January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

Aisee! Yeye si ndio alisema amri hizi ziliwafanya Tanesco washindwe kufanya ukarabati ambao sasa hivi unafanyika na ndio sababu ya umeme kukatika hovyo?!! Ama kweli mwanasiasa akikwambia sasa hivi ni usiku toka nje kahakikishe.

Sababu alizotoa January kwa umeme kukatika ni kwamba kuna matengenezo yanayofanyika ndio sababu ya umeme kukatika. Je katika hizo wiki mbili alizowapa matengenezo yatakuwa yamekamilika hata umeme usikatikekatike? January should learn to be thorough otherwise these impromptu answers to sensitive questions will ruin his credibility as an able minister!
 
Pia ali-tweet 'tanesco walikuwa wanalazimishwa kutokata umeme hivyo kushindwa kufanya ukarabati' sasa hii kauli yake si ndio anarudia yale yale?
 
habari yenyewe ya mwezi September kabla wahindi hawajampelekea dili la kuuza majenereta saizi tuko November
Hapa nilikuwa nashindwa ku comment sijui hii habari ya lini, naona uzi mpya ukisoma habari 17 September najiuliza au typing error maana kama habari ya Sept halafu leo Nov na wiki 2 zilishapita umeme ndio kwanza wanakata kwa mwendo wa SGR uzi ufungwe tu hakuna cha kuchangia hapa.
 
Mkuu na wewe ndiyo unazidi tu kunichanganya zaidi!

Septemba17 hadi leo ni wiki2 kweli!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
N
Nonsense
 
Mkuu na wewe ndiyo unazidi tu kunichanganya zaidi!

Septemba17 hadi leo ni wiki2 kweli!

Sent using Jamii Forums mobile app
Waziri wa Nishati, January Makamba ametoa wiki mbili kuhakikisha hakuna tatizo la kukatika umeme nchini Tanzania.
Leo Ijumaa Septemba 17, 2021 Makamba amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) baada ya malalamiko ya wananchi kuongezeka kuhusu kukatika kwa umeme.
 
post imewekwa jana ila ukisoma tarehe za Sept sasa sielewi ni imekosewa tu habari ya zamani mtu kaibeba tu kaitupia jana hata sielewi
 
Marekebisho ya mitambo ya tanesco yanaisha lini ili tupate umeme wa uhakika?
====
Kuna uwezekanao kunamaneno kalishwa..hasa kuipongeza tanesco
 
Leo Ijumaa Septemba 17! Mbona sielewi pakuanzia kwani inaonekana kama alitembelea jana Jamatatu Nov 15! Post iliwekwa jana Nov.15.
 
Hii nayo chadema watapinga as if wanataka umeme ukatike

USSR
Tunapinga kwa sababu bado unakatika!
Si bado unakatika ndugu zangu?
Ccm chama cha wanafiki,.walozi na wauaji..zilongwa mbali, zitendwa mbali.
 
Kuna watu wana damu ya uongozi na kuna wanaojipaka mafuta ya uongozi. Mwenye damu hata ukimwamsha usingizi usiku wa manane, jibu lak linasikilizwa kwa uhakika na kuwekwa maananani na anaowaongoza; yule mwenye kujipaka mafuta, ukimwamsha usiku wa manane atatoa jibu ambalo watu hawatatilia maanani mpaka akaoge ajipake mafuta kwanza. Na hata akishajipaka mafuta ya uongozi, akipigwa jua kidogo tu akatoka jasho au akinyeshewa mvua, mafuta yote yanaondoka anakuwa yule yule asiyetiliwa maanani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…