johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Zanzibar ni nchi walitakiwa wapate 50%.Hii hatari, mbona Zanzibar wamechukua mgao mkubwa hivyo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zanzibar ni nchi walitakiwa wapate 50%.Hii hatari, mbona Zanzibar wamechukua mgao mkubwa hivyo?
Mkuu mikoa mitatu mbona mingiHicho kizanzibar ambacho ukubwa wake ni sawa na mikoa3 ya Tz bara, why kila siku kinapokea misaada mikubwa lkn hakibadiriki?
Yaani miundombinu yao ya hovyo, huduma za kijamii hovyo, mipango miji hovyo, sas hizo pesa wanapelekaga wapi?
Hiyo zanzibar ilitosha kwa kuiwekewa robo bajeti ya Tz bara nakuifanya Zanzibar kuwa kama London [emoji23][emoji23][emoji23] au natania ndugu zangu???
Ukwel mchungu, bado kuna matumiz mabovu ya fedha na mikopo.
Mpka leo bado wanahangaika na miradi ya maji??
Nonsense
Hivi tutakapoanz kulipa mkopo Zanzibar nayo italipa fungu lake au ni bara tu itakayobeba mzigo wa deni?Serikali ya Japan imeipatia Tanzania mkopo wa shillingi billion 761.8 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo nchini!
Katika mkopo huo kisiwa cha Zanziba kimepewa mgao wa Tsh billion 218+
Kazi iendelee...
=====
View attachment 2108391
Serikali ya Tanzania na Japan zimesaini mikataba mitatu ya mkopo na msaada yenye thamani ya Yen za Japan bilioni 37.9 sawa na takriban shilingi bilioni 761.8 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ukarabati wa Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na Ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili.
Mikataba hiyo imesainiwa jijini Dar es Salaam, kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan, Bw. Naofumi Yamamura, kwa naiaba ya Serikali ya Japan.
Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mikataba hiyo, Bw. Tutuba alisema kuwa Mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma utatekelezwa kwa msaada wa Yen za Japan bilioni 2.73 sawa na takriban shilingi bilioni 54.79, ukihusisha Ukarabati wa gati za mashariki na kaskazini mwa Bandari ya Kigoma, ukarabati wa majengo ya kushushia abiria na mizigo, ukarabati wa barabara zilizopo katika Bandari hiyo na ujenzi wa majengo mapya ya abiria na mizigo.
“Bandari ya Kigoma ilijengwa katika kipindi cha mwaka 1912–1927 na imekuwa bandari muhimu katika kusafirisha mizigo na abiria kwenda nchi jirani za Burundi, DR Congo, Zambia na mikoa iliyopakana na Kigoma, hivyo kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo kutachangia kuongeza ufanisi wa Bandari, kutoa fursa za ajira, kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kuchochea shughuli za kiuchumi na kuchochea biashara kati ya Tanzania na nchi hizo jirani” alisema Bw. Tutuba
Alisema kuwa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji Zanzibar, utatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Yen za Japan bilioni 10.86 sawa na takriban shilingi bilioni 218.382 ambapo mradi huo utahusisha kujenga na kukarabati miundombinu ya maji Mjini Zanzibar.
Kama ni nchi waende wakope wenyeweZanzibar ni nchi walitakiwa wapate 50%.
I agreeHuu Muungano ni wa kinyonyaji kwa Tanganyika,..we need our country back
Tanganyika ndio mnawabania!Kama ni nchi waende wakope wenyewe
Ni jambo jemaSerikali ya Japan imeipatia Tanzania mkopo wa shillingi billion 761.8 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo nchini!
Katika mkopo huo kisiwa cha Zanziba kimepewa mgao wa Tsh billion 218+
Kazi iendelee...
=====
View attachment 2108391
Serikali ya Tanzania na Japan zimesaini mikataba mitatu ya mkopo na msaada yenye thamani ya Yen za Japan bilioni 37.9 sawa na takriban shilingi bilioni 761.8 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ukarabati wa Bandari ya Kigoma, uboreshaji wa miundombinu ya maji Zanzibar na Ujenzi wa Barabara ya Arusha-Holili.
