Japan kulipa $536 Million kwa makampuni yake 56 yahame kutoka China, yarudi nyumbani au nchi nyingine za Asia

Ukweli ambao hawapendi kuusikia.....
 
Marekani nae sio mkandamizaji?? Huyo ndo mnafiki mkubwa.........wote hapo hovyo hakuna wa maana sema tu mmoja anaona anazidiwa ndo anahangaika kujitetea ila hakuna msafi hapo kati ya Mmarekani na Mchina
Huwezi mlinganisha USA, na MCHINA, hata siku moja, mchina ni mnyonyaji hasa, na yeye kwake Demokrasia, ni msamiati, hata iweje huwezi sikia ana toa hata sauti kuwa kuna ukiukwaji wa Demokrasia, kwenye nchi husika, madam mambo yake yanakwenda vizuri!!! Wazungu wana unafuu sana!! Hiyo misaada gani ya ki ubinadamu anayotoa?? Bora mzungu kuliko, mchina na mrusi!!
 
Soma Tena wanapewa hela wakihama
 
Ni Mapema sana Jambo lolote wanaofanya wazungu wanaangalia mbali sana, impact yake itaonekana baadae na sio leo kusema mbinu zimegonga mwamba ni uongo,

Marekani anachukulia advantage ya bifu la china na majirani zake, china ana ugomvi wa mipaka karibua na nchi zote alizopakana nazo including Russia, India, Vietnam, taiwani, Japan, Philippines, malysia, na indonesia
 
In 10 yrs to come china itakua nje ya 10ten mtaniambia...amuulize Mrusi atamwahadithia sawa sawa
Hii siyo kweli; ukiangalia mlolongo wa matukio yaliyosababisha urusi kuanguka, haujaigusa China. Kosa ambalo nchi za Magharibi zilifanya miaka ile ya tisini na mwanzoni mwa 2000 ni kuhamisha viwanda vyao wakapeleka china kwa sababu ya cheap labor, halafu China ikadukua teknolojia yao yote. Ni teknolojia hiyo ambayo china walidukua ndiyo inayowapa nguvu leo. Sasa basi China ikajijenga zaidi kwa kuweka tentacles zake Afrika na Amerika ya kusini kibiashara zaidi ya kijeshi, huku ikijijenga kijeshi ndani. Makosa ya urusi enzi zake ilikuwa ni kwamba wao walikuwa wanawekeza kijeshi tu, hawakuwekeza kibiashara, kwa hiyo walipoanguka walianguka wazima wazima.

Kosa kubwa la Marekani litakalofanya China iendelee kupaa ni kwa sababu ya kuwa wanajiondoa kwenye ulingo wa kimataifa na vile vile kuvunja alliances ilizokuwa nazo. Rais trump anaangalia mambo ya dunia kwa lens ndogo sana ya kuuza nyumba na kupata faida lakini haiongozi Marekani strategically. Kwa mfano marekani kujitoa kwenye TPP lilikuwa ni kosa sana, kwani walipojitoa tu China ikaingia na kukamata hizo nchi za Phillipenes na nyingezo za ukanda huo. Hata kama viwanda vya Japan vitahamia nchi nyingine za Asia, havitaacha pengo kubwa kabisa China kwa sababu tekenolojia yao yote ilishdukuliwa, na China ina influence leo kwenye nchi nyingi za Asia leo kwa sababu ya misaada wanayowapa.
 
Acha uongo china ana beef na majirani zake kazikamataje,
 
Acha uongo china ana beef na majirani zake kazikamataje,
Haya maneno ya lugha za matusi za "ACHA UWONGO" yanaharibu mjadala wote. Ningejibu kwa nini nimesema hivyo lakini ninapenda kuwa najadiliana na mtu anayesikiliza na kutoa mawazo ya upande wake kuliko kubishana kutumia kivuli cha "Uwongo" na kupersonalize mjadala.
 
