Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’

Baada ya wiki moja wakiwa kwenye amri ya kutotoka nje hali itakuwa mbaya zaidi kwa sababu hata kile kidogo walichonunua kwa pesa kidogo walizonazo kitaisha.

Kwa nchi zetu za Afrika unaweza kutoa amri hiyo ya kukaa ndani iwe kwa siku moja au mbili lakini siyo kwa zaidi ya wiki moja!

..kulazimisha watu wakae ndani unaweza kusababisha MACHAFUKO na MAASI.
 
Mkuu, revisit your details. Kwa jinsi nilivyoiona hiyo barua ni kuwa Prof anajulisha watu wa taasisi yake kuwa kuna mtu A hatakuwa ofisini hivyo mtu B atakaimu nafasi yake ktk hiyo idara kipindi huyo mhusika hayupo. Simple like that.

Unless uwe haujui mambo ya office au hujawai kukaimisha au kukaimishwa.
Ulifanya haraka tu kui-quote lakini ulii-quote wakati nami na-edit kuzungumzia hoja ya kipi hasa alilaumiwa JPM! Thanks anyway
 
..kuwaweka watu majumbani huku huna CAPACITY ya kuwapima na " kuwachomoa" waathirika na kuwahifadhi haisaidii chochote.

..Magufuli hakuna options zozote zile. Kuwaambia wananchi waongeze MAOMBI amekuwa mkweli.

..Wananchi wasio na maji salama ya kunywa utawaambiaje waoshe mikono mara kwa mara, tena watumie na sabuni? It is unrealistic.
I doubt kama atakuelewa... anyway, long time no see!!!
 
ataanza zanzibar atafuata mtanganyika kufunga. wiki ijayo tujiandae kwa mengi!!
 
Ila huyu mzee namsifu hapa tu. Kwa kweli kwa huku Africa swala la watu kubaki nyumbani ni haliwezekani. Tusidanganyane.

Huko Kenya kama hivo hali tete imebidi wabadili msimamo.
Uganda hali ngumu mpaka wanachapana bakora.
Hivi mimi uniambie nikae nyumbani na hela ya kula sina? Serious??
Tuna tatzo mkuu

Kitabibu haikupaswa tuzurure,vifaa tunavyotumia kwa ajili ya hili jambo ni duni
Uangalizi wetu ni dhaifu sana
Labda kibiolojia tuna bahati hayujadhurika


Kumbuka wadau wetu wa kiuchumi ndio waathirka wakubwa,wao kwa wao hawakaribiani sababu ya tahadhari

Wanapoona tunazembea katka hili amini itatupa wakati mgumu kutoka nje na kupokelewa
Majirani tu hawatupokei

Anayoamua kiongozi wetu tunapaswa kuyatafakari mno


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu hasa wanasiasa kutaka Rais Magufuli na serikali yake wafunge mipaka ya nchi na kutoa tamko la kuwataka/kuwalazimisha wananchi wabakie majumbani mwao ili ‘’ kupambana’’ na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 yasisambae nchini.

Mashinikizo yanayotolewa kwa Rais Magufuli unaweza kuyaona niya msingi kama utadhani mazingira ya Tanzania kiuchumi na kijamii ni sawa na mazingira ya ''Nchi za Magharibi'' ambazo zinatumia mbinu hii.

Ni ukweli kuwa, Mazingira ya kiuchumi na kijamii nchini yako tofauti sana na mazingira ya nchi za Magharibi na kwa msingi huu, haiwezekani mbinu za kupambana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 yakafanana na nchi hizo.

Mwanasiasa wa Marekani aitwaye Donald Rumsfeld aliwahi kusema, ‘’You go to war with the army you have, not the army you might want or wish to have at a later time.”

Kwa kiswahili ambacho sio sanifu, Donald Ramsfeld alisema, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’.

Kwa mantiki hii, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi la kiuchumi na kijamii alilonalo na sio ambalo baadhi ya wanasiasa wanataka liwepo wakati halipo.

Kwenye suala la kiuchumi, nchi za Magharibi zimeweza kufanikiwa kufunga mipaka na kuwalazimisha wananchi wake wabakie majumbani mwao kwa masaa 24 bila kutoka nje kwa sababu mazingira ya kiuchumi yanaruhusu kufanya hivyo. Kwa sasa wananchi wote wa nchi hizo pamoja na kwamba hawafanyi kazi lakini serikali imeamua kuwalipa mishahara na pesa za kujikimu na maisha wananchi wake wote mpaka pale watakapoanza kufanya kazi tena. Hata malipo rehani (mortgage) kwa sasa yamebebwa na serikali.

