SoC03 Janja janja ya China kupata faida maradufu Yani (super profit)

SoC03 Janja janja ya China kupata faida maradufu Yani (super profit)

Stories of Change - 2023 Competition

fundi radio

Member
Joined
Apr 2, 2023
Posts
52
Reaction score
95
Kwa Hapa nchini Tanzania ambayo Ili kuwa na mfumo wa kijamaa, kutoka TANU mpaka CCM.

CCM Bado Ina urafiki na nchini ambazo zilikuwa na mfumo wa kijamaa kama washirika wake wakaribu. Na china (ujamaa) inaitumia fursa hiyo vizuri sana,Kwa kujiweka karibu sana na viongozi waandamizi wa chama tawala (CCM).

Hali ni tofauti Kwa nchi za magharibi (kibepari) wao wakiwa na urafiki wa watu wa Chache kwenye chama tawala na wa vyama vya upinzani,
lakini China ina mafungamano ya karibu sana na chama tawala kiasi Cha kuwa na ushawishi mkubwa.

Kisiasa:
Mafungamano hayo :
I) chama tawala Cha china Kila mara kime kuwa kikitoa misaada ya kifedha na rasilimali mbalimbali Kwa ajili ya Chama Cha CCM.

ii) chama tawala cha china kimekuwa kikitoa mafunzo ya kiutawala na uongozi Kwa viongozi mbalimbali wa chama Cha CCM. (scholarship).

iii). Na Sasa wamejenga chuo Cha uongozi hapa nchini Tanzania, bila shaka kwenye hayo masomo ya uongozi yatakuwa yameandaliwa na Serikali ya China Kwa Falsafa za kijamaa zaidi, ya chama kimoja kutawala pekee.
IMG_20220219_214120_648.jpg

Ni Bora wangeongeza masoma kama ujasiriliamali, uchumi wa kijani,bluu,tehama Katika utumishi, diplomasia, Ili kuleta tija Kwa viongozi wanao tahiniwa.

iv). China kuisadia Tanzania kwenye maswala ya ulinzi na usalama.

Je nchi yetu inahitaji sera za kijamaa ,(chama kimoja), Ili iweze kujiletea maendeleo?

HAPANA, Tanzania inahitaji viongozi watakao fanya kazi Kwa moyo wa dhati kabisa ikiwa pamoja na kusimamia katiba na Sheria za nchi yetu.

a). China kuandaa viongozi watakao kuwa na falsafa za kijamaa zitakazo wasaidia kuwa karibu na viongozi wa chama tawala, kumbuka siku zijazo ,hato chaguliwa kiongozi wa CCM ila awe amepitia kwenye hicho chuo.

Matokeo ya china kujiweka karibu sana na viongozi wa sekretaiti ya Chama tawala (NEC), kama ifuatavyo

Kiuchumi.
Kandarasi za ujenzi wa barabara,madaraja, majengo makubwa, kandarasi za miundombinu ya nishati, ulinzi Kwa asilimia kubwa anachukua china.

Mzunguko wa fedha za kigeni zinaangukia mikononi mwa china.

Fedha za mikopo nafuu Kwa ajili ya Miradi ya maendeleo kutoka IMF, world Bank, UK, AFDB, ufaransa, EU , kandarasi zote anapewa China,
Kumbuka hizi nchi wafadhili wana viwanda vyao na mitaji huko nchini china .

ambapo baadae tunauziwa bidhaa kutoka china, Na Bado Tena china anachukua kandarasi zote za Hawa wafadhili Kwa hiyo mzunguka wa fedha za kigeni unazungukia upande wa china pekee.

Na kupelekea china kupata faida maradufu , Yani (super profit)🤑

Changu changu chako changu (win win)

Ni tofauti na nchi za magharibi mfano USA, UK, EU wanapotoa misaada, wanazipa fedha Serikali kuu au kuanzisha programu za maendeleo ya jamii nchini.ili kuleta uchumi jumuishi kwenye jamii.

Serikali ya China ikitoa misaada ya kifedha Kwa ajili ya maendeleo asilimia zaidi ya 95% ataitekeleza yeye mweyewe, Kwa hiyo mzunguko wa fedha bado unabaki upande wake TU yani.

