Jana na leo alfajiri nimeota ndoto zimenistaajabisha kidogo

Jana na leo alfajiri nimeota ndoto zimenistaajabisha kidogo

Nilishtuka toka usingizini, ila niliogopa, nilifunga na kuomba. Baanda ya wiki moja hivi nilimuota tena, nilikua mtoni nachota maji, yeye akawa amesimama pembeni ananitazama kwa huruma sana. Ndoto Kama hizi zinaogopesha japo tunambiwa ndoto ni mambo uliyowaza, unajikuta na maswali mengi mengi. Mi mpaka sasa sijui tafsiri ya ndoto
ni kweli inaleta maswali sana
 
U see how God love his people!

Km ww ni mkristo najua utakua unajua jinsi ya kuomba,pangua kila kinachoendelea ktk ulumwengu wa roho,coz hicho umeonyeshwa ili uombe bt usipochukua hatua ya kuomba trust mi kitatokea km kilivyo,au kwa namna nyingine lkn something bad!

Unaona imerudia hiyo ndoto Mungu ameweka msisitizo hapo,
soma,Ayubu 33:14-18
Uone Mungu anasema nn kuhusu ndoto,na huwa anarudia.....

Kikitoka kitabu gani kinaingia ayubu
 
juzijuzi niliota nafanya mapenzi na mdada ninayemfahamu wa huko home bush, siyo kawaida yangu kuota nafanya mapenzi kama vile laivu, huyu mdada ananisumbuaga sumbuaga kutaka eti nimuoe, nilivyompigia simu nikamuelezea ndoto akasema na kusisitiza kwamba eti nimelala na jini, kwakweli toka niote hiyo ndoto nilikuwa siko sawa kabisa,maisha yangu ya kiroho kama yanapoa, kasi ya maombi ilipungua, lakini siku nyingine nikaota namtafuta na nikamkosa...ukweli kuna ndoto siyo za kupuuzwa
sijui nini kinaendelea hapo..naendelea na maombi
 
pole..
mm mtu wangu aliwahi niambia hivo kuwa anaota anasex na mtu hamfahamu.. kama vile live...
huwa ananikwaza sana ,sielewagi
 
juzijuzi niliota nafanya mapenzi na mdada ninayemfahamu wa huko home bush, siyo kawaida yangu kuota nafanya mapenzi kama vile laivu, huyu mdada ananisumbuaga sumbuaga kutaka eti nimuoe, nilivyompigia simu nikamuelezea ndoto akasema na kusisitiza kwamba eti nimelala na jini, kwakweli toka niote hiyo ndoto nilikuwa siko sawa kabisa,maisha yangu ya kiroho kama yanapoa, kasi ya maombi ilipungua, lakini siku nyingine nikaota namtafuta na nikamkosa...ukweli kuna ndoto siyo za kupuuzwa
sijui nini kinaendelea hapo..naendelea na maombi
Ni kweli ulilala na jini. Nia yake ni kukutenga na Nguvu ya Mungu. Na ndiyo maana nguvu zimepungua.
Angalia haya.
1.Tafuta mlango ni wapi hiyo ndoto imepata kibali cha kuja kwako na omba toba. Yawezekana unawaawazia sana wanawake,au unachat sana story A mapenzi, unangalia picha za matanio, au unajihushisha na mapenzi yasiyo kustahili.

Vunja roho hiyo kwa kuitaja. mf wewe uliyekuja jana ukafanyaapenzi nami nikuona navunja nguvu zako,najitenga nawe nk kemea hatarudi tena

Mlazimizeshe arudishe alichochukua kwako. mfono nyota, nguvu zako za kuomba,roho ya kumpenda Mungu nk
 