Kwa upande wa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ kama Tanzania, serikali haiwezi kubeba jukumu la kiuchumi kama zilivyofanya nchi za Magharibi kwa sababu haina uwezo huo na kama italazimisha wananchi wake wabakie majumbani basi tutegemee machafuko nchini au familia nyingi kufa kwa njaa hasa zile zinazoishi kwenye maeneo ambayo bila kutoka ‘’nje ya nyumba’’ familia haiwezi kupata chakula cha siku. Kwa nchi za ‘’dunia ya tatu’’ ikiwamo Tanzania, binadamu anaishi kwa jasho/nguvu zake lakini kwa ‘’nchi za Magharibi’’, binadamu anaweza akaishi bila jasho/nguvu zake.

Tanzania vile vile ni ''lango kuu'' na mkondo wa usafirishaji katika nchi karibu nane ambazo hazina bahari.

Haishangazi kwa sasa tumeanza kuona wananchi wakipigwa risasi katika nchi za Rwanda na Uganda kwa sababu wamekataa kutii amri ya kubakia majumbani mwao kutokana na ukweli kuwa kubaki ndani pia ni kukaribisha kifo kwa njaa. Ni bora watoke nje wakajaribu bahati ya kutafuta chakula kuliko kubaki majumbani mwao. Nadhani baada ya wiki moja hali itakuwa mbaya zaidi.

Huko Kenya, Rais Kenyatta amegundua makosa na kwa sasa amebadili msimamo wake ambapo badala ya amri ya kuwataka wananchi wabakie majumbani mwao kwa saa 24 kwa sasa watafanya hivyo kuanzia majira ya saa 11 za jioni hadi saa 11 alfajiri. Hii mbinu inashangaza!

Kwenye suala la kijamii, nchi za Magharibi zimefanikiwa kutokana na ukweli kuwa jamii zake zinaishi maisha ya ‘’kipweke’’. Ninaposema kipweke nina maana mazingira ya hali ya baridi na kazi yamewafanya wananchi wawe wanaishi maisha ya kujifungia ndani hata wakitoka kazini. Wenzetu hawana hii dhana ya ‘’kwenda kwenye kijiwe’’ kupiga stories au kwenda kwa ndugu au rafiki bila kutoa taarifa.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo mikusanyiko ya kijamii na kifamilia ni sehemu muhimu ya maisha, ni vigumu sana kwa serikali kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wengi kama itatoa amri ya kuwataka wananchi wasifanye hivyo na badala yake wabakie majumbani mwao kwa saa 24.

Nimalizie kwa kusema, sio kwamba alichokifanya Rais Magufuli na serikali yake ni ‘’mwarobaini’’ wa kupambana na Janga la COVID-19. La hasha! Njia wanazotumia nchi za Magharibi zinaweza kuwa ni nzuri zaidi lakini kwa mazingira ya Tanzania na nchi za ‘’dunia ya tatu’’ haiwezekani kutokana na hali halisi ya kiuchumi na kijamii.

Kama alivyosema Donald Ramsfeld, ‘’ Unaenda vitani na jeshi ulilonalo, sio jeshi ambalo ungetaka au ungetamani kuwa nalo baadaye’’. Kwenye janga hili la COVID-19, Rais Magufuli ameenda vitani na jeshi alilonalo!
Huu mchezo wa COVID-19 bado sana hata half time bado
 
MsemajiUkweli ,

..Tz haina CAPACITY ya kuwapima, kuwahifadhi, na kuwatibu, wagonjwa wa Corona ikiwa ugonjwa huo utaingia hapa nchini.

..Kutegemea msaada wa serikali hii ni UENDAWAZIMU. Hivyo basi ni bora kumuomba MUNGU atuepushe kwasababu hatuna serikali ya kuitegemea.

..Uamuzi wa Raisi ulikuwa very simple. He does not have the options ambazo mataifa mengine yanayo. Uamuzi hapa ni KUSUBIRI tuone nini kitatokea. Kwa wale wenye imani wanatakiwa KUSALI.

..Hatuna vifaa, hatuna wataalamu, hatuna fedha. Lakini tunaweza KUSALI.
Pamoja na hayo, tungejifungia ndani ndo tungekufa zaidi kuliko hiyo covd-19.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi Popote sijawahi kusuport ujinga wa kufunga mipaka ila hoja yangu ilikuwa kuweka vipimo mipakani kwanza ukifungia watu ndani binafsi siwezi kushinda ndani kulingana na mazingira ya kazi.

Tukikukuta una ugonjwa mpakani unarudishwa ulikotoka fasta kufungia watu ndani itabidi serikali iwalipe je tunaweza binafsi nikikaa ndani naweza poteza pesa nyingi sana na vijana wangu wanaonisaidia kazi watakwama na kukosa chakula tuendelee kuchapa kaz ugonjwa utapita 2.
 
Back
Top Bottom