Mfano mradi wa Bomba la gesi la mtwara mpaka dar es salaam,china alitoa mkopo wa takribani Dola bilioni $ 1.2, na akautekeleza yeye mweyewe na kutuachia deni lenye riba , ambayo sisi raia hatuijua hilo deni Kwa Sasa limefikia kiasi Gani.

Gesi inapita kwenye hiyo Bomba bado haitumiki kikamilifu , kwenye kuzalisha umeme wa kutosheleza nchini, pia gesi ,bado hatujaanza kuunza nje ya nchi , Kwa hiyo bado tuko kwenye hasara kubwa.

Ulanguzi

Kuwekeza kwenye kamari, mpaka vijijini watu wanatapeliwa ,na Serikali inakaa kimya, huu ni uwekezaji Gani wahovyo namna hii, walalahoi na wavuja jasho na wapiga kura wa Chama tawala ,wanakamuliwa mpaka senti zao za mwisho.
images (3).jpeg

Faida inayopatikana mfano ikiwa ni laki mchina anachukua zaidi ya asilimia 90%, fikiria Kwa jiji la dar mchina anakusanya maokoto kiasi gani Kwa mwezi.🤑

Kwanini wasianzishe miradi mbalimbali ya kilimo ambayo yana mahitaji nchini kwao kama, muhugo,mtama, nyama ya nguruwe , na Kila upande uka faidika (win win).💪

Kukamatwa Kwa raia wa China wakijihusisha na uuwaji wa tembo na faru na usafirishwaji wa meno ya tembo, pembe za ndovu, na pembe za faru nje ya nchi,
images (1).jpeg

bila Shaka waliona Tanzania ni shamba la Bibi, je waliwezaje kufanikisha kufanya huu ujambazi Kwa kiasi kikubwa hicho na Kwa muda mrefu,

bila vikosi vya usalama kujua, mpaka zilivyoanza kelele za Taasisi za kimataifa kuhusu ujangili , Ndio Serikali ikaamua kujitutumua kuondoa aibu.

Huku Wenzao USA, UK EU, wakitoa misaada Kwa ajili ya kulinda wanyama pori na hifadhi zake.
Screenshot_20230727-210827.jpg


Je hii ni ( win win) au (janja janja)?

Kutokuwepo Kwa makubaliano ya kibishara ya kimkakati ya maendeleo Kwa muda mrefu.

Mfano wa (win win) (janja janja) hii sio mkataba bali ni makubaliano TU ya kirafiki (mtego) ya kufanya Biashara baina ya nchi mbili Kwa makubaliano Fulani.

Ambapo Kila nchi Inakuwa na uhuru wa kufanya Biashara.

Kwa hiyo mwenye kisu kikali ndio atakaye kula nyama, hii ilipelekea mpaka wachina wakaja kuuza yeboyebo kariakoo,
images.jpeg


Ila Kwa sisi wa Tanzania hatuna uwezo na Bidhaa za kutosha za kuuza China.

Ni tofauti na AGOA wa USA ,ni mkataba wa makubaliano rasmi inaoeleweka kimkakati baiana ya nchi husika,

mfano mkataba wa AGOA , ambapo Tanzania iliridhia kusaini na kupata fursa ya kuuza mazao yake ya chakula na Bidhaa zingine bila ushuru wa forodha kwenda nchini marekani.

Je kwanini mpaka leo Tanzania hatuja Saini mkataba wa EPA?

Je china Yuko nyuma yake kuzuia EPA isisainiwe, maana Yuko karibu na viongozi wa chama tawala.
Maana wanajua Kama Tanzania tukisaini mkataba wa EPA, watanzania watanunua kwa wingi,Bidhaa za ulaya ambazo zinaaminika Kwa ubora duniani, na China kukosa soko la kuuza Bidhaa zake.

Kulingana na repoti ya wizara ya fedha ya mwaka 2022, deni la China nchini Tanzania lilifikia Dola bilioni 11.6,ikijumuisha mikopo ya kibiashara na maendeleo.

Ushauri:
Ndugu zetu washirika wa maendeleo USA, UK, EU, IMF and world Bank, mnapotoa misaada Kwa ajili ya maendeleo nchini Tanzania,itekelezeni wenyewe na Serikali pasipo nchi nyingine, katikati (third party) kuja kuikamilisha hiyo Miradi.