asante sana, nitafanyia kazi hili
 
Ndoto ni mlango wa kiroho ndani ya mtu
Ayubu 33:14-18 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; 16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, 17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; 18 Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.”
Ufungua masikio ya ndani ili MUNGU anaposema kupitia ndoto upate kusikia
Ukuwezesha kugundua kuwa MUNGU anasema nawe kwa kuthibitisha pale unapo pokea mafundisho yasiyo ya kweli ama yale ya kweli
MUNGU anaweza kukusemesha juu ya somo na mafundisho kupitia ndoto
Utuma ndoto katika nafsi ya mtu
Utumia mlango huu kusema na mtu.
Si kila ndoto inatoka kwa MUNGU
Kuna vyanzo 4 vya ndoto
1. Kutoka kwa MUNGU mwenyewe
Matendo 2:17 “Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.”
ROHO MTAKATIFU uweza kuachilia ndoto za MUNGU ndani ya mtu
2. Kutoka kwa shetani
Kumb 13:1-4 “1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.”
Usihishie tu kufurahi kwamba ulichotabiriwa ama alichosema nabii fulani kimetimia ama kimetokea
La msingi angalia na fuatilia baada ya kutokea hilo jambo je? hali yako ya kiroho imeongezeka? Iko pale pale? ama imeshuka?
Kama unafundishwa ama unatabiliwa kitu ama umeota na ukaona kimetimia lakini kimeua mahusiano yako na YESU kuwa mwangalifu sana
Wakati mwingine hata kuomba kwako kunashuka baada ya kutabiliwa kuwa makini sana maana za namna hyo hazitoki kwa MUNGU.
3. Uja kwa sababu ya shughuli nyingi
Muhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.”
4. Uja kwa sababu ya hali ya kiroho ya mahali ulipolala
Mwanzo 28:10-17 “10 Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. 11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. 12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. 13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. 14 Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. 15 Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. 16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. 17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.”
Waweza lala mahali ambapo pana upako na wengi hawajui kuomba ktk maeneo hayo hata kuyaweka wakfu
Maana BWANA ujifunua ktk ndoto ukilala maeneo hayo sababu ni madhabahu yake.
Ndoto zote za uhakika zina tafsiri zake kwa hiyo usizipuuze
Daniel 2:45 “45 Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti. ”
Ndoto ilikuwa ni hakika na tafsiri yake ilikuwa thabiti
Mwz 41:1-7, 32 “1 Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. 2 Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. 3 Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. 4 Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. 5 Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. 6 Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. 7 Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu. 32 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.”
Ayubu 33:14, 18 “14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 18 Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga.”
MUNGU usema mara ya kwanza kama hujaelewa ama umepuuza usema tena na tena kwa ndoto
Yeye ujaribu kukujibu maombi ulio nayo shida ya mtu ni kutoelewa maana ya ndoto hizo
Ndoto inaweza kutumika Kama mlango wa kujeruhi na kuvunja moyo wako na hali hiyo inaweza kujitokeza kwenye maisha ya nje
MIFANO:-
I. Kupitisha adhabu au ya MUNGU au ya miungu
Daniel 4:4-33 “4 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. 5 Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha……….10 Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; naliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana. 11 Mti ule ukakua, ukawa na nguvu, urefu wake ulifika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka mwisho wa dunia. 12 Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake. 13 Nikaona katika njozi za kichwa changu kitandani mwangu, na tazama, mlinzi, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka mbinguni. 14 Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake. 15 Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi; 16 moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake. 17 Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge. 18 Mimi, Nebukadreza, nimeiona ndoto hii; na wewe, Ee Belteshaza, eleza tafsiri yake, kwa maana wenye hekima wote wa ufalme wangu hawawezi kunijulisha tafsiri yake; bali wewe waweza, maana roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako. 19 Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako. ……. 31 Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako. 32 Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng'ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. 33 Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.”
Adhabu aliyoipata Nebukadreza ni kukaa na wanyama na kula majani kondeni kwa miaka 7
Aliona hayatimii alidharau na kuona ni ndoto tu kwanza ameota miezi 12 iliyopita na hakuona kilichotokea
. Ndoto inaweza kufungua mlango wa roho nyingine kuingia na kuharibu maisha yako
Ayubu 4:12-16 “12 Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake. 13 Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu. 14 Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote. 15 Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama. 16 Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake,
 
16 Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,”
Hali aliyokuwa nayo ktk ndoto ilifungua mlango na roho ya hofu ikamwingia mpaka kumtetemesha mifupa
Daniel 4:4-5 “4 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. 5 Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha.”
Alikuwa hana hofu mpaka alipoota. Ndoto ilifungua mlango roho ya hofu ikaingia ndani yake.
 
Hicho ulichokiota ni kati ya vitu vya kawaida sana kuongelewa na wanawake pindi wakaapo vibarazani,
sasa inawezekana mlishawahi kujadili siku nyingi zilizopita vitu kama hivyo ulivyoviota jana,
na kawaida ndoto huwa ni vile vitu ulivyoviwaza au ulivyowahi kukumbana navyo siku zilizopita,....
UMENIELEWA ora ?

ndoto inaweza kuelezea future pia!
 
twice nimeota Niko nyumbani (ikulu) kwa marais wawili. Nchi zao zinaanzia herufi Z na ziko Africa, nimepokelewa mapokezi makubwa sana.
Ndoto ni nyakati tofautitofauti.
Nini tafsiri yake kwa mujibu wa BIBLIA?
 
Ni kweli ulilala na jini. Nia yake ni kukutenga na Nguvu ya Mungu. Na ndiyo maana nguvu zimepungua.
Angalia haya.
1.Tafuta mlango ni wapi hiyo ndoto imepata kibali cha kuja kwako na omba toba. Yawezekana unawaawazia sana wanawake,au unachat sana story A mapenzi, unangalia picha za matanio, au unajihushisha na mapenzi yasiyo kustahili.

Vunja roho hiyo kwa kuitaja. mf wewe uliyekuja jana ukafanyaapenzi nami nikuona navunja nguvu zako,najitenga nawe nk kemea hatarudi tena

Mlazimizeshe arudishe alichochukua kwako. mfono nyota, nguvu zako za kuomba,roho ya kumpenda Mungu nk
Ni kweli ulilala na jini. Nia yake ni kukutenga na Nguvu ya Mungu. Na ndiyo maana nguvu zimepungua.
Angalia haya.
1.Tafuta mlango ni wapi hiyo ndoto imepata kibali cha kuja kwako na omba toba. Yawezekana unawaawazia sana wanawake,au unachat sana story A mapenzi, unangalia picha za matanio, au unajihushisha na mapenzi yasiyo kustahili.

Vunja roho hiyo kwa kuitaja. mf wewe uliyekuja jana ukafanyaapenzi nami nikuona navunja nguvu zako,najitenga nawe nk kemea hatarudi tena

Mlazimizeshe arudishe alichochukua kwako. mfono nyota, nguvu zako za kuomba,roho ya kumpenda Mungu nk

Pastor Emmanuel Munguatosha Mtui MUNGU akurehemu zaidi na zaidi
 
Back
Top Bottom