Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,828
- 165,667
Zikiwa zimebaki takribani siku saba kabla ya siku 30 za kufunga vyuo na mashule zilizotolewa na serikali kuisha,ni vizuri serikali ikatoa tamko mapema kama inaongeza siku au inaruhusu vyuo na mashule kufunguliwa ili kuwawezesha watu, wakiwemo wazazi na wanafunzi, kujipanga angali mapema.
Sababu za kuitaka serikali itoe tamko mapema ziko nyingi ila mojawapo ni kuwawezesha wanafunzi wa vyuo kujua kama walipe kodi za nyumba au waache kwani kuna uwezekana wa watu kulipa kodi alafu vyuo visifunguliwe ikiwa ni hasara kwao na faida kwa wenye nyumba.
Ikumbukwe wakati serikali inatoa tamko la kufunga vyuo na mashule kwa siku 30, baadhi ya wanafunzi walikuwa likizo huku baadhi yao wakiwa wameacha vitu vyao katika sehemu walizokuwa wamepanga na sasa wanatakiwa kulipa kodi ila mtihani unakuwa ni unalipaje kodi wakati hujui kama vyuo vitafunguliwa au serikali itaongeza muda zaidi.
Naamini hili la wanafunzi kutakiwa kulipa kodi huku wakiwa hawaelewi kama watarudi vyuoni baada ya hizo siku 30 kukamilika au muda utaongezwa, ni mojawapo tu ya changamato miongoni mwa changamoto nyingi zinazowakabili wanafunzi, wazazi,walezi,vyuo.mashule,n.k, kutokana na zuio hili lililotolewa na serikali kwa nia njema tu.
Kwa mfano,ni wazi hata mashule na vyuo navyo vinahitaji taarifa za mapema ili waweze kujipanga kupokea wanafunzi bila kusababisha usumbufu wowote kwao na kwa wanafunzi wao.
Hivyo, tunaiomba serikali itoe tamko (ikiwezekana hata kesho) ili watu wajipange kwani tunaamini serikali mpaka kufikia sasa ina taarifa za kutosha juu ya mwenendo mzima wa ugonjwa huu humu nchini, taarifa zinazoweza kuwafanya watoe maamuzi bila kuhitaji muda zaidi.
Waheshimiwa Wabunge, tunaomba mtusaidie kufuatilia swala hili Bungeni.
Wazungu wanatuambia: The ealier, the better.