Pia Chama tawala kisiegemee upande mmoja TU, upande ambao anapata kuungwa mkono Kwa chama kimoja kutawala, ukiukwaji wa haki za binadamu na demokrasia , mizania ikae sawa.
 
Upvote 8
Nchi yeyote duniani haiwezi kupiga atua kw akutegemea misaada na mikopo tena yenye riba kubwa,
Kuna haja kwa nchi kama Tz kujiimarisha kwanza kisha kufungua mipaka yake, haitoshi kulalamika ukijua mwenzako amekuzid shart umkwepe kwanza ndio ujipange upya, ama utafute baadaye pakutokea
Si Tz pekee imezidiwa hilo hata ulaya kwa sasa moto ni huu huu kutokea china, ajira za watu zinanyang’anywa usiku na mchana.
China ina cheap labor kuliko nchi yyte duniani, na bado wanauwezo mkubwa wa uzalishaji!
Kuwatukana wachina kwamba wanyonyaji ni unawakosea sana, wanapoteza pesa nyingi kwenye uwekezaji wa kimataifa, mfano hayo madeni wanayokopesha ni ngumu kulipika na serikali nyingi za africa zina roop hol pakutokea!
Hata marekani kwenyewe hakuna viwanda vya uzalishaji kwa sasa hutegemea china kuzalisha na kuuza America!

Hakuna nchi inayoshindana na china kwa uzalishaji ulaya! Wametuzidi sharti tujipange wasituumize zaidi,
Huwezi kumkwepa mchina na mikataba ya win win hata marekani anahangaika hilo

Mpaka sasa china inaidai Marekani kiasi cha dolla $859.4 billion ni unkwepable debt

Huku africani zaidi ya dollar 73 billion na $ 9 billion private sectar sasa zinalipikaje?

"Huku africani zaidi ya dollar 73 billion na $ 9 billion private sectar sasa zinalipikaje"

👆👆 Hapo Kwa Africa deni ni kubwa Zaidi.

Alafu unatakiwa uelewe Mimi nimefanya uchambuzi jinsi china inavyofanya business tz, ambapo ina reflect nchi za Africa.

Sio kwamba na ikandia china, ila nimeelezea kinachofanywa na China in tz including Africa
 
various unfair trade practices that China has been accused of using to gain an unfair advantage over its competitors. These practices include dumping, subsidies, intellectual property theft, state-owned enterprises, and currency manipulation.


Here are some specific examples of how China has used these practices to make super profits;-


Dumping: China has been accused of selling goods below cost in foreign markets in order to drive out competition. This has led to job losses in the United States and other countries.


Subsidies: China has provided billions of dollars in subsidies to its companies, which has helped them to lower their costs and compete more effectively.


Intellectual property theft: China has been accused of stealing intellectual property from foreign companies, such as patents and trade secrets. This has cost foreign companies billions of dollars in lost revenue.


State-owned enterprises: Chinese state-owned enterprises (SOEs) often receive preferential treatment from the Chinese government, such as access to cheap loans and government contracts. This gives SOEs an unfair advantage over private companies.


Currency manipulation: China has been accused of keeping its currency, the yuan, undervalued, which makes Chinese exports cheaper and imports more expensive.


This has hurt US exporters and helped Chinese exporters.


The use of these practices by China has had a significant impact on the global economy. It has led to job losses in the United States and other countries, and it has hurt the competitiveness of businesses in these countries.
 
Dumping: In 2017, the United States accused China of dumping solar panels in the US market. The US government imposed tariffs on Chinese solar panels, which helped to protect US solar panel manufacturers.


Subsidies: China has provided billions of dollars in subsidies to its steel industry. These subsidies have helped to make Chinese steel cheaper than steel from other countries, which has hurt steel producers in the United States and other countries.


Intellectual property theft: China has been accused of stealing intellectual property from a variety of companies, including Apple, Microsoft, and Samsung. This has cost these companies billions of dollars in lost revenue.


State-owned enterprises: Chinese SOEs are often given preferential treatment by the Chinese government, such as access to cheap loans and government contracts. This gives SOEs an unfair advantage over private companies.


Currency manipulation: China has been accused of keeping the yuan undervalued, which makes Chinese exports cheaper and imports more expensive. This has hurt US exporters and helped Chinese exporters.
 