Kwenye hiyo taarifa hujaelewa nini? Maana ya serikali kutenga hizo pesa ni kwa ajili ya kucover hayo uliyoandika hayawezekani.

Ingekuwa ni kujihamisha wenyewe hiyo ingekuwa ngumu.
 
Reactions: BAK
China ana mgogora wa mipaka na nchi 18 iweje Leo ghafla anaelewana nao ndo maana nikasema ni uongo
 
Wao wameshafanya analysis wakaona zinatosha, lakin anatokea mkazi wa kwa mtogole anapinga
Zinatosha kwa makampuni ya kitoto, wewe unayekaa Tokyo twambie kampuni gani zenye akili zitatosheka kugawana $500M kama subsidies. Kwanza unajua market shares za makampuni kama LG, Toshiba, HITACHI, etc.

Giants wa tech kama Samsung, Apple, Qualcomm, Huawei na wale wa bidhaa kama Adidas, Nike na wengine wanahesabu zaidi ya tens of billions in USD kutoka China.
Yani unamwambia LG atoke China kisa kuna vimilioni 500 vya kugawana. Gharama za plants, workforce, capital na mambo kibao hazifidiwi kirahisi.

Ni sawa na kumwambia Bakhresa ahamishe viwanda na aache wafanyakazi bara aende Zanzibar ajenge upya kisha aajiri wafanyakazi wapya. Utalipa na fidia ya kupoteza soko?
 
Unabishana na mtu anayeonekana hana elimu, that's why hawezi kutoa hoja bila kuweka maneno ya vijiweni.
 
China ana mgogora wa mipaka na nchi 18 iweje Leo ghafla anaelewana nao ndo maana nikasema ni uongo
Wewe unaongea tatizo dogo kati ya mambo makubwa. Angalia kuwa pamoja na Phillipines kugombana na China kuhusu ile bahari ya South China Sea, bado pai wanaitaka Marekani iondoe vituo vyao vya jeshi kutoka Phillipines, na bado wameendelea kuwa wanashirikiana kibiashara na na China zaid ya Marekani leo hii. Halafu angalia Uhusiano kati ya China na Laos, Singapore, Thailand, Pakistan, Mynamar kwa mfano. Friction baina yake na Vietnam na Taiwan siyo kigezo kikubwa cha kupima influence ya China kwenye eno hilo.
 
Dola za Marekani milioni 500+ kwa makampuni yote hayo ni kidogo mno. Huawei ilikuwa iwekeze mradi wa dola za Marekani bilioni moja nchini Uingereza.
Investments, refund, compasations, ni mambo 3 tofauti kabisa mkuu...huyo alikua anaweka mtaji, kwan japan angetaka wekeza hata kama ni 3B angeshindwa?
 
Philippines anaepush ni dutete, ambaye akiondoka akija rais mwingine atawarudia marekani, wa-philipines wengi hawasupport hiyo move kwa sababu diaspora wengi wapo marekani

Marekani hawez ondoka kienyeji enyeji sababu aliingia mikataba
 
Mtanzania wa kumtogole huwezi mbishia mjapani aliyesema atatoa million 500, Tanzania ndo nji pekee watu wanabishia watu na professional zao

apple, Nike, addidas, Samsung je hizo ni kampuni za kijapani, japani amesema ni kwa kampuni zake za kijapani tupende kujikita kwenye mada
 
Investments, refund, compasations, ni mambo 3 tofauti kabisa mkuu...huyo alikua anaweka mtaji, kwan japan angetaka wekeza hata kama ni 3B angeshindwa?
Angeshindwa kwa kukosa hela ya kutosheleza kuwekeza na kuendeshea biashara. Yani 1B inayowekeza China inakuwa ni zaidi ya hapo ikiwekeza Japan. Pia running costs zingekuwa kubwa nchini Japan.
Kama wangeweza kwa nini walienda China, kuna factors ambazo ziliwaweka uko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…