Mikataba hiyo imesainiwa jijini Dar es Salaam, kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan, Bw. Naofumi Yamamura, kwa naiaba ya Serikali ya Japan.
Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mikataba hiyo, Bw. Tutuba alisema kuwa Mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma utatekelezwa kwa msaada wa Yen za Japan bilioni 2.73 sawa na takriban shilingi bilioni 54.79, ukihusisha Ukarabati wa gati za mashariki na kaskazini mwa Bandari ya Kigoma, ukarabati wa majengo ya kushushia abiria na mizigo, ukarabati wa barabara zilizopo katika Bandari hiyo na ujenzi wa majengo mapya ya abiria na mizigo.
“Bandari ya Kigoma ilijengwa katika kipindi cha mwaka 1912–1927 na imekuwa bandari muhimu katika kusafirisha mizigo na abiria kwenda nchi jirani za Burundi, DR Congo, Zambia na mikoa iliyopakana na Kigoma, hivyo kukamilika kwa utekelezaji wa mradi huo kutachangia kuongeza ufanisi wa Bandari, kutoa fursa za ajira, kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kuchochea shughuli za kiuchumi na kuchochea biashara kati ya Tanzania na nchi hizo jirani” alisema Bw. Tutuba
Alisema kuwa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji Zanzibar, utatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Yen za Japan bilioni 10.86 sawa na takriban shilingi bilioni 218.382 ambapo mradi huo utahusisha kujenga na kukarabati miundombinu ya maji Mjini Zanzibar.
Kawaulize JaicaHii hatari, mbona Zanzibar wamechukua mgao mkubwa hivyo?
Kuna kitu mtaacha kupinga?Mama anaupiga mwingi. Mpaka miaka minne iishe, Zanzibar itakuwa mbali sana kimaendeleo na madeni tutaachiwa kulipa Wadanganyika. Ndiyo maana ACT Zanzibar wametulia. Mdanganyika amka!
Wewe hata uuchukie haikusaidii,walioweka wanaupenda..Nauchukia sana mfumo wa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar sema tu ndo hivyo nautafutia mkakati wa kuuvunja kwa amani ili haki ya Watanganyika irudi tena
Safi Sana mbona miaka yote mlikuwa mnawanyonya Wazenji na hamkuwasikiliza?Watanganyika Tunanyonywa ,
Ndio maana nomewajibu hapo, Zanzibar wali file Project Japan as so kwa Bara na wao projects yao imepita,kwa hiyo huu ni Mgao au?Sisi Watanganyika Elimu zetu hazijatusaidia kabisa. Tunapenda kupotosha mambo for unnecessary. Kuna tofauti Kati ya mgawo fedha kwa Zanzibar na utekelezaji wa mradi wa Serikali ya Muungano ndani ya Zanzibar. Pesa zimeombwa kea specific projects na moja Kati ya projects hizo ni hiyo ya maji Zanzibar. Kuna shida gani kwa serikali ya Muungano kutekeleza mradi wa maji Zanzibar? Mbona kule Arusha umetekelezwa mradi wa Bilioni 500+? Mbona JPM alitekeleza mradi wa shule za kisasa kila Wilaya Zanzibar na Pemba?
Hapa mumewapa bei gani?Haiwezekan wapewe kiasi chote hicho, watu wenyewe wavivu kupindukia
Huu utoto na upotoshaji unakusaidia nini?Bajeti ya zanzibar ni 450b kwa mwaka nadhani.Tangu aingie madarakani SSH nadhani zanzibar imepokea zaidi ya hiyo hela naona kazi inaendelea vizuri
Waulize JaicaMbona mgao unaoenda Zanzibar ni kubwa sana ukilinganisha na Tanzania Bara. Ukubwa wa Zanzibar ni kama Mkoa wa Lindi lakini mgawo waliopewa ni 218 billioni kati ya zaidi ya billioni 700. Hapana mgawo huo ni mkubwa sana.
