Geneina (Al-Junaynah), Sudan Magharibi, watu 773 (wengi vijana, wanawake na wazee) wameuwawa kwa kuchinjwa na Janjaweed (Sudanese Arab militia group). Nyumba zimechomwa moto, wengi wametekwa.
JANJAWEED (devils on horseback - mashetani juu ya farasi) ni washirika wa kimkakati wa mtandao wa wanamgambo katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini unaojumuisha HAMAS na HEZBOLLAH.
Huwezi kusikia ni habari kubwa Duniani. Huwezi kusikia waafrika na watanzania wakilaani mauaji hayo. Huwezi kusikia serikali katili ya CCM ikitoa tamko kuhusu mauaji hayo ya raia huko Sudan.
Lakini vifo vya wapalestina na watu wa Israeli vimewaumiza watanzania kweli hadi wametangaza maandamano ya kusimama na Palestina wengine Israeli. Nani atasimama na raia wa Geneina, Sudan Magharibi?
Wizara ya mambo ya nje, imejikausha kama hakijatokea kitu Sudan. KIPARA anasubiri kuonekana kwenye ziara za ughaibuni na mapicha picha ya hapa na pale na ‘kavideo’ kamnato. Hawawezi kutoa tamko kulaani mambo haya!
Geneina (Al-Junaynah) ni mji mkuu wa West Darfur na umeathiriwa na vita ya Sudan. Battle of Geneina (Geneina massacre) watu 5,000 wameuwawa kati ya 24 April na 24 June na watu 370,000 ni wakimbizi.
Huwezi kuona hashtag za kuhusu tukio hilo. Hazilipi. Haziwalipi wanaharakati mchongo wa kiafrika. Wakazi wa Geneina (Al-Junaynah) 98% ni waumini wa dini ya Kiislam. Waislam wa Tanzania hawasimami nao?
Anyways, tukipata nafasi tutajadili vizuri hii vita ya Sudan.
View attachment 2808359