekima na siyo kumkebehi, kumchamba au kuandika maneno yasiyofaa ya kumdhihaki) nitamtumia replies zenu!

View attachment 3237530
Ana options mbili, ampe au aombe talaka. Muulize kati ya hizo lipi ni rahisi zaidi kulifanya?
Kupanga ni kuchagua.
 
Hicho ni kigezo tosha cha kuvunja ndoa,..vunja hiyo ndoa au kubali kutoa mixx by yas uingie dhambini pia uwe hatarini kupata madhara mengine ya kiafya na pia utatembea na pampasi maisha yako yote (gharama ),hapo ujavaa pedi, kumbuka utakuwa unanuka mavi muda wote
 
Kweli kiswahili kinakuwa, bila kusoma ndani nilikuwa sijaelewa uliposema Ndogo

Bora tumezeeka sasa 🙌
 
Nahisi uongozi wa jamii forums huwa unavutiwa sana na mada za aina hii, kuliko hata zile mada za Wananchi kuikosoa serikali isiyo jielewa.
Mada za wananchi ni muhimu sana na kila mtu anapaswa kushiriki kwa namna moja au nyingine huko mtaani na pia JamiiForums kama sehemu ya kuexercise civic duties zake.

Ila pia mada za kijamii, zile zinazogusa maisha binafsi ya watu zina umuhimu wake. Inatulazimu kuongelea maswala ya kimahusiano au changamoto nyingine za maisha kutoa balanced reflection ya jamii zetu.
 
Hii dhambi Mungu hutoa adhabu mwenyewe ukiwa bado hai.Kumbuka katika ndoa miili yenu tu ndo mmoja.Lakini kila mtu anabeba nafsi yake.Hivyo kama nafsi yako inakaataa ifuate.Mungu atakupa mume mwingine
 
Kichwa cha uzi kinasema Jamvi la wanawake nashangaa kuona wanaume ndo wa kwanza kuchangia.
Asante kwa Reply Dede,

Jamvi la leo la wanawake linaelezea mkasa wa mwanamke uliosababishwa na mwanaume. Naona ni vizuri kabisa kwa wanaume kushiriki pia.
 
Back
Top Bottom