January Makamba: Umeme mwisho kukatika wiki mbili, baada ya hapo nitafukuza watu

Yaani TANESCO ikusanye zaidi ya trillion 2 kwa mwezi wakati makusanyo ya nchi nzima kutoka vyanzo vyote vya mapato ya serikali hayafiki trillion 2 ?? Mkuu ukiwa unaongea jitahidi kujisikiliza ili uone wapi unakosea. Hebu tupe makusanyo ya nchi kwa mwezi.
Hata mimi nilishangaa haya makusanyo anayosema Waziri ama mwanzisha thread kahamua kujiandikia tu
 
Hao wateja si ni idadi ya nyumba mkuu. Na nyumba moja yaweza kuwa na mtu zaidi ya mmoja.
Ni kweli nyumba inaweza kuwa na watu wengi. Ila kila nyumba ambayo iko connected ni mteja moja.

Kwa Dar yenye watu karibu 6 million kama Kila nyumba ina watu 6, hapo tayari ni wateja zaidi ya 1 million. Ndiyo maana nahisi kutakuwa na lots of illegal connections au data za kuwa umeme umesamazwa kila corner ya nchi si za ukweli.
 
Kichwani mwako inaonekana umejaza tope tu, nimesema wwe unapinga data za waziri Makamba kuwa sio,tupe za kwako basi tukuamini,unabaki unatema pumba tu,hivi unafikiri Makamba anadanganya ili kupata nini?,kama si chuki zako binafisi zidi ya tanesco
Kumbe bado huelewi nilichokuandikia hapo?
Maana yangu ni kwamba ukilaza uliokujaa haukupi uwezo hata wa kuangalia takwimu za uongo ulio dhahili na kuutambua.

Huwezi kunidai takwimu mimi; mimi natambua tu takwimu maghumashi, uwezo huo ninao kuliko ulivyo wewe usiyeweza hata kutambua uongo uliowazi kwa kuamini tu kwamba kwa kuwa umesemwa na waziri basi ndio ukweli!
 
Waziri wa Nishati January Makamba ametembelea ofisi za Tanesco na kulipongeza shirika hilo kwa kufikisha wateja 3.2 millioni ndani ya miaka 5 iliyopita.

Wanaoliwezesha kukusanya zaidi ya trillioni 2 kwa mwezi na kulifanya kuwa shirika pekee linalokusanya fedha nyingi nchini.

Makamba ametoa wiki mbili kwa shirika hilo kuacha kukata umeme la sivyo ataanza kuwafukuza kazi mameneja wote wazembe wote wanaokata umeme.

--

Waziri wa Nishati, January Makamba ametoa wiki mbili kuhakikisha hakuna tatizo la kukatika umeme nchini Tanzania.

Leo Ijumaa Septemba 17, 2021 Makamba amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) baada ya malalamiko ya wananchi kuongezeka kuhusu kukatika kwa umeme .

Makamba amesema atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake na malalamiko ya kukatika kwa umeme yakiendelea kujitokeza, wahusika wote watachukuliwa hatua.

"Ndani ya wiki mbili sitaki kusikia kukatika kwa umeme nikisikia kuna malalamiko nitachukua hatua Kwa wahusika walioshindwa kutekeleza wajibu wao," alisema Makamba.

Alisema wanahitaji Shirika hilo lijiendeshe kibiashara, kisasa ambapo mabadiliko yenye tija yataongeza ufanisi na mapato yataongezeka.

"Shirika lina wateja wa mita 3.2 milioni wanakusanya zaidi ya Sh2 tirioni na hakuna Shirika lolote hapa nchini linalotengeneza fedha hizo, hivyo wateja wanatakiwa kuongezeka ili Shirika liweze kujiendesha" amesema

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uzalishaji wa Umeme, Pakaya Mtimakaya amesema wameyapokea maagizo hayo na watayafanyia kazi.

Chanzo: Waziri Makamba atoa wiki mbili kumaliza tatizo la umeme
Ndugu Waziri wetu mpya, ulikaa nao wakakuelezea kisa cha kukatika umeme mara kwa mara linaweza kutatulika ndani ya wiki mbili. Je sio tatizo linalohitaji fedha nyingi/ or wide interventions ambalo lipo nje ya hao mameneja wa Mikoa? Usije waonea watu bure go into the core problem do not go into shallow analysis and give unachievable orders. You will go back to the former Minister's style. Tumesikia kwenye vyombo vya habari TANESCO wanabadili nguzo za miti kuweka za concrete hili haliwezi kuwa ni majawapo la chanzo cha kukatika kwe umeme kupisha kazi hii?
 
Kumbe bado huelewi nilichokuandikia hapo?
Maana yangu ni kwamba ukilaza uliokujaa haukupi uwezo hata wa kuangalia takwimu za uongo ulio dhahili na kuutambua.

Huwezi kunidai takwimu mimi; mimi natambua tu takwimu maghumashi, uwezo huo ninao kuliko ulivyo wewe usiyeweza hata kutambua uongo uliowazi kwa kuamini tu kwamba kwa kuwa umesemwa na waziri basi ndio ukweli!
Kama huna takwimu ,unajuaje hizo takwimu ni magumashi
 
Simbachawene alitwambia matatizo ya upatikanaji umeme itakuwa historia gesi ikifika Dar es Salaam. Gesi imefika Dar es Salaam lakini bado matatizo yapo pale pale.

Tunajua Simbachawene siyo Makamba.
Je gas ilipofika Dar es Salaam tumeitumia alisimia ngapi? Hadi sasa kama uongozi ulipobadilika walienda kujenga Bwawa la Nyerere na kuacha kununua generators za kufua umeme kosa ni la Waziri? Hapa ni shida ya prioritisation tu. Nchi inajengwa kama building blocks not otherwise, tutaenda in circles and circles tutakuwa pale pale siku zote.
 
