Jana mechi ya Chelsea na Man City, Guardiola tena kaonesha ubaguzi hadharani

Jana mechi ya Chelsea na Man City, Guardiola tena kaonesha ubaguzi hadharani

Binafsi nahisi Doku alitolewa mchezoni baada Yellow Card aliyopewa kwa kosa la kujiangusha. Huenda Guardiola aliona Doku anaweza asiperform vzuri tena coz kama kaaibishwa flani hivi. Kitendo cha Doku kuanza na kumuach Jack bench tayari hyo ni respect. Pia Grealish anakaba kuliko Doku kwa mechi ile ya jana alifaa kupunguza kasi.
 
Yapo ya kulaumu. Ila hilo la kumtoa Doku wala si mojawapo. Yaani unataka wachezaji weusi waachwe hata kama mpango wa timu unabadika, ili tu kuonesha hakuna ubaguzi?

Doku alilambwa kadi dakika ya 56, kisha akatolewa dakika ya 59. Mpaka Doku anatoka, City alikuwa anaongoza 3-2.

Anaingizwa Grealish, mwenye uwezo wa kutuliza pressure ya timu na kupiga pass zenye macho zaidi.

Doku ni aina ya mchezaji mwenye makeke, speed na nguvu. Ila kwa approach ya jana, Chelsea alikuwa moto. Ukiangalia pia, Doku jana kabla hajafanyiwa Sub, ilipigwa counter attack, mwenzake wa kumpasia yupo akaamua kupiga shuti la hovyo na kuwa chakula kwa Sanchez. Uchoyo wa kipuuzi tu.

Ila Mkuu, wachezaji wote hulilia kuanza kikosi cha kwanza. Na baadaye kujihakikishia namba.
Doku ni mchezaji mzuri mno, ila winga ya kushoto alikuwepo mtu bora sana msimu uliopita. Ashukuru Mungu amekuwa katika kiwango bora na Guardiola kaanza kumuamini. Hizo dakika nyingi zinamtosha mno, kuliko kusubiri kwenye mbao ndefu.

Hakuna ubaguzi wowote. Ni mbinu za Mwalimu.
 
Tuache mawazo ya kijima, why kila kitu a black person akiona kinyume anacheza RACE CARD, why?,tuelewe kila kitu kizuri kinapokua touched na black man kinakua cha ovyo, angalia zim,sa,ni craze, kocha wa citizens hana ubaguzi, ni mawazo ya kijima ya black man
 
Guardiola Alivyopewa tu Timu ya Barca 2008 alimuondoa Ronaldinho akahamia AC Milan. Wakati dunia nzima inaona Ronaldinho hagusiki yeye akamuondoa. Itakuwa kina Yaya na Eto'o?
Naona hujaelewa nilichoandika. Wapi nimezungumzia maswala ya uhamisho hapo. Yaani watu kama nyie ndio huwa mnafanya Afrika tunadharaulika.
 
Mzuka Wanajamvi.

Ilikuwa hamna haja ya Pep kumuondoa Doku na kumuweka Grealish.

Wadau hatukupendezwa ukizingatia Doku alicheza vizuri sana. Na angebaki hadi mwisho City wangechukua point zote Tatu.

Hata kumuanzisha Doku tu ilikuwa Zuga. Huyu jamaa ataacha lini ubaguzi?

Herzog mkorea
Ila kile ki Doku ni moto sana.
 
pep kuna tabia hazitaki hasa kujiangusha ni mtu wa displine sana, ila pep aliharibu kumuanzisha doku greilish akianza huku akijua sub yake iko nnje anakuwa wa moto na makin sana,
pia foden inatakiwa acheze AMF doku na greilish wagawane pande bernando aanzie njee kwa ajili ya kumpokea mmoja wapo
rodri na stone DMF ball linatulia sana
 
Back
Top Bottom