Janeth Mahwanga Achangia Wizara ya TAMISEMI Agusia Mikopo ya 10%

Janeth Mahwanga Achangia Wizara ya TAMISEMI Agusia Mikopo ya 10%

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. JANETH MAHAWANGA ACHANGIA WIZARA YA TAMISEMI MIKOPO YA 10%

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Elias Mahwanga amechangia Wizara ya TAMISEMI kwa kuiomba Serikali kuangalia upya utaratibu mzuri wa mikopo ya 10% ambayo inatolewa kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

"Tunafahamu kuwa mikopo hii sasa hivi imesimamishwa na kuandaliwa utaratibu mzuri wa kupitia kwenye Taasisi za kifedha."

"Pesa nyingi zimepotea kutokana na sababu mbalimbali kama, walengwa kutokuwa na elimu ya kutosha, Wasimamizi kutokuwa waaminifu hali iliyopelekea kuwa na utitiri wa vikundi hewa." - Mhe. Mahwanga

Mhe. Mahwanga ameiomba Serikali kuangalia mapungufu yote hayo na kuyafanyia kazi huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona sasa kuna haja ya mikopo hii kutolewa kwa kuzitumia Taasisi za kifedha hali itakayosaidia kuondoa tatizo la vikundi hewa lakini pia kuziba mianya ya upotevu wa hizi pesa.

Pia, Mhe. Mahawanga ameiomba Serikali kukaa na Taasisi za kifedha kuweka mifumo mizuri ambayo haitawaumiza wakopaji, lakini itatoa pesa hizi kwa watu sahihi.

Vile vile, Mhe. Mahawanga ameiomba Serikali iwafikirie Vikundi vya huduma ndogo za fedha (Vicoba) kuwa sehemu ya wanufaika kwani wao tayari wana pesa zao wanazonunua hisa kila mwezi hivyo wanauwezo wa kukopeshana wenyewe kwa wenyewe wakipewa pesa hizi watafanya mambo makubwa kama kufungua makampuni na Viwanda vitakavyopelekea ajira kwenye jamii yetu. Na Wanavicoba wanauwezo wa kurudisha marejesho ya mikopo hii.

Lakini pia, Mhe. Mahawanga ameiomba Serikali kwenye majengo yote ya biashara yaliyojengwa na yanayoendelea kujengwa kutengwe maeneo ya akina Mama Lishe wanaofanya biashara ya chakula kwani wanasahaulika ingawa hao wafanyabiashara ndio wateja wao wa chakula. Nao wanamikopo na marejesho wanategemea biashara yao wakalipe marejesho hapo ndio sehemu sahihi ya biashara yao.

Mwisho, Mhe. Mahawanga ameiomba Serikali kwenye ajira mpya zilizotangazwa hasa kada ya Walimu wawafikirie walimu ambao wapo mashuleni wanajitolea, wahakikishe wanapata kwanza wao ajira kabla ya wengine.

#TishaMama
#MamaVicoba
#ItazameDarKiutofauti
#Kaziiendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-18 at 14.20.30.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-18 at 14.20.30.jpeg
    44.2 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2023-04-18 at 14.20.31(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-18 at 14.20.31(1).jpeg
    37 KB · Views: 8
Back
Top Bottom