Kama huna takwimu ,unajuaje hizo takwimu ni magumashi
Ina maana hujui takwimu ni kitu gani, na kwa maana hiyo hata ukileytewa takataka utaziita takwimu. Hivyo ndivyo unavyojitambulisha hapa wewe.
 
Sio kweli kaka mimi ni ninauhusika flani, kampuni za kutengeneza cement tu kwa uchache, twiga, simba na tembo cement hizi kwa mwezi zinalipa matumiz ya umeme zaid 1.8b, hivyo kwa mahesabu ya 2.0b aliyosema ni kweli na kukujuza tu ni zaid ya 2.3billions kama hutaki haulazimishwi na alicho ongea wazir kuhusu makusanyo ni kweli, isipokua sisi tunahitaji umeme wa uhakika usio katika hapo serikali itapata mapato zaid na sisi wananchi tutafurah
Huo mkwala Mbuzi, suala la kukatika umeme c la wiki mbili utafukuza wote na mwishoe utajifukuza. Shirika limekuwa likiendeshwa kisiasa kwa muda mrefu Sana, pia shirika linamadeni sugu zaidi ya 1.1 trilioni,
Makusanyo ya tanesco ni around bil90 kwa mwezi na kwa mwaka around 1.4 trilioni, hiyo 2.0 trilioni kwa mwezi ni uongo.
Hakuna Jambo gumu kutatulika tanesco Kama kukatika kwa umeme, shida kubwa ni ubora wa vifaa vilivotumika na uchakavu wa miundombinu ambayo hayarekebishiki kwa wiki mbili
 
Sio kweli kaka mimi ni ninauhusika flani, kampuni za kutengeneza cement tu kwa uchache, twiga, simba na tembo cement hizi kwa mwezi zinalipa matumiz ya umeme zaid 1.8b, hivyo kwa mahesabu ya 2.0b aliyosema ni kweli na kukujuza tu ni zaid ya 2.3billions kama hutaki haulazimishwi na alicho ongea wazir kuhusu makusanyo ni kweli, isipokua sisi tunahitaji umeme wa uhakika usio katika hapo serikali itapata mapato zaid na sisi wananchi tutafurah
Safi mkuu
 
Ina maana hujui takwimu ni kitu gani, na kwa maana hiyo hata ukileytewa takataka utaziita takwimu. Hivyo ndivyo unavyojitambulisha hapa wewe.
[emoji1787][emoji1787]
 
Waziri wa Nishati January Makamba ametembelea ofisi za Tanesco na kulipongeza shirika hilo kwa kufikisha wateja 3.2 millioni ndani ya miaka 5 iliyopita.

Wanaoliwezesha kukusanya zaidi ya trillioni 2 kwa mwezi na kulifanya kuwa shirika pekee linalokusanya fedha nyingi nchini.

Makamba ametoa wiki mbili kwa shirika hilo kuacha kukata umeme la sivyo ataanza kuwafukuza kazi mameneja wote wazembe wote wanaokata umeme.

--

Waziri wa Nishati, January Makamba ametoa wiki mbili kuhakikisha hakuna tatizo la kukatika umeme nchini Tanzania.

Leo Ijumaa Septemba 17, 2021 Makamba amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) baada ya malalamiko ya wananchi kuongezeka kuhusu kukatika kwa umeme .

Makamba amesema atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake na malalamiko ya kukatika kwa umeme yakiendelea kujitokeza, wahusika wote watachukuliwa hatua.

"Ndani ya wiki mbili sitaki kusikia kukatika kwa umeme nikisikia kuna malalamiko nitachukua hatua Kwa wahusika walioshindwa kutekeleza wajibu wao," alisema Makamba.

Alisema wanahitaji Shirika hilo lijiendeshe kibiashara, kisasa ambapo mabadiliko yenye tija yataongeza ufanisi na mapato yataongezeka.

"Shirika lina wateja wa mita 3.2 milioni wanakusanya zaidi ya Sh2 tirioni na hakuna Shirika lolote hapa nchini linalotengeneza fedha hizo, hivyo wateja wanatakiwa kuongezeka ili Shirika liweze kujiendesha" amesema

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Uzalishaji wa Umeme, Pakaya Mtimakaya amesema wameyapokea maagizo hayo na watayafanyia kazi.

Chanzo: Waziri Makamba atoa wiki mbili kumaliza tatizo la umeme
Litakuwa jambo zuri provided siyo hekaya za Abnuwasi. 2 trilion ni pesa nyingi na zikitumika vizuri miundombinu ya umeme haitakuwa na mfano kwa east and central Africa
 
Maneno mengi sana vitendo zero
 
Hapa kwanini nisiweke tangazo langu aiseeh!
0756060183
Screenshot_20211113-214032_Facebook.jpg
 
Mkuu mbona bei ya iyo nyumba ni rahisi Sana. Kweli bei ni iyo? Am interested Niko tayari kununua. Je zinapatikana zingine zenye bei kama hizo? Nahitaji kama ishirini hivi.
Hahaa aiseh mkuu si utajiri huu unanitangazia jamani!!
Yote kwa yote karibu sana nyumba ninazo nyingi za kutosha karibia kila kona ya huu mji mijengo ipo tena ziko za bei rahisi zaidi
Screenshot_20211113-204138_Facebook.jpg
Screenshot_20211113-213237_Facebook.jpg
Screenshot_20211113-204006_Facebook.jpg
Screenshot_20211113-203515_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom