January Makamba: A New Generation Leader!

January Makamba: A New Generation Leader!

Binti Maringo

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
2,804
Reaction score
96
Watu wanampinga sana ndugu Januay Makamba (majority vijana wale wenye roho za kwa nini)...juzi hapa ndani ya white house January kapiga story na Barack Obama kuliko hata Obama alivyoongea na JK....hadi Obama mwenyewe kamkubali kuwa kIJANA January Makamba ni kichwa/Smart na ndiyo new generation leader of Tanzania au kwa maana nyingine Future leader wa Tanzania...kama akipikwa vizuri basi....olooo "Change is coming to Tanzania"


From Mo's Blog said:
Nilizaliwa tarehe 28 Januari 1974. Nalipenda sana jina langu kwasababu mara nyingi ninapojitambulisha kwa watu, automatically linaanzisha mazungumzo. Mara nyingi huulizwa kama nilizaliwa mwezi Januari ndio maana nikapewa jina hilo. Ukweli ni kwamba hiyo sio sababu per se. Sababu kubwa ni kwamba, wakati nazaliwa, Mzee wangu alikuwa na rafiki yake mkubwa aliyempenda sana aliyeitwa Januari. Akaamua kunipa jina lake kwa mapenzi yake kwa rafiki yake. Ilikuwa ni coincedence tu kwamba nilizaliwa mwezi wa kwanza. Lakini jina ambalo Babu yangu mzaa baba alinipa na alipenda kuniita kabla hajafariki mwaka 1984 ni Rajab, ambalo ni jina lake yeye. Kwahiyo hadi leo, kijijini kwetu Mahezangulu, Lushoto, hasa kwa wale wazee wa kule, na hata kwa bibi yangu, najulikana kama Rajab.

Nimesoma kwenye shule mbalimbali za msingi katika mikoa mbalimbali nchini, kadri wazazi wangu walivyohama kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kingine. Nilianzia Monduli mwaka 1981. Mwaka 1983, nikapelekewa kukaa na bibi mzaa mama kijijini Kituntu, karibu na Kyaka, Bukoba Vijijini. Mama yangu kwao amezaliwa peke yake, kwahiyo bibi alihitaji mjukuu wa kukaa naye kumsaidia. Ndio nikatolewa kafara. Hahahaha! Kwahiyo darasa la tatu, la nne na la tano, nimesoma kijijini. Siwezi kusahau maisha yale: asubuhi ni kupiga umande literally kwenda shule umbali wa kama kilomita nne na nusu hivi kutoka nyumbani, ukirudi saa tisa ni kwenda kuchunga mbuzi, ukisharudisha mbuzi zizini saa kumi na mbili jioni ni kwenda kuchota maji mtoni, usiku kazi ni kumsaidia bibi kuuza pombe ya ndizi inayoitwa lubisi (bibi alikuwa na kilabu maarufu pale kijijini).

Samahani hapa nime-digress kidogo kwa kukumbuka na kuelezea zaidi kipindi hiki. Lakini experience hii ni sehemu ya mimi. Siku hizi NGOs zinayaita haya "mazingira hatarishi", lakini watoto wengi vijijini ndio maisha yao ya kila siku. Some make it, through pure luck or strength of character, some don't.

Anyway, nilirudi kukaa na wazazi wangu tena wakiwa Lushoto kwahiyo nikasoma darasa la sita pale, Shule ya Msingi Kitopeni, na kwenda kumalizia darasa la saba shule ya Msingi Masiwani Tanga Mjini. Hapa Tanga Mjini niliingia na kusoma madras which was quite rewarding ingawa sikumaliza msahafu. Pamoja na kuhamahama, na dhahama za maisha ya kijijini, I have always done well in school. Sikumbuki kama nilishawahi kushuka chini ya nafasi ya nne.

Form one nilisoma Handeni Secondary School, hii ilikuwa ni shule mpya, sisi tulikuwa Form One ya pili – kulikuwa hakuna walimu, madawati, maabara, n.k. Form Two hadi Form Four nikasoma Galanos, Tanga Mjini. Wakati nikiwa Form Three nilichaguliwa Deputy Head Prefect pale Galanos. Form Five na Six nikawa Forest Hill Secondary School, Morogoro, ambapo siku ya graduation nilitunikiwa cheti cha Overall Best Student.

Anyway, wakati nasuburi kwenda university, nikaenda kutafuta kazi kwenye kambi za wakimbizi Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma. Nikafanikiwa Kasulu. Ukiacha maisha ya kijijini na bibi, this was another rewarding experience kwenye maisha yangu. Nilipata responsibilities kubwa kadri muda ulivyoenda, hadi kufikia ngazi ya Assistant Camp Manager kwenye kambi ya Mtabila Extension au Mtabila II, ambayo literally niliianzisha mimi (baada ya kuwa Serikali imetoa eneo) from the scratch kwa maana ya kusimamia ujenzi wa infrastructure za kambi na kugawa plots kwa wakimbizi. Kwenye kazi hii ndipo kwa mara ya kwanza nilipokutana na kuanza ku-engage na kujenga urafiki na watu wa mataifa mbalimbali waliokuwa expatriates kwenye camps. Muda wa kwenda Chuo ulivyofika, sikwenda kwani nilinogewa na kazi, mwaka uliofuatia sikwenda tena kwani nilipata responsibilities kubwa zaidi kambini and I was making and saving good money.

Eventually nikapata Chuo Marekani. Nilianza Boston baadaye nikajiunga na St. John's University, Minnesota. Hiki ni Chuo cha Wakatoliki Wabenedicto kilichokuwa katikati ya pori na lakes, a very beautiful and quiet place, katikati ya Jimbo la Minnesota. Pale, degree niliyochukua ni BSc in Peace and Conflict Studies. Niliamua kusoma hii kozi kutokana na experience yangu kwenya makambi ya wakimbizi. Nilitaka kuelewa ni kwa namna gani tunaweza kuzuia watu wasikimbie kabisa nchi zao, kwani maisha ya ukimbizi, kwa nilivyoyaona, ni ya udhalilishaji mkubwa sana na yanaondoa dignity ya mtu.

Wakati nikiwa St. John's University, nilirudi tena kufanya research yangu na UNHCR kwenye makambi ya wakimbizi Kasulu na Kibondo lakini pia kwenye way stations ndani ya Burundi na DRC.

Baada ya kumaliza St. John's, nikapata research assistantship kwenye ofisi ya Rais wa zamani wa Marekani, Mzee Jimmy Carter, Carter Presidential Centre, kule Atlanta, Georgia. Kazi hiyo ilinipeleka hadi kufanya kazi Sierra Leone, ambako pia nilijifunza mengi. Pia Atlanta ndiko nilikofanikiwa kukutana na mke wangu mpendwa, Mona, ambaye mwakani itakuwa miaka kumi tangu tujuane, na ambaye, pamoja naye, tuna mtoto mmoja wa kike wa miaka mitatu na nusu.

Baada ya Carter Center, nikajiunga na George Mason University, iliyoko maeneo ya Fairax, Washington DC metro area, kusoma Masters kwenye fani ile ile ya diplomasia na usuluhishi wa migogoro. Nilikuwa a very active graduate student kwa maana ya kushiriki mijadala na professional and advocacy associations mbalimbali pale DC. I created a vast network of friendships in DC ambayo hadi leo nafaidika nayo. Nikiwa graduate school, nilipata fursa ya kufanya internship Wizara ya Mambo ya Nje.

Baada ya kumaliza graduate school nikaomba kazi Serikalini na kuajiriwa na Wizara ya Mambo ya Nje kama Afisa wa Mambo ya Nje Daraja la Pili (Foreign Service Officer II). Nikiwa Wizara ya Mambo ya Nje, nilipata fursa ya kufanya kazi kwa karibu na Waziri wetu wakati ule (Mhe. Kikwete), hasa kwenye harakati za kutafuta suluhu ya mambo ya Burundi na DRC. Kwahiyo, wakati alipoamua kugombea Urais, akaniomba nichukue likizo isiyo na malipo Serikalini nisaidie kuwa errand boy kwenye kampeni yake, ku-organise makaratasi na notes zake, na kuchangia hapa na pale kwenye tafakuri za kuendesha na ku-organise kampeni yake wakati ule. Tulifanikiwa kufanya mambo mengi mapya na ya kisasa kwenye kampeni ile (including TV campaign ads kwa mara ya kwanza). Nilishukuru sana kupata fursa ya kuzunguka Mikoa yote na Wilaya zote nchini, kwa kweli kila kona ya nchi, kwa njia ya barabara na kujua na kujuana na watu na kujua kwa kina changamoto na fursa za maendeleo katika maeneo yote. Mhe. Kikwete alipofanikiwa kuchaguliwa, akaniteua nije kumsaidia hapa Ikulu na hapa ndipo nilipo hadi leo.

Kazi hii ni ya heshima kubwa sana na ni muhimu kui-approach with humility. In fact, kuna nyakati natafakari sana kwamba, katika kufanya kazi hii, inawezekana nafaidika zaidi mimi katika kujifunza kuhusu nchi yetu, Serikali inayoendeshwa, maamuzi yanavyofanywa, sera zinavyotengenezwa, na siasa na uongozi wa nchi kwa ujumla unavyoendeshwa, kulivyo Rais anavyofaidika na usaidizi wangu.

 
Hmmmm...wewe nawe hizi hoja zingine...laaaawd have mercy
 
Ndiyo nani huyo January Makamba? Kwa sasa ana shika nyadhifa gani? Labda ungetupa historia yake kwa ufupi na ni nini ana fanya kwa sasa.
 
Ndiyo nani huyo January Makamba? Kwa sasa ana shika nyadhifa gani? Labda ungetupa historia yake kwa ufupi na ni nini ana fanya kwa sasa.


MwanaF!....Google him utapata his biography Mwanawane!....


YE!...Hahahaha nimezipata hizi jikoni you know.....you knw me i have inside friends/intelejensia.
 
why do you judge my hojas?...is it because obama is involved?....

Sijui hata kama unajua maana ya hoja and there is no need for you to get defensive. But I'm out on this one. No more questioning from me. Adios
 
Sijui hata kama unajua maana ya hoja and there is no need for you to get defensive. But I'm out on this one. No more questioning from me. Adios

i am not trying get defensive ila habari ndiyo hiyo....swali wewe ulivyoandika kwa nini wanawake wa shave..uliona hiyo ni hoja ya maana?....just curious!>..
 
i am not trying get defensive ila habari ndiyo hiyo....ila angeandika mwanaume kama wewe ndiyo ungeona ana make sense ila kwa sababu ni mimi so unaona kama vile i dont make sense kisa i am a female...ianchie hoja kama ilivyo...mr smart guy!...

Una project gender inferiority yako. Hoja mbovu ni hoja mbovu tu. Haijalishi kama aliyeitoa ni mwanamke, mwanamme, transgender, hermaphrodite, gay, au hata klingons...

I'm going to heed your advice and let it be...okay?
 
i am not trying get defensive ila habari ndiyo hiyo....swali wewe ulivyoandika kwa nini wanawake wa shave..uliona hiyo ni hoja ya maana?....just curious!>..

Nope, that was one of the most ridiculous topics of the day and I admit it. I did it by design. There is no shame in my game.
 
Una project gender inferiority yako. Hoja mbovu ni hoja mbovu tu. Haijalishi kama aliyeitoa ni mwanamke, mwanamme, transgender, hermaphrodite, gay, au hata klingons...

I'm going to heed your advice and let it be...okay?


define hoja ya maana!....nimeshakuuliza swali wew eulivyoandika kwa nini wanawake wana shave...hiyo uliona ni hoja ya maana?...au kwa sababu nimemtaja January makamba ndiyo unaona hoja hai-make sense?...kama mtu ana qualification zake give him/her pro...roho za kwa nini tuache..hatutafika huko.
 
Watu wanampinga sana ndugu Januay Makamba (majority vijana wale wenye roho za kwa nini)...juzi hapa ndani ya white house January kapiga story na Barack Obama kuliko hata Obama alivyoongea na JK....hadi Obama mwenyewe kamkubali kuwa kIJANA January Makamba ni kichwa/Smart na ndiyo new generation leader of Tanzania au kwa maana nyingine Future leader wa Tanzania...kama akipikwa vizuri basi....olooo "Change is coming to Tanzania"

mimi simjui vizuri january makamba.yeye alionana na kuongea kwa mda mrefu na obama kama nani na maswala gani waliongea kama yeye sio mwakilishi wa nchi? nataka kumjua tu vizuri manake hua namsikia tu juu juu.nitashukuru sana ukinifahamisha.
 
define hoja ya maana!....nimeshakuuliza swali wew eulivyoandika kwa nini wanawake wana shave...hiyo uliona ni hoja ya maana?...

Nimeshajibu hilo swali. Hujaridhika na jibu langu?

au kwa sababu nimemtaja January makamba ndiyo unaona hoja hai-make sense?...kama mtu ana qualification zake give him/her pro...roho za kwa nini tuache..hatutafika huko.