Kama pesa zilizo tumika kujenga pomba la gesi zingetumika kujengea mitambo ya kuchakata umeme utokano na gesi basi tz🇹🇿 umeme ungekuwa wa uwakika, na chenchi ingebaki.

SEMA msoga gangs ni wa binafsi Sana wakaona ni Bora Wao wapate cha juu wagawane na wachina.

Nina wasiwasi Sana na akili za viongozi wa Tanzania
 
NIMEFURAHI SANA KUONA SERIKALI IMELIFANYIA KAZI POST YANGU HII . NAMI NIMEKUWA MIONGONI MWA WATU WALIO NA MCHANGO + KWA 🇹🇿.

HASA KWENYE SWALA LA WAKANDARASI WAZAWA KUPEWA ZABUNI ZA KUTOSHA.

KAZI IMEBAKI KWENU SASA WAKANDARASI WAZAWA KUTEKELEZA MIRADI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA .

👇👇👇
Rais Samia ameamua Kuwabeba Wakandarasi wazawa mabegani mwake Ili kuwafanya matajiri ambao watakuwa injinia ya uchumi Nchini.

Hayo yamebainishwa na Waziri Bashungwa wakati wa kikao cha Mashauriano cha kutatua changamoto za Wakandarasi wa ndani.

Katika kufanikisha azma hiyo ameamua kufanya yafuatayo;

1/ Kupandisha thamani ya Miradi ambayo inaweza kutekelezwa na Wakandarasi wa ndani kutoka Bilioni 10 Hadi Bilioni 50.

2/ Kubadili Sheria ya Local Content ambayo iliwanyima fursa ya kuwa main contractor hivyo Wakandarasi wa ndani watakuwa na uwezo wa kuomba kazi na ku sub Kwa Wakandarasi wageni.

3/ Serikali itapunguza na kufuta vigezo vilivyokuwa vinawanyima fursa Kwa visingizio vya hawana uwezo

4/ Serikali itaingia ubia na Mabenki Ili yatoe uwezeshaji wa kifedha Kwa Miradi ya Wakandarasi wa ndani Kwa utaratibu maalumu Ili kuwawezesha watekeleze kazi walizopewa.

5/ Kutoa upendeleo maalumu Kwa wakandarasi wanawake, Vijana na Vikundi Kwa kuwatengea Asilimia 30% ya kazi zote.

6/ Kuandaa Utaratibu wa kuwakuza Wakandarasi wa ndani Kwa kuwajengea uwezo wa kitaalamu na kifedha Ili waweze kuvuka mipaka.

Kwa Hatua hizo Samia anakuwa Rais wa kwanza kutekeleza Kwa vitendo azma ya Waasisi wa Nchi hii ya kuhama kutoka kwenye uhuru wa bendera na kuwa na uhuru wa Kiuchumi.

Inasikitisha sana kuona Asilimia 61% ya thamani ya Miradi yote Wanapewa wageni na Asilimia 39% tuu ndio wakandarasi Wazawa.Hao wageni wako 800 na Wazawawako zaidi ya 14,000.

MIKAKATI YA RAIS SAMIA KUINUA MAKANDARASI WAZAWA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, anataka kuona ushiriki mkubwa zaidi wa Makandarasi wazawa katika kazi za utekelezaji wa ujenzi wa miradi nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa leo tarehe 21 Novemba, 2023 katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Makandarasi wazawa na Washauri elekezi wa ndani jijijini Dodoma, kujadili nafasi yao katika utekelezaji wa miradi.

Bashungwa amesema Wizara ya Ujenzi, kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), inaendelea kutenga miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara kwa ajili ya Makandarasi wa ndani kwa lengo la kuwasaidia Makandarasi hao kukua na kupata uzoefu.

“Katika mwaka wa fedha 2023/204, jumla ya miradi minne ya barabara yenye urefu wa kilometa 50 kila moja zimetengwa kwa ajili ya makandarasi wa ndani tu, kwa hiyo kilometa 200 zitajengwa na wazawa, hii ni fursa kubwa ya kuwasaidia makadarasi”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amesisitiza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 Jumla ya kilometa 20 za barabara zimetengwa kwa ajili ya makandarasi wanawake, ambapo zitagawanywa katika vipande vya kilometa tano tano, na kazi hizo zitashindanishwa kwa makampuni ya wanawake peke yao, hii inafanya jumla ya km 220 kujengwa na makandarasi wazawa kwa mwaka 2023/24.

