Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Unaikumbuka barcelona ya Xvavi,Iniesta,Messi,Pedro na David Villa? Hawa jamaa ilikua ni kosa la jinai kuwatangulia kuwafunga. Mpira unahamia golini kwako huku goli zikimiminika km maji.Muulize Sir. Alex atakusimulia kwa kina. Kibongobongo ndo naiona Simba ya sasa ya kiwango hicho.Azam walipofunga tu lile goli lao ndo ilikua mwanzo wa kufungwa. Niliwaona ghafla wachezaji wa Simba wakibadilika na kuwa wakatili wasio na huruma.Dilunga akawa mtu mwingine kabsa! Sheboub ndo akawa malaika mtoa roho. Kila mara Azam walipojaribu kujikongoja ndani dk 2 au 3 Simba walipigilia msumari mwingine na hivyo kuwakatisha tamaa kabsa wapinzani wao. Jana Azam hawakua na chakufanya zaidi ya kutulia na kusubilia mpira uishe. Tuache unazi wa kinafiki Simba ipo vzr jamani!