January Makamba: A New Generation Leader!

kelly 1, GT

umesema JM ni kichwa sanaaaaaa....
na GT ameleta picha.....

kelly1
nakuomba utuweleze mafanikio ya JM ampaka wewe umemuona special na anafaa kuwa rais, labda kuna vitu unavijua juu yake lakini watu wengi humu ndani atuvijui, ukifanya hivyo itakuwa vizuri sana kulikoni kuweka maneno matupu

GT
asante kwa kutuletea picha za JM ambazo zimetoka vizuri sana...
kutokana na hizo picha nina imani kabisa unaweza kutueleza kazi za JM anazofanya kila siku ni zipi na ni mambo gani ambayo unadhani JM ameyafanya kustahili sifa
maana yake humu ndani watu wamesema yeye ndio huwa anamshauri kikwete hata kwenye hotuba na mambo mbalimbali ya nje ya nchi na hata akisafiri amuachi lakini JK amekuwa akiboronga na watu wanasema hiyo ni kazi ya JM, kwa hiyo kama si kazi yake naomba utueleweshe na utuambie kazi zake ni zipi na mafanikio yake katika taifa hili ni yapi (kwa mawazo yako) na ni special anaweza kuwa rais
 

- Mkuu haya ni maneno yaliyojaa busara na ukweli, na hasa kuona mbali katika picha kubwa, naona maneno mengi humu lakini ukweli haupo kosa la huyu kijana ni lipi? Na ni nani hasa anayejua kazi yake ya kila siku kwamba sasa atuambie wapi amekosea na wapo yuko sawa!

- Mwacheni kijana afanye kazi, mengine ni fact of life kila mmoja na bahati yake katika maisha.

Ahsante.

William.
 
Kama uongozi unatolewa kwa kupiga story, ndo maana wajanja wanaoweza kupiga story kwa wakubwa wanatula kwa ulaini. Makamba kuongea huwa anaongea mpaka anasahau kaongea nini. Labda kamrithisha mwanae? Itakuwa bahati mbaya kama watu tutatumia criteria ya jamaa kumchekesha Obama ndio uwezo wa kuwa kiongozi.
 
Dukuduku la watu ni kutorithishana Tanzania. Badala yake watu warithishane Nyumba na mashamba etc ambayo baba zao wanamiliki. Kama ni kiongozi safi, hakuna shaka wa TZ tunamuhitaji. Ila kama cheo na nafasi aliyonayo ni shukrani au ni suala la kupewa fadhila ya baba kuwa kwenye mtandao, hana sababu ya kufikiria kurithi kwa upole madaraka labda ya chama. Mana leo hii TZ yote yanazungumzwa atii
 

Kwanza waje hao wanaodai JM hafai walete sababu zao na mimi nitakuja na sababu zipi anafanyaa

MImi nilishaoanisha kwenye hii thread nadani kwenye post namba tatu au nne

wote wamekimbia hakuna aliyerudi
 
Unajua kumfanya mtu ashinde kiti cha uraisi siyo kwa wananchi tuu kukaa na kusema kuwa hatumtaki fulani...Ila si jinsi gani uta ji-market wewe kwa watu!...Ule mwaka 2000 Bush alivyokuwa nagombea uraisi watu wengi sana walikuwa wanampinga ila kutokana na watu aliokuwa nao around akina genius kama Karl Rove walivyokuwa wanaendesha kampeni .......inabidi kwanza kuwa na strategy then market that person...wewe unataka kuniambia W bushi alikuwa na sifa gani hadi awe raisi?......

Kama sasa Obama watuw alisema hana experience hana sifa lakini kutokana na ile public relation na marketing plan waliyokuwa nayo akina David Axerlod ndiyo kawez akushinda...its what you do and not sit down and tall to talk!@.......
 