Bashungwa ameongeza kuwa kazi za matengenezo ya barabara zinazosimamiwa na TANROADS kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara zenye thamani ya Shilingi Bilioni 600 zitatekelezwa na Makandarasi wa ndani tu katika mikoa yote 26 nchini.

“Katika Mwaka wa fedha 2023/2024 kazi zote za matengenezo ya barabara kwa mikoa yote 26 nchini, Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kutekelezwa na Makadarasi wa ndani”, amesema Bashungwa.

Halikadhalika, Bashungwa amefafanua kuwa Sheria ya Ununuzi wa Umma imefanyiwa marekebisho kwa kuongeza kiwango cha thamani ya mradi ambao utatekelezwa na Makandarasi wa ndani tu, bila kushindanishwa na Makandarasi wa nje.

Dhima kuu ya mkutano huu ni kujadili na kudadavua mikakati mbalimbali kati ya Serikali na wadau wa Sekta ya Ujenzi kuhusu kuwajengea uwezo makandarasi wazawa na washauri elekezi.

Screenshot 2023-11-23 115210.png
 
Active Naona baadhi ya picha nilizo ziposti kwenye huu Uzi mmezi Hide images 1,3 , naombeni sababu za kuzi hide?

Niko nasubiri majibu
 
▪️BASHUNGWA ATOA SIKU 7 KWA CRG7 KUJA NA MPANGO KAZI WA KUKAMALISHA MIRADI.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametoa siku saba kwa Mkandarasi Kutoka China, China Railway Seventh Group Ltd (CRG7) kuwasilisha Wizarani mpango kazi wa miradi mitano anayoitekeleza hapa nchini kutokana na utekelezaji wa miradi yote kusua sua na kuwa nyuma ya muda wa mikataba.

Ametoa maelekezo hayo leo tarehe 01 Disemba 2023 wakati alipokutana na Uongozi wa juu wa Kampuni hiyo, ulioongozwa na Mkurugenzi mkuu Msaidizi wa Kamapuni ya CRG7 Kutoka China, ndugu Xianyang Dong.

Bashungwa amemtaka Mkurugenzi mkuu huyo wa CRG7 kuhakikisha anawasilisha kwake Mpango kazi wa kila Mradi na namna alivyojipanga kukamilisha, kutokana na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi yote mitano waliyopewa kujenga hapa nchini.

Ameeleza kuwa Mkandarasi CRG7 anatekeleza miradi mitano ambayo ni Ujenzi wa Kiwango cha lami barabara ya Amanimakoro - Ruanda km 35 iliyopo mkoani Ruvuma ambapo utekelezaji wake ulitakiwa kuwa asilimia 92 lakini sasa umefikia asilimia 24.

Bashungwa ameeleza mradi mwingine ni ujenzi wa Kiwango cha lami barabara ya Sanzate - Natta km 40 iliyopo mkoani Mara ambapo walitakiwa kuwa asilimia 99 lakini sasa hivi wamefikia asilimia 41.

Aidha, Ameeleza Ujenzi wa Kiwango cha lami barabara ya Kibaoni - Mlele junction km 50 iliyopo mkoani Katavi ambapo walitakiwa kuwa asilimia 26 lakini sasa wamefikia asilimia 12.

Amebainisha miradi mingine ambayo utekeleaji wake haujaanza ni barabara ya Nyamwage - Utete km 33.7 mkoani Pwani, Ujenzi wa Daraja la mpiji chini na barabara unganishi ya km 2.3 vilivyopo mkoa Dar es Salaam.

Kadhalika, Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kuondokana na hali ya kutoa miradi mingi ya ujenzi kwa Mkandarasi mmoja, jambo linalosababisha miradi kushindwa kutekelezwa kwa wakati kulingana na mikataba.

Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inayongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan haitamvumilia Mkandarasi yoyote anayeshindwa kuteleleza miradi kwa wakati, Kutoka na sababu zozote ambazo zinakwamisha Utekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
 
Yan china anapewa Miradi mingi ya ujenzi mpaka ina muelemea, Yan daa👆😂💰
 
Back
Top Bottom