Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Nilichogundua humu JF, MACHOGO wengi hawana elimu ya uraia.

Hoja zao nyingi kuhusu Muungano ni kama wauza nyanya za mafungu magengeni.

Yaani inatia kinyaa kwa kweli.

Halafu mtu anajiona ametoa zinga la point.
Hoja zako zipo wapi?
Je, Zanzibar wana Bajeti ya Ulinzi , Mambo ya ndani, nje, Wizara za muungano na taasisi zake?

Je, mikopo inayochukua ambayo si tatizo, watarudisha kwa utaratibu gani?
Ikiwa hawawezi kumalizana na Tanesco, mabilioni wanayokopa nani atakayelipa? Mtanganyika!

Tunasema, wakati umefika turudi rasimu ya Warioba ya mambo 7 . Tanganyika isimame na kujisimamia na Zanzibar nayo ijisimamie ikakope mtrilioni kadri inavyoweza.
 
Ndio vizuri kwani anakumbatia Muungano ni Zanzibar au Tanganyika?

Pili mbona Zanzibar wanataka kujitenga, kwani hawayaoni hayo? Jibu ni kwamba huu ni uzushi na wao kwa uchache wao wanaona watafika mbali wakiwa peke yao.
Ndio maana tunasema waende kukopa wenyewe hata matrilioni 1000. Mbona wameuza visiwa je, umesikia Mtanganyika akizungumzia hilo.

Habari ya kupitia JMT halafu mzigo wanamwachia Mtanganyika ni mbaya sana.

Tusaidiane kuidai Rasimu ya Mzee Warioba na mambo 7 tu, tena kwasasa Wazanzibar mtasaidia sana maana Rais wa JMT na SMZ ni Wazanzibar! tusaidiane ili muwe huru kuijenga Dubai yenu na Tanganyika izibe mashimo ya barabara zake. Hii habari ya kubebeshana Bill inachosha!
 
Ukigawanya kila mkoa wa bara utapata bil 22, mfano tabora irapata bil 22 wakazi zenji inalamba bil 231
 
We need to step up,mikopo hii kidogo ni aibu
 
Kwny kulipa inakuwa Muungano wa Nchi moja tu Tanganyika
Mie naona Tanganyika ndio imechukua mgao mkubwa, zilitakiwa zigawiwe sawa kwa sawa. Ni Muungano wa nchi mbili.
 
Kwani huu Muungano sisi tunaung'ang'ania una faida gani na sisi, kidhati kabisa mie sioni faida kwetu kwenye huu muungano, halafu kibaya zaidi ni sisi ndio tunafosi, wazanzibar wakitaka nchi yao inakuwa msala.
Kwa hili,tunaomba tuwaaxhe jamaa waende zao.no longer material,wale wazee waliwaza nini jamani kwenye muungano
 
Aliyekwambia hawawezi Kukopa nani? Wakitaka Kukopa wanalazimika kuomba kibali Bara,na Bara ndio wanatoa final decision..

Binafsi napenda Zanzibar ikae peke yake Ili iwe kama Dubai tuache kufuata mizigo mbali huko wakati tunaweza ifuata hapo Zanzibar tuu.
 
Hivi tutakapoanz kulipa mkopo Zanzibar nayo italipa fungu lake au ni bara tu itakayobeba mzigo wa deni?
Inayokopa ni Tanzania.
Inayolipa au kutakiwa kulipa ni Tanzania hiyo hiyo.
Hakuna sehemu Tanganyika au Zanzibar inalipa au itatakuwa kulipa madeni yaliyokopwa na TANZANIA.

Mkitaka kuhuisha hizo ndogo zenu kwanza vunjeni Muungano kila nchi iwe huru, halafu kama mnaona bado Muungano mnauhitaji anzisheni shirikisho full stop


Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Muungano tukiuvunja Wazanzibari wanaoishi bara watakuwa kama Wazanzibari wanaoishi UK, US, Canada, Sweden, Afrika Kusini n.k. Watahesabika kama Wazanzibari wengine wa diaspora, watakaribishwa nyumbani wasaidie kuwekeza na kujenga nchi. Michango yao itahitajika sana kuendeleza na kujenga Zanzibar. Mkiwafukuza huko watahamia nchi nyingine au watarudi nyumbani. Si unaona jinsi Wayahudi dunia nzima wanavyoisadia Israel kupata maendeleo?

SMZ inatambulika na CCM tuu. Haitambuliki umoja wa mataifa (UN), haitambuliki Arab League, haitambuliki pengine popote. Vunja rasmi huo unaoita muungano Zanzibar ijiendeshe. Nyie machogo mliochoka na muungano wapeni ushauri watu wa CCM waache fikra kama za huyu hapa

 
Hapa nakuunga mkongo. Ukiwauliza wanaoulinda huo muungano umeleta faida gani hawana majibu. Umaskini Zanzibar umezidi. Zanzibar ingeungana na nchi mama yao Oman leo hii Zanzibar ingekuwa kama Muscat. Utajiri wa mafuta ungechuruzika mpaka kufika Zanzibar. Makosa ni kuungana na nchi fukara iliyoitwa Tanganyaika iliyojaa watu wenye ukabila, ukanda, udini, ubaguzi, ufukara wamebaki kuirudisha nyuma Zanzibar na siasa chakavu.

#FreeZanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…