Uchaguzi 2020 January Makamba asema hana uhakika kama atagombea Ubunge 2020

Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kwa sasa bado hana uhakika kama atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema atafanya uamuzi Desemba mwaka huu atakapokuwa mapumzikoni.

“Sina uhakika juu ya hili, sina hakika kama nitahitaji tena kugombea ubunge mwakani. Nitafanya maamuzi sahihi nikiwa mapumzikoni Desemba mwaka huu,” ameandika Makamba.

Makamba amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano, kabla Rais Dk. John Magufuli hajatengua uteuzi huo mapema mwaka huu!

Pia amewahi kugombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, lakini alibwagwa kwenye kura za maoni ambapo chama chake kilimteua aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Chanzo: Mtanzania
Kama hana uhakika, kwa nini kaongelea hili?

Aliulizwa swali?
 
Hapana, ana zaidi ya 45, japo sio mzee. Yeye ni baadhi ya watu walioendekeza siasa za hujuma, sasa zimemrudia anazikimbia. Kwa ujumla Januari hawezi siasa zisizo na mbeleko, na safari hii mbeleko imekatika.
Hapa nakuunga mkono na mguu
 
Mbunge ukishakaa jimboni miaka 5 na hakuna mabadiliko ni bora kubwaga manyanga...

Hii iwe utamaduni kwa wabunge wote.
 
Huyu kijana anapendwa sana jimboni kwake, kafanya mengi sana.
Hizi Kick za Wanasiasa achana nao kabisa, Hiyo Desemba atakuja na Ngonjela ooooohhhh Wazeee wa Bumbuli wamenifuata na kunisihi saaaana niendeleee na Kijiti cha Kusogeza mbele maendeleo ya Jimbo letu pendwa la Bumbuli hivyo sina budi kuendelea. Time will Tell
 
Mkakati wao kuelekea ACT yeye na Membe umesukwa umekamilika. Tusubiri ingawa inaweza kuwa technic pia ya urais 2020 ndani ya chama.
 
Kwani si alisha samehewa? Yale yalishapita!!!!!!!!!!!!!!

Inaonekana kuna watu hawajamsoma JIWE kuwa ni mtu wa kulpiza visasi na mnafiki mkubwa! BIFU bado linafukuta kati ya Jiwe na Mzee Makamba na swahiba wake Kinena hivo Januari na Nape nna hakika hawata chomoka 2020…!
 
Hapana, ana zaidi ya 45, japo sio mzee. Yeye ni baadhi ya watu walioendekeza siasa za hujuma, sasa zimemrudia anazikimbia. Kwa ujumla Januari hawezi siasa zisizo na mbeleko, na safari hii mbeleko imekatika.
Umenena vyema mkuu kipindi hiki hakuna ujanjaujanja na fitina ndani ya chama
 
Naona watu wameelewa vibaya kauli ya February, mtu kasema atasema kipindi chake cha likizo mwezi Disemba watu washapata cha kuandika,
Anyway huko bumbuli watakua na mengi zaidi juu ya utendaji kazi wake, binafsi namkumbuka katika sakata la mifuko ya plastic
 
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kwa sasa bado hana uhakika kama atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema atafanya uamuzi Desemba mwaka huu atakapokuwa mapumzikoni.

“Sina uhakika juu ya hili, sina hakika kama nitahitaji tena kugombea ubunge mwakani. Nitafanya maamuzi sahihi nikiwa mapumzikoni Desemba mwaka huu,” ameandika Makamba.

Makamba amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano, kabla Rais Dk. John Magufuli hajatengua uteuzi huo mapema mwaka huu!

Pia amewahi kugombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, lakini alibwagwa kwenye kura za maoni ambapo chama chake kilimteua aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Chanzo: Mtanzania
Nape na Ngereja nao wangefanya hivyo hivyo. Maana Wajidhalilisha saana! Mwanaume ni yule anayesimamia Msimamo wake na si hawa Wametia aibu kabisa. Watanzania wamewadharau saana!
 
Umenena vyema mkuu kipindi hiki hakuna ujanjaujanja na fitina ndani ya chama

Fitina na ujanjaujanja ndani ya ccm upo sana, ila yeye sio kipenzi cha muendesha fitina mkuu wa chama wa sasa.
 
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kwa sasa bado hana uhakika kama atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema atafanya uamuzi Desemba mwaka huu atakapokuwa mapumzikoni.

“Sina uhakika juu ya hili, sina hakika kama nitahitaji tena kugombea ubunge mwakani. Nitafanya maamuzi sahihi nikiwa mapumzikoni Desemba mwaka huu,” ameandika Makamba.

Makamba amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano, kabla Rais Dk. John Magufuli hajatengua uteuzi huo mapema mwaka huu!

Pia amewahi kugombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, lakini alibwagwa kwenye kura za maoni ambapo chama chake kilimteua aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Chanzo: Mtanzania

Badilisha heading, amesema mpaka December ndio atajua
 
Back
Top Bottom