lakini wewe ndio umemuweka JM ahead na kusema ni new generation leader na ni kichwa sana,
halafu wewe ndio unasema rais sio lazima awe na akili na anaweza kuwa mtu yeyote(sipingi), rais anaweza kubebwa na watu kama karl rowe (nakubali)

swali kwa hiyo JM ni kichwa kama ulivyosema mwanzo (naomba sababu) au JM ni mpumbavu na anabebwa, na atabebwa kama bush alivyobebwa

dada watu wamekutukana wamekuita kimbelembele, mimi nakupa nafasi ya kusema kwa nini umemuona JM ni kichwa kuliko wengine (naomba uwende straight kwenye jibu usilete story za kina carl rowe)


kelly1
nakuomba utuweleze mafanikio ya JM ampaka wewe umemuona special na anafaa kuwa rais, labda kuna vitu unavijua juu yake lakini watu wengi humu ndani atuvijui, ukifanya hivyo itakuwa vizuri sana kulikoni kuweka maneno matupu
 

- Mkuu haya ni maneno yako tu kama ya wengine wengi, ambayo hayawezi kuongeza wala kuzuia anything, Januari ni raia kama wengine wote wa Tanzania ana haki za ku-pursue anything baba yake ni kiongozi wa taifa sio a crime kama unavyotaka kuiweka,

- Akiamua kugombea uongozi ni uamuzi wa wananchi kama Tanzania tuna sheria zinazoruhusu baba kumrithisha mtoto uongozi, then omba katiba ibadilishwe, lakini kumlaumu Januari na kumkashifu bila sababu wakati yeye yuko juu tayari sidhani kama inaweza kusaidia, mkuu huyu Januari sasa ni msaiidzi wa karibu sana wa rais wa jamhuri yetu, sasa niambie akitoka hapo atakuwa nani? Katibu tarafa? No way aliye juu huwezi kumngoja chini ni lazima umfuate huko huko juu!

Ahsante.


William.
 
Mnamsema sana mtu wa watu utafikiri kashasema anataka uongozi wa juu. Mnamchambuaje mtu katika uongozi kama yeye mwenyewe haja sema anataka huo uongozi? Stop scrutinizing the man sasa. Hii ni sawa sawa na kugombania pesa kabla hata haujaipata, IT MAKES NO SENSE!!! If and when he decides to seek a certain office then you can discuss how he is qualified for that post. Hauwezi kumjadili mwali kabla haja chumbiwa.
 

MwanaFA, inawezekana JM au wapambe wake walileta hii mada kama kipimajoto ili kucheki watu wanamuonaje

Utawaona sana tu ila tuwape pole zile heal za siasa ya uchaguzi wa wazazi hakuna sasa
 
MwanaFA, inawezekana JM au wapambe wake walileta hii mada kama kipimajoto ili kucheki watu wanamuonaje

Utawaona sana tu ila tuwape pole zile heal za siasa ya uchaguzi wa wazazi hakuna sasa

Unajua mkuu nilikuwa sijali wazia hilo. You make a very good point. Hii yaweza kuwa kipima joto kwa njia moja amaa nyingine. Maana hii mada ilisha kufa kwa muda fulani ghafla nika shangaa ina tokea tena kwa nguvu mpya, kasi mpya na ari mpya hahaha.
 
kwikwikwikwikwikwikwi mkuu umeuaaaa.....sio kucha tu hata huko chini kushalowa......

Kwikwikwikwi. Hawachelewi kuanza kutafuna nyasi. Anyway, sasa hivi nchi inahitaji watu kufanya vitu (get things done) hata kama hawatakuwa wazungumzaji. Na hili ndilo linaloshindikana toka uhuru upatikane.

Na vilevile kwa sababu ni mtoto wa maKamba na msaidizi wa rais, watu wanaomjua wasifikiri kuwa watanzania wengine tunamfahamu kama wao wanavyomfahamu.
 

Si ndiyo huyu huyu ambaye akienda Washington DC hataki kukutana na watanzania wenzie anabaki kujichimbia hotelini! ...sasa kama anamawazo mazuri ya kuijenga nchi why run away from fellow Tanzanians????...interesting!
 
Si ndiyo huyu huyu ambaye akienda Washington DC hataki kukutana na watanzania wenzie anabaki kujichimbia hotelini! ...sasa kama anamawazo mazuri ya kuijenga nchi why run away from fellow Tanzanians????...interesting!

Wa Tanzania wenyewe mmejaa majungu tu...hata nigekuwa mimi ninge jichimbia hotelini!
 
Wa Tanzania wenyewe mmejaa majungu tu...hata nigekuwa mimi ninge jichimbia hotelini!

Kui do you no JM at a personal level? Meaning is he a friend or someone you are acquainted to?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…