January Makamba awe kipimo cha Mawaziri wa Rais Samia

Kamwambie aliyekutuma hatokuja kuwa Rais wa nchi hii na hizi pesa anazowaibia watanganyika kuna siku atazitapika
 
twell said. Umeeleza vizuri sana Luqman. Viongozi wote kuanzia ngazi ya kitaifa hadi vijjji watende kama Makamba tutafanikiwa

ek
 
Umeongea meeeeeengi ya kinadharia, lakini hujabalance stori kwa kutueleza hayo maono ya Waziri January yanaelewekaje na wananchi wa kawaida? Kiukweli, huku site hakuna anayejua chochote ulichoongea.
 
🤔🤔🤔🤔
 
Kadiri wanavyomchukia Makamba ndivyo Mungu anavyozidi kumpandisha!
 
Huyu Jamaa hajui Jo Description ya Wizara yake ya Nishati
 
Kama ni mpenzi wa vipindi vya mapishi US popular BBQ joints zao unakuta nyama inakufukizwa na moshi kwa masaa kadhaa, inahifadhiwa siku kadhaa baada ya hapo halafu ndio inachomwa slow cooking moshi tena unahusika.

Ukienda huko Alaska maporini wanaoishi huko winter kupata chakula ni shughuli pevu na nyama yao ni ya kuwinda au samaki; kabla ya winter watu wanafanya stocking na kuhifadhi mbinu ni smoking.

If smoking was that poisonous nadhani duniani tungekufa wengi sana mishikaki tunayochoma imejaa moshi.

Sumu ya carbon fuels zote iwe makaa ya mawe, gas au petrol ni kuvuta fumes directly.

Hivi umeshajiuliza mtu anatambua watu wengi ni self reliant wanakula wanancholima na kuvuna; na namna yao ya ku-preserve food stock ni smoking. Hivi unadhani hawa watu kwa tabia na njia waliyozoea kutunza chakula wataacha kutumia kuni na mkaa kabla ya kujua mbinu za kuhifadhi chakula kwa muda mrefu kwanza.

Achilia mbali mkoa mzima wa mwanza useme uamie kwenye kupikia gas let’s say ata miaka mitatu ijayo; wanafahamu hiyo reserve inayotakiwa kuwa huko kila siku na security ya supply measures zinazotakiwa kuwepo kwanza.

January ni mtu mwenye kuongea ujinga mara nyingi amumuoni tu; asijuchuze kuweka tarehe na kutangaza zuio hizo shida atakazowapa watu ni balaa na policy yenyewe sio cheap kabisa.

Yaani kabisa mtu ulieenda shule ukapata ata ka degree kakuunga unga unaweza sema January ni clever, mtu ambae mara nyingi anaongea ujinga mtupu. Angekuwa mwerevu angeua ndege wawili kwa jiwe moja kupitia ziara yake ya kugawa majiko ilitakiwa kuwa sambasamba na primary research ya sera; then wajipange wanaanza vipi na hii sera hatua kwa hatua. Ki wilaya, mikoa au kitaifa kutokana na sababu luluki za majibu ya research yao.

Ni hivi the whole thing is just waste of taxpayers money.
 

NENO!
Ovyo sana jamaa!
 
Mbona kwenye kampeni hiyo ya clean cooking waziri anaipigia chapuo kampuni ya gesi ya taifa gas. Kwanini asizungumzie matumizi ya gesi bila kutembea na kugawa mitungi ya kampuni fulani?

Alafu mbona maelezo yanatoka kisiasa siasa? Miaka nenda rudi mbona hao madaktari wa muhimbili hawajawahi kutueleza hayo? Au January Makamba anawazidi elimu kuhusu mambo ya afya na kukaa ICU.
 
....mwanakijiji akishapata jiko na mtungi ,maisha ysnakua mepesi..." Hapa luqman umekosea kidogo.

Hili suala nikiwa karibu na January ntamueleza ukweli. Ni idea nzuri Ila utekelezaji wake ni ngumu na ni hauwezekaniki.

Nusu ya watanzania ni maskini ambao hataa Milo mitatu hawawezi kupata. Leo Hawa uwaambie waache kuokota kuni bure waanze kutumia gesi ambayo wataipata kwa gharama ni kujiongopea tu. Mjini hapa wenye vippato kidogo tu Ila kumudu gesi wameshindwa.

Mimi niliwanunulia wazazi wangu jiko la gesi kubwa na nikawa nawajazia, Ila baadae nilishindwa maana kwa mwezi inaweza kuisha Hadi Mara 3. Wakati gunia 1 la mkaa wanatoboa mwezi mzima
 
mama yangu katumia kupikia kuna miaka 50 na wala hajalazwa ICU
 
Ndo huyo Kigogo kakutuma uje utuandikie hiyo insha siyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…