Jana ilikuwa siku ya Furaha kukutana na Graduate anachoma mahindi Barabarani

vipi kama anatafuta mtaji wa kununua komputa? madhara ya kusoma kwa kukariri vitabu ndo haya hapa, maisha sio kukariri maisha ni kujizidisha ni kubadilika kulingana na wakati.
elimu zetu pia zina shida sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mrejesho mkuu wa hii biashara
 
IT ukitoka hujui kitu utachoma sana mahindi..hii course ni kipaji na kujituma...lakini ukiwa mzuri IT huwezi kuchoma mahindi
 
Somo kubwa la kujivunza hapa ni kutokuwa na uoga na aibu!!
Ila kukusanya mtaji kwa kuchoma mahindi, huduma zingine za kimaisha anaziendesha vipi na anasevu kiasi gani??!!

Unajua hebu tutulize vichwa kwanza.
Hindi 1@200/= kinatoa vipande 10@200.
Hindi moja anapata tsh 2000 kila hindi.
Toa 500, kwa ajili ya mkaaa na usafiri. Na other cost.
Akiuza mahindi 30 tu kwa siku.
30*2000= 60000kwa Sikh.
Tupate gharama kamili.
1500*30=45000@day
45000*30=1350000.
Endelea kuzomea tuuu.
 
Na huyu adaiwi kodi ma tra
 
Huko si kukusanya mtaji! Ni kusukuma siku imradi maisha yaende!
Mkuu usimdharau huyo mtu.Unaweza shangaa kesho anakuwa mwajiri wako.
Nina mfano wa dogo mmoja ni mdogo sana kwangu ni rafiki wa Karibu wa mdogo wangu.
Huyo dogo alikuja Dar kurudia mtihani wa kidato cha nne akachemka mara kadhaa.Akaacha habari Za kurisiti.
Akaamua kufungua genge dogo tu la mboga mboga.Bahati mbaya akawa hapati hela ya kumfikisha popote,ikawa inaishia kula Na Kodi tu.Akajiingiza kwenye zile biashara Za kutembeza vyombo barabarani.Alipotoka hapo kwenye kutembeza vyombo akapata mchongo wa kuuza maduka ya hardware ya Mhindi kule Kariakoo.Baada ya muda Fulani dogo naye kafungua hardware yake.Pia ameanza kilimo pia.Muda huu mpaka naandika dogo yupo mbali sio wa level yetu.Ni Kijana mdogo lakini kapiga hatua sana.Lakini ukiangalia alipopitia ni mateso tupu.
 
Kuchoma mahindi ni njia tu.Hawezi kaa Bila kazi wakati muda unapita.wakati anatafakari cha kufanya ndio anachoma mahindi.Usishangae katika ujasiri wake wa kuchoma mahindi akapata mchongo au wazo la biashara nyingine
 
Tatizo Huwa lipo kwenye matumizi.Kuna jamaa hapa Huwa anaosha magari Na huwa anapata visenti Walau lakini jamaa ana ratiba yake lazima kila siku jioni apite kwa Malaya apige mzigo.Ndio maana kila siku jamaa utamkuta analalamika hela
 
Huyo graduate tena IT unachoma wahindi???. Self mind yake uko chini sana.
 
hz hesabu hua za kisenge ndo maana watu wanaingia ingia kichwa kichwa sasa 60k si kila mtu angechoma hayo mahindi
 
Wanaomzomea huyu jamaa kuna siku atawaaajiri kwenye kubeba mahindi shambani Na wanaenda.Mtu anayejishughulisha si sawa Na Yule asiyejishughulisha
 
Katika Maisha ukiamua kutoa uoga Na aibu kuiweka pembeni basi ujue njia ya mafanikio inaanza kuonekana.Kinachotucost wengi ni Woga Na aibu
 
Nina mifano mingi tu ,jamaa mwingine alisoma pale Ardhi alivyomaliza Chuo akawa anafanya kazi ya kusukuma magogo ya mbao msituni (Pingili) kazi ambayo inafanywa au imezoeleka kufanywa Na darasa la Saba au walioacha shule ya msingi .Jamaa alijitosa Bila kujali maneno ya watu,lkn muda huu he is a big boss.Muda huu yupo busy sidhani kama anaweza pata muda wa kuja kupiga porojo hapa Jf,yeye Sasa hivi ni Employer tena wa watu wengi sio mtu mmoja tu
 
ULIVYO NA WAZAZI WEWE UNADHANI WOTE WANA WAZAZI NA KWAO POLE SANA DUNIA HUJAIFAHAMU BADO
 
Watu wanadharau..bila kujua..
Bei ya jumla sokoni ni 280-350 kwa Hindi moja
Mkaa kwa siku ni elfu NNE...
Hiindi moja mjini linauzwa sh. 700-1000...
Akiwa sehemu nzuri anawastani Wa mahindi 100kwa Siku.. Na uharibifu mahindi 15 ... Huyu MTU anatumia max 45,000/-
Na anapata gross ya 100,000/-
Net 55,000/- tucheke ujinga tu.
 
hz hesabu hua za kisenge ndo maana watu wanaingia ingia kichwa kichwa sasa 60k si kila mtu angechoma hayo mahindi
Nadhani ni mfano tu jamaa kaweka.Yale mahindi kutoa vipande kumi ni ngumu.But wale wachoma mahindi hela ipo asikudanganye mtu kuwa hawapati kitu.Ingekuwa hawapati faidi wangeacha kufanya ile kazi.Huoni mtu yupo Na familia lakini anaishi kwa kuuza supu ya pweza,kuchoma mahindi kuuza machungwa.By the way hiyo 60k ni kubwa mno lkn amini hela ipo.Ni tofauti Na kukaa bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…