Jana mechi ya Chelsea na Man City, Guardiola tena kaonesha ubaguzi hadharani

Jana mechi ya Chelsea na Man City, Guardiola tena kaonesha ubaguzi hadharani

Yapo ya kulaumu. Ila hilo la kumtoa Doku wala si mojawapo. Yaani unataka wachezaji weusi waachwe hata kama mpango wa timu unabadika, ili tu kuonesha hakuna ubaguzi?

Doku alilambwa kadi dakika ya 56, kisha akatolewa dakika ya 59. Mpaka Doku anatoka, City alikuwa anaongoza 3-2.

Anaingizwa Grealish, mwenye uwezo wa kutuliza pressure ya timu na kupiga pass zenye macho zaidi.

Doku ni aina ya mchezaji mwenye makeke, speed na nguvu. Ila kwa approach ya jana, Chelsea alikuwa moto. Ukiangalia pia, Doku jana kabla hajafanyiwa Sub, ilipigwa counter attack, mwenzake wa kumpasia yupo akaamua kupiga shuti la hovyo na kuwa chakula kwa Sanchez. Uchoyo wa kipuuzi tu.

Ila Mkuu, wachezaji wote hulilia kuanza kikosi cha kwanza. Na baadaye kujihakikishia namba.
Doku ni mchezaji mzuri mno, ila winga ya kushoto alikuwepo mtu bora sana msimu uliopita. Ashukuru Mungu amekuwa katika kiwango bora na Guardiola kaanza kumuamini. Hizo dakika nyingi zinamtosha mno, kuliko kusubiri kwenye mbao ndefu.

Hakuna ubaguzi wowote. Ni mbinu za Mwalimu.
Kwanza Ile hali ya Guadiola kumuamini Doku kwa haraka hivi ni jambo kubwa sana ambalo kimsingi limewashangaza wengi.

Doku ndio kwanza ana umri wa miaka 21 na hajawahi kucheza timu yoyote Ile kubwa ametoka Rennes huko timu ya daraja la Kati(midtable team) Leo amefika Manchester city timu yenye pressure na ubingwa na kuingia kwenye first eleven moja kwa moja huku akimpiga benchi muingereza mzungu Jack Grealish halo sio jambo dogo eti... Yaani mpaka nashangaa watu kama huyu mleta mada hizi nguvu za kum accuse Pep kuwa ni mbaguzi wanapata wapi? Sijui ni ujinga tu una msumbua

Unajua wengi tulitarajia huyu Doku angalau atspend hata msimu mmoja akitokea bench Kisha ndio aje awe regular starter baada ya kutoa Etihad... Lakini Pep kamuamini hivyo hivyo pamoja na kwanza Bado hana experience yoyote kwenye miki miki ya EPL.
 
Back
Top Bottom