Hakuna mtu mwenye roho ya kwanini hapa. He does his thing and I do my thing. Wewe kama unamwona yeye anafaa kuja kuwa kiongozi hapo baadae that's fine. You are entitled to it.
 
nyani ngabu hivi january makamba ana cheo gani kwenye nchi yetu? naomba unisaidia manake simfahamu vizuri.
 

Watu wanampinga sana ndugu Januay Makamba (majority vijana wale wenye roho za kwa nini)...juzi hapa ndani ya white house January kapiga story na Barack Obama kuliko hata Obama alivyoongea na JK....hadi Obama mwenyewe kamkubali kuwa kIJANA January Makamba ni kichwa/Smart na ndiyo new generation leader of Tanzania au kwa maana nyingine Future leader wa Tanzania...kama akipikwa vizuri basi....olooo "Change is coming to Tanzania"

Ulimsikia Obama akimsifia Makamba au yeye kakuimbisha sera ukanunua tu kwa huruma?

Makamba ataonewa wivu kwa kitu gani, kazi ya Ikulu ya mapande au shahada ya Marekani za usomi wa kuiba makala za NY Times na kuziweka kama zake kwenye blogu?
 
January has the stars aligned, which could be a blessing and a curse.

1. To start with he has the "right" surname, not to tarnish his brightness, lakini tuna watu bright wangapi Tanzania na hawapati hata nafasi za kutoa michango yao? Let's face it, January is relatively bright, some would even say brilliant by Tanzanian standards, lakini kuna personal connection kati ya Kikwete na Makamba ina play part. Undoubtedly rais anataka ku appoint aides atakao waamini, kwa hiyo mara nyingine ni vigumu kuchukua watu wa mbali. Kikwete na Yusuf Makamba wanajuana tangu siku zao za propaganda za chama katika jeshi. Sitashangaa kama January anaandaliwa kwa ubalozi au ataenda kugombea ubunge sometimes and pull a "Mizengo Pinda" of sorts.

2. January has academic credentials, he went to some allright schools - I believe Minnesota and George Mason. So no one can say he is unqualified, which is a good thing. It is one thing to show favoritism to a qualified candidate, and quite another to do the same to an unqualified candidate. Although favoritism is still favoritism by any tother name.His conflict resolution training, stints with refugees (UNHCR?) in Kigoma and fellowship at the Carter Presidential Center should have equipped him with a much needed global outlook, especially in the Kikwete Ikulu.

3. This guy used to be very progressive in his outlook, but as with all "revolutionaries" who start out with a brilliant vision to implement, he has cooled off and is continually surrendering his passion to the status quo. Indeed he is becoming part of the status quo. In any case I believe JK is better off with a young mind like January's if only to utilize his voracious leadership and hence benefit from sound advise on current affairs and international relations. JK is an airhead and just as he needed Dim to show him the ropes at MOFA, he needs January to advice him in this internet age at Ikulu.

4. The one downside of January is that he fancy himself a policy wonk and as a result he comes off as arrogant. Just recently when he was with JK he almost created a diplomatic row by badmouthing Nigeria's export of oil while Nigerians lack oil, in an attempt to caution Kikwete and say openly that however the deal will unfold Tanzania will not tolerate leaving it's people hungry while exporting food. This statement is both good and bad, it is good to know that at least he was thinking this way and he got to air this concern at a time where Kikwete was probably giggling and smiling ready to sign all documents without laying down serious policy positions.It is bad because it was very undiplomatic and had it been made in an environment where the press was active it could have escalated matters to the level of a public apology.Apart from his experience January showed that he is still a rookie by trusting a "journalist friend" with his private views, only to read them on the papers the next day. A simple "Tanzania will not export food while it's people are lacking" without badmouthing Nigeria and creating a potential row would have sufficed.

5. There are some concerns about his drinking habit and his newly minted marriage that borders on the ethics of leadership, but I would deem some of these rather private for now.The guy is just an aide, presidential or not.
 
Ulimsikia Obama akimsifia Makamba au yeye kakuimbisha uongo kuwa anaonewa wivu?

Makamba ataonewa wivu kwa kitu gani, kazi ya Ikulu ya mapande au shahada ya Marekani za usomi wa kuiba makala za NY Times na kuziweka kama zake kwenye blogu?

Heheheheheee....sometimes you make sense...and I give props where props are due. The guy is a plagiarist halafu watu wanadai eti ni kichwa. Kichwa my foot....vichwa hawaibi maandiko ya wengine.
 
Back
Top Bottom