Japan ni magari pekee?

Japan ni magari pekee?

Nafikiri bidhaa nyingi za Mjapan ni bora kuliko za Mchina, lakini Mchina kaliteka kwa sehemu kubwa soko la Tanzania.
Mchina ni mjanja sana. Anajua waafrika wanapenda vitu vya bei rahisi hata kama havina ubora . Ndio maana kateka soko la afrika. Mjapan kashindwa kutengeneza vitu vya bei rahisi kwa kuwa anajali mno ubora.
 
Unaifahamu brand ya SONY?
Ndiyo, hasa miaka ya nyuma! Tulikuwa tukitaka kununua REDIO, chaguo la kwanza ni SONY. Sijui kwa sasa, lakini walikuwa na REDIO, TV, sijui na friji? Sikumbuki. Lakini kwa sasa ni kama vile "hawasikiki"
 
Kwa sasa hali ikoje? Naona kama vile ukiacha magari, bidhaa zingine karibia zote Mchina ndiye anayelilisha soko la Tanzania.
Kwa wanaozingatia Quality products....we go to Japan, kwa wanaopenda Broilers Mchina amejaza tele mtaani mpaka barabarani kwa bei yako tu
 
Japan ina viwanda vingi, vya magari vikiwemo.

Lakini bidhaa za Japan zinazoletwa sana nchini ni magari na, pengine, spea za magari.

Kwa nini baidhaa zingine za Japan si maarufu nchini?

Au kumepangwa kuwe hivyo, kwamba kwa magari Mjapan awe "supplier" wa Tanzania na bidhaa zingine awe Mchina?
Hamuwezi ku afford bidhaa za Japan(mpya). Hata magari ni kwasababu mnanunua ya miaka 20 iliopita vinginevyo ni serikali tu na watu wachache. ingeweza kununua. Bidhaa mnaxoweza kumudu ni low class kutoka China na ndio zimejaa Kariakoo.
 
Japan ina viwanda vingi, vya magari vikiwemo.

Lakini bidhaa za Japan zinazoletwa sana nchini ni magari na, pengine, spea za magari.

Kwa nini baidhaa zingine za Japan si maarufu nchini?

Au kumepangwa kuwe hivyo, kwamba kwa magari Mjapan awe "supplier" wa Tanzania na bidhaa zingine awe Mchina?
Japan zamani alikuwa electronics ila hilo taji kalipoteza si tu kwetu na kwingine. Mchina kamnyanganya taji la electronics. Ila bado anamataji ya kuunda materials zinazotumika kutengeneza fabs za kuunda processors
 
Umewahi jaribu vyakula vya kijapan? Waache walete magari na electronics tu. Maana siku wakileta vyakula vyao ..
Vikoje mkuu? Kama siyo sumu mbona vinalika tu? Na haviwezi kuwa sumu kwa sababu nao ni binadamu kama sisi.
 
Japan pia wana makampuni ya simu na hapa bongo wengi wanatumia used zake.
 
Mchina ni mjanja sana. Anajua waafrika wanapenda vitu vya bei rahisi hata kama havina ubora . Ndio maana kateka soko la afrika. Mjapan kashindwa kutengeneza vitu vya bei rahisi kwa kuwa anajali mno ubora.
Mkuu si kwa sababu tunapenda vitu bei rahisi. Watu huwa mnadhani mchina anauza sana afrika ila sio kweli. Mauzo ya mchina afrika hayafika hata 5% ya mauzo yake ya duniani kote.
Mchina bado anauza sana marekani bidhaa nyingi. Na takataka zote zilizoko kariakoo na nchi nyingine za afrika bado hazifiki hata asilimia 5 ya mauzo yake nje
 
Back
Top Bottom