January Makamba amefuta mradi wa kujenga Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa KICC na kuja na miradi ya upigaji ya kujenga magorofa nchi za nje

1.Kwa hiyo Ulaya hakuna mipangilia Hadi waje Nairobi na Kigali? Acha ujinga.

2.Hospitality industry inaanza na kuwa na sehemu stahiki Kwa shughuli

3.Soko la Biashara ya Utalii na Mikutano halio West pekee

4.Kigali na Tanzania wapi Kuna usafiri wa Anga wa uhakika?

5.Tanzania Iko Juu ya Nchi zote hizo Kwa idadi na thamani ya Utalii,hiyo marketing Yako ni ipi hasa?

Acha blaa blaa Miji Yao Ina facilities za ku handle mikutano ya deligates kuanzia 3,000-5,000 Kwa level za VIP.

Tanzania tuna advantage zaidi Yao ila hatuna Kumbi Zenye hadhi.
Hujui chochote, unabwabwaja tu kwa sabubu ya kukosa exposure.
 
Mikutano Mingi sana imefanyika ya wajumbe Hadi 2,000 achilia hao buku ya hivyo inafanyika Kila mwaka.

Mfano mwezi ujao Kuna Mkutano wa Mambo ya Uvuvi Afrika zaidi ya deligates 1,5000 wanakuja.
Itaje hiyo mikutano kwa majina yake, acha porojo zako.
 
Wewe ndio mropokaji,Ingia kwenye tovuti ya AICC utaona hiyo mikutano.

Mmjawapo ni huu hapa 👇
Screenshot_20240530-112135.jpg

Na mingine inakuja ukiwepo huu hapa

View: https://www.instagram.com/p/C7d2F_3Iz3Y/?igsh=YjZlbnE1N2pvbGc4
 
Wizara ya mambo ya nje inatumia sana kuliko mapato/inavyozalisha; achilia mbali madeni na misaada michache.
Katika kubuni vyanzo vya mapato kupitia wizara yake, yuko sahihi; ingawa kimuonekano itakuwa inapendezesha miji ya wengine.
Muhimu tu angeeleza baada ya muda gani hiyo fedha ya uwekezaji itakuwa imerudi.​
 
Upuuzi,huo sio ubunifu ni ujinga.Kuna vitu vingi vya maana wanaweza kubuni na vikafanya vyema hapa hapa ndani ya Nchi.

Wanashindwa nini kuungana na TBA au National Housing kuweka majengo ya biashara?

Mbona sekta binafsi wanashirikiana na Hayo mashirika na wapangaji wapo?

Ni miradi ya wizi hakuna kitu hapo.Kama Wana viwanja viko poa wawape wawekezaji huko huko wajenge wao wachukue Kodi sio kutumia pesa zetu kujenga Nchi za watu ,hii ni upunguani.
 
Labda tupate elimu kidogo kuhusu hii miradi. Binafsi sifahamu manufaa yake japo huku kwetu waarabu wanamiliki magorofa na tumepangisha huko
 
Miradi kama hiyo ni kichaka cha upigaji nchi haiwezi faidika chochote!
Imagine miradi iko hapa bongo tu upigaji kama wote huko nje ya nchi sindio itakuwa balaa zaidi?!.
Na ukikamilika wahuni wanaingia mikataba na wapangaji serikali inapata m 500 wahuni wanaweka mfukoni bilioni hata 2!.
 
Upuuzi,huo sio ubunifu ni ujinga.Kuna vitu vingi vya maana wanaweza kubuni na vikafanya vyema hapa hapa ndani ya Nchi.

Wanashindwa nini kuungana na TBA au National Housing kuweka majengo ya biashara?

Mbona sekta binafsi wanashirikiana na Hayo mashirika na wapangaji wapo?

Ni miradi ya wizi hakuna kitu hapo.Kama Wana viwanja viko poa wawape wawekezaji huko huko wajenge wao wachukue Kodi sio kutumia pesa zetu kujenga Nchi za watu ,hii ni upunguani.
Mfano, kama wewe ndio ungepewa hiyo wizara, na unatakiwa ubuni vyanzo vya mapato kwenye wizara yako na uhakikishe mapato katika wizara yako yanazidi matumizi; ungekuja na wazo lipi?
 
Kwanza sio kazi ya Wizara ya mambo ya Nje kubuni Vyanzo vya Mapato,hiyo ni kazi ya Wizara ya Fedha na zile za kiuzalishaji.

Kwa.muktadha wa swali lako na mada ya Makamba anatakiwa kufanya yafuatayo
1.Kutangaza viwanja ambavyo wanaweza kuviendekeza Ili wapate private companies zijenge majengo na watakuwa wanachukua Kodi yaani utaratibu wa PPP.

2.Pili wanatakiwa wawe wanahamasisha uwekezaji,kutafuta masoko ya bidhaa zetu na kusaidia kuitangaza Nchi na kuwasaidia Watanzania wafanyabiashara,Wana taaluma nk.
 
Mwaka Jana Serikali ya Tanzania ilisema inaenda kufufua Mradi mkubwa wa kujenga Ukumbi mkubwa wa Mikutano ya Kitaifa Kwa jina la Kilimanjaro International Convention and Exhibition Centre-KICC Arusha ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua Washiriki zaidi ya 3,000 Kwa Ajili ya kushindana na Kenya, Rwanda kwenye biashara ya Utalii wa Mikutano.

Sasa alivyoingia bwana Makamba Amefuta Mradi huo na badala yake amekuja na plan ya kuanza kujenga majengo makubwa aliyoita ya kibiashara na ya kupangisha kwenye Nchi zingine Kwa kutumia viwanja vinavyomilikiwa na Balozi zetu.

