Niko Dar,maeneo mengi haipiti wiki bila umeme kukatwa,na hali ilizidi kuanzia last year 2020.
Mfano huku kwetu ni guarantee kila alhamisi lazima umeme ukatwe.Ukiwauliza sometimes watakwambia hitilafu,wakati mwingine wanasema ni scheduled maintenance ingawa hawatoagi taarifa eneo husika,ni sisi wakorofi ndio tunajuaga sababu ya kuwasumbua,maana wengine wetu umeme ndio ajira yetu hapa mjini.
I wish ningekuwa na uwezo wa kuzileta post zangu zote nilizoandika kule uzi wa Tanesco kila mara umeme unapokatika maeneo mbalimbali nnapokuwepo.Ni mlolongo wa post za kila wiki,kila mwezi takriban miaka yote miwili ya hivi karibuni.
Sasa mtu kama mimi ninayelipia umeme wangu,nimenunua mita na kufunga,naishi kwa ajili ya umeme,halafu nakutana na hali hii ya kukatika umeme mara kwa mara kwa miaka sio wiki,ni miaka,then nasoma jibu la waziri wa nishati kama hivi,unategemea ntaelewa kweli?
Baadhi yenu mnazungumzia tatizo hili kama vile lina miezi miwili tu,ilhali ni tatizo la muda mrefu tangu miaka ya mwisho ya Magufuli(late 2019 then 2020 baada ya election limezidi mpaka leo) hili lipo.Nani atakuelewa ukisema ni scheduled maintenance?
Uongozi ni kitu cha mwendelezo,sisi tunauliza kiti cha waziri,regardless ni Makamba,Kalemani etc,wawajibike.Ukimrithi Kalemani unapaswa kuyatolea majibu hata yale yaliyofanyika akiwepo yeye.Ni jambo lisilo na mantiki mtu azungumze kama vile kuna mapinduzi yametokea na sasa serikali yake ni mpya.Makamba azungumze kama Waziri wa Nishati,sio kama Makamba.
Tatizo limedumu muda mrefu,halijaanza juzi,so ni scheduled maintenance na hitilafu all through the year?Then tunalipia kitu gani sasa?Hata gari haiendi service kwa kiwango hicho.
Kama Dar umeme unasumbua hivi,then ni wapi Tanesco wanaweza kutuonyesha wanajitahidi kutoa huduma bora?
Halafu kwanini hawasemi hadi waulizwe?
Kitu cha mwisho baadhi yenu mjue watanzania wana makovu.Miaka iliyopita especially before Magufuli waliumizwa sana na umeme.
Unapokuja kwetu kuzungumzia umeme uwe na hoja za kueleweka....SABABU TUNAWAJUENI MAMBO YENU VIZURI TU,mmetuchosha kwa miaka mingi.Shirika lile lilikuwa zuri sana,lakini nyie viongozi mmelivuruga.Kama sio nyie mlioko hivi sasa basi wenzenu waliopita na mzigo wao mnaubeba nyinyi, hamuwezi kubisha,ni matakwa ya uongozi.Kwa hiyo mkija kwetu kuzungumza muongee ukweli,acheni uongo kwa mambo yanaumiza jamii.Umeme ni sensitive,uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa taifa.Msiufanyie utani utani!