RICH-MONDULI
New Member
- Jul 5, 2011
- 4
- 5
Waziri wa Nishati, January Makamba, anamfanyia hujuma za wazi Rais Samia Suluhu Hassan ili kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hujuma yake ilithibitika wakati wa bajeti ya Wizara ya Nishati ya 2023/2024 jijini Dodoma wiki hii ambapo Makamba aligawa pesa kwa baadhi ya wabunge na kuwapa maelekezo kuwa wamsifie yeye binafsi, badala ya Rais Samia.
Baadhi ya wabunge wa Zanzibar na mikoa ya bara walipewa vitita vya pesa na Makamba ili kuhakikisha kuwa wanamwagia sifa Bungeni na kupitisha bajeti ya wizara yake.
Pia alifanya mkakati kuwa wabunge wenye msimamo ambao wangesimama kumkosoa hawapewi nafasi ya kuongea wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati.
Lengo la mpango huo wa Makamba ni kujijenga yeye binafsi kisiasa akiwa na mahesabu ya kuupata Urais 2025 au 2030.
Baadhi ya wabunge wameeleza kuwa Makamba aligawa pesa nyingi kwa wabunge ili kubadili upepo, baada ya kubaini kuwa wabunge wengi walijipanga kumlipua Bungeni kwenye bajeti yake.
Tangu aingie kwenye Wizara ya Nishati, Makamba ametuhumiwa kuhusika na tuhuma lukuki za ufisadi na usimamizi mbovu wa sekta ya nishati nchini.
Umeme umekua unakatikakatika hovyo nchi nzima tangu Makamba aingie madarakani, huku TANESCO wakishindwa kutoa huduma za uhakika na kuwa kero kwa wananchi na kudhoofisha ukuaji wa uchumi.
Mradi wa umeme wa JNHPP unaendelea kusuasua, huku kukiwa hakuna usimamizi makini wa mkandarasi na kusababisha gharama za ujenzi kuongezeka maradufu,.huku mradi ukichelewa kukamilika.
Pia Makamba anadaiwa kuvunja sheria za nchi kwa kufanya mazungumzo ya mradi wa LNG kuwa siri, kinyume na sheria inayotaka vipengele vya MKATABA utakaosainiwa mwezi huu viwekwe wazi na upitishwe na Bunge.