Mfano anasema Serikali utajenga jengo la Gorofa 22 Nairobi Kenya

Itajengwa jengo la Gorofa 25 Kinshasa

Gorofa 18 Lusaka Zambia nk

Hivi na Nchi zingine zinafanya mambo ya ajabu kama hivi? Yaani badala ya kuendeleza kwenu mnajenga Miji ya watu Kwa maelezo kwamba mtapangisha.

Binafsi siungi mkono Mpango huu naona kama ni ufujaji wa pesa za Umma.Tujenge kwetu Kwa manufaa ya Watanzania.

----
TANZANIA KUVUNA TSH 36B KILA MWEZI UJENZI WA MAGHOROFA NJE YA NCHI

Serikali kwa mwaka wa fedha ujao, umepanga kujenga majengo ya kiuchumi katika majiji ya Kinshasa (DRC- ghorofa 25) na Nairobi (Kenya- ghorofa 22).

Picha za majengo ya Nairobi na Kinshasa zipo tayari na picha za majengo mengine ya kitega uchumi katika majiji ya Maputo (Msumbiji), Bujumbura (Burundi), Kigali (Rwanda) na Lilongwe (Malawi) nayo imewekwa wazi.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Mei 28, 2024 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Wizara imeliomba Bunge kuidhinisha Sh241.069 bilioni ambapo kati ya fedha hizo Sh229.4 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh11.6 bilioni ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.

Maombi hayo ya fedha ni pungufu kwa asilimia tatu ikilinganishwa na bejeti iliyopita na hiyo imetokana na kupungua kwa fedha za maendeleo kwa asilimia 34.

Kwa mujibu wa Makamba, Serikali ina nyumba na viwanja 109 dunaini kote na kodi ya pango wanayolipa ni Sh29 bilioni kwa mwezi.

Amesema uwekezaji huo ukikamilika utaingiza Sh36 bilioni kwa mwezi na kwa mwaka Sh692 bilioni.
Huyo january ni wenu!
 
Naona una point Ila pengine unashindwa kuelezea
Kwamba wawekezaji wajenge hayo majengo alafu Kodi wachukue bolozi za Tanzania?
Upuuzi,huo sio ubunifu ni ujinga.Kuna vitu vingi vya maana wanaweza kubuni na vikafanya vyema hapa hapa ndani ya Nchi.

Wanashindwa nini kuungana na TBA au National Housing kuweka majengo ya biashara?

Mbona sekta binafsi wanashirikiana na Hayo mashirika na wapangaji wapo?

Ni miradi ya wizi hakuna kitu hapo.Kama Wana viwanja viko poa wawape wawekezaji huko huko wajenge wao wachukue Kodi sio kutumia pesa zetu kujenga Nchi za watu ,hii ni upunguani.
o
 
Mwaka Jana Serikali ya Tanzania ilisema inaenda kufufua Mradi mkubwa wa kujenga Ukumbi mkubwa wa Mikutano ya Kitaifa Kwa jina la Kilimanjaro International Convention and Exhibition Centre-KICC Arusha ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua Washiriki zaidi ya 3,000 Kwa Ajili ya kushindana na Kenya, Rwanda kwenye biashara ya Utalii wa Mikutano.

Sasa alivyoingia bwana Makamba Amefuta Mradi huo na badala yake amekuja na plan ya kuanza kujenga majengo makubwa aliyoita ya kibiashara na ya kupangisha kwenye Nchi zingine Kwa kutumia viwanja vinavyomilikiwa na Balozi zetu.

Mfano anasema Serikali utajenga jengo la Gorofa 22 Nairobi Kenya

Itajengwa jengo la Gorofa 25 Kinshasa

Gorofa 18 Lusaka Zambia nk

Hivi na Nchi zingine zinafanya mambo ya ajabu kama hivi? Yaani badala ya kuendeleza kwenu mnajenga Miji ya watu Kwa maelezo kwamba mtapangisha.

Binafsi siungi mkono Mpango huu naona kama ni ufujaji wa pesa za Umma.Tujenge kwetu Kwa manufaa ya Watanzania.

----
TANZANIA KUVUNA TSH 36B KILA MWEZI UJENZI WA MAGHOROFA NJE YA NCHI

Serikali kwa mwaka wa fedha ujao, umepanga kujenga majengo ya kiuchumi katika majiji ya Kinshasa (DRC- ghorofa 25) na Nairobi (Kenya- ghorofa 22).

Picha za majengo ya Nairobi na Kinshasa zipo tayari na picha za majengo mengine ya kitega uchumi katika majiji ya Maputo (Msumbiji), Bujumbura (Burundi), Kigali (Rwanda) na Lilongwe (Malawi) nayo imewekwa wazi.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Mei 28, 2024 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Wizara imeliomba Bunge kuidhinisha Sh241.069 bilioni ambapo kati ya fedha hizo Sh229.4 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh11.6 bilioni ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.

Maombi hayo ya fedha ni pungufu kwa asilimia tatu ikilinganishwa na bejeti iliyopita na hiyo imetokana na kupungua kwa fedha za maendeleo kwa asilimia 34.

Kwa mujibu wa Makamba, Serikali ina nyumba na viwanja 109 dunaini kote na kodi ya pango wanayolipa ni Sh29 bilioni kwa mwezi.

Amesema uwekezaji huo ukikamilika utaingiza Sh36 bilioni kwa mwezi na kwa mwaka Sh692 bilioni.
Nakumbuka nilishakuambiaga marope ni mwizi,ila ulimtetea,jamaa wakati yuko nishati ulikua mtetezi namba 1 nashukuru na nafurahi sasa umeanza kumjua
 
Hivi tumefikia mahali pa serikali kufanya biashara ya nyumba za kupanga kweli?!!!
 
Back
Top Bottom