Uchaguzi 2020 January Makamba asema hana uhakika kama atagombea Ubunge 2020

Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kwa sasa bado hana uhakika kama atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema atafanya uamuzi Desemba mwaka huu atakapokuwa mapumzikoni.

“Sina uhakika juu ya hili, sina hakika kama nitahitaji tena kugombea ubunge mwakani. Nitafanya maamuzi sahihi nikiwa mapumzikoni Desemba mwaka huu,” ameandika Makamba.

Makamba amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano, kabla Rais Dk. John Magufuli hajatengua uteuzi huo mapema mwaka huu!

Pia amewahi kugombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, lakini alibwagwa kwenye kura za maoni ambapo chama chake kilimteua aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Chanzo: Mtanzania

Ndio uzuri wa elimu hata hivyo hana uhakika ktk mchujo
 
Hizi Kick za Wanasiasa achana nao kabisa, Hiyo Desemba atakuja na Ngonjela ooooohhhh Wazeee wa Bumbuli wamenifuata na kunisihi saaaana niendeleee na Kijiti cha Kusogeza mbele maendeleo ya Jimbo letu pendwa la Bumbuli hivyo sina budi kuendelea. Time will Tell

Ikitokea hivyo ujue ndani mwao kumepoa
 
Naona watu wameelewa vibaya kauli ya February, mtu kasema atasema kipindi chake cha likizo mwezi Disemba watu washapata cha kuandika,
Anyway huko bumbuli watakua na mengi zaidi juu ya utendaji kazi wake, binafsi namkumbuka katika sakata la mifuko ya plastic
Angesubiri huo mwezi wa 12....basi.
na sio kupima upepo
 
Hii Gia alishaitumiaga, baadae anakuja zuga eti wazee wamemtuma na watamchukulia form.
 
Inaonekana kuna watu hawajamsoma JIWE kuwa ni mtu wa kulpiza visasi na mnafiki mkubwa! BIFU bado linafukuta kati ya Jiwe na Mzee Makamba na swahiba wake Kinena hivo Januari na Nape nna hakika hawata chomoka 2020…!
Lakini wangetazamwa pia kwa huruma na umri wao wote bado wadogo ili waweze kujifunza zaidi. Ukiwapa RED KADI wanakosa mechi zote zambeleni.
 
Pia amewahi kugombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, lakini alibwagwa kwenye kura za maoni ambapo chama chake kilimteua aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Aliingia katika 3 bora
 
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba amesema kwa sasa bado hana uhakika kama atagombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amesema atafanya uamuzi Desemba mwaka huu atakapokuwa mapumzikoni.

“Sina uhakika juu ya hili, sina hakika kama nitahitaji tena kugombea ubunge mwakani. Nitafanya maamuzi sahihi nikiwa mapumzikoni Desemba mwaka huu,” ameandika Makamba.

Makamba amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Muungano, kabla Rais Dk. John Magufuli hajatengua uteuzi huo mapema mwaka huu!

Pia amewahi kugombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, lakini alibwagwa kwenye kura za maoni ambapo chama chake kilimteua aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.

Chanzo: Mtanzania
Atalima mapeasi shida i wapi?
 
Back
Top Bottom