Ni ukweli wewe miaka yote 6 ya Mwendazake uliwahi sikia kuna pesa imeenda Zanzibar? Hata zile za Halali kisheria hazikwenda.Nasikia zilikua zinatumika huku tu mara karibu zote
Huu ni upotoshaji,kuna sheria yoyote Serikali ya SSH imevunjwa?SSH anajua anachofanya. Hata kama hamtamchagua 2025, ndoto za KUIENDELEZA nchi yake Zanzibar ALIKOZALIWA itakuwa imetimia. Na huko atakuwa shujaa mkubwa. Sisi kwa kuwa tumekubali acha mama ajenge nyumbani. East or West HOME is BEST!
Kuna sheria na kanuni za Muungano zimekiukwa?Kuna SMZ yenye wizara ya maji na hilo si moja ya mambo ya muungano
Pili, Zanzibar walipewa uwezo wa kukopa nje, wafanye hivyo kwa kupitia SMZ
Aliyeongoza harakati hizo ni AG Maosud ambaye ni VP sasa na wenzake wa CUF.
Tatu, kama ni pesa za JMT zinagawanywa , Zanzibar wanachangiaje kurudisha deni hilo?
Nne, pesa zinazotolewa ni deni la Tanganyika ambako Arusha ni sehemu yake.
Pesa zinazopelekwa Arusha, Simiyu au Tandahimba zinalipwa na Tanganyika( JMT)
Tano, Simiyu na Njombe ni mikoa michanga sana isiyo na miundombinu ikiwemo maji. Mikoa ina maeneo makubwa na idadi kubwa kuliko Zanzibar.
Simiyu na Njombe zinaonekana katika kuchangia pato la Tanzania kule BoT.
Kwanini robo ya mkopo wa Tanzania iende Zanzibar kwa watu 1.2M ambao nusu wanaishi bara? Ni hesabu gani zinatumika au vigezo gani vinatumika
Sita, kwa miezi michache mikopo ya JMT kwa Zanzibar ambayo ni zaidi ya Bilioni 500. Watanganyika wanajiuliza, Zanzibar haikuweza kulipa 60B Tanesco, watawezaje 500B?
Saba, ni kiasi gani na kwa hesabu au mchanganuo gani Zanzibar inalipia madeni ya Taifa?
Kwanini kuna migao hatuonyeshwi wapi Zanzibar wanalipa na kuwajibika katika mikopo
Nane, zile kero 11 za muungano zimeishaje ikiwemo misaada, mikopo na madeni?
Nani alisimama kuyaangalia masilahi ya Tanganyika wakati wa kujadili kero hizo
JokaKuu
Na infact Zanzibar kama visiwa vingine ingeshakuwa kama Dubai kitambo Sana ni vile Bara ndio wanaizuia..Machogo msiumie sana. Vunjeni tuu huo mnaouita muungano tubaki tuu kama nchi jirani. Zanzibar huru itaendelea tuu. Wazanzibari waliosambaa dunia nzima watarudi nyumbani kuijenga. Hata kuungana na Oman inawezekana maana kihistoria Zanzibar ilikuwa ni Oman. Nyie machogo kaeni na ubaguzi wenu, ukabila wenu, ukanda wenu na udini wenu huko bara.
Kwani ukivunjwa ndio itaongeza Kasi ya maendeleo bara? 😁😁Huu muungano hauna faida yoyote zaidi tanganyika inachafuka jina kama imekiteka kisiwa kile.huu muungani ungerekebishwa tu.
Sawa sisi no ndugu tuache tushirikiane kama majirani tu tusiwe na mipaka ya ushirikiano kwa wananchi ila kila nchi ijiendeshe kea kujitegemea
Ila kimbembe kitakuwa kwa hawa jamaa zetu.hawatopenda kumuoma m bara kule hata akiuza duka roho zinawauma hatari
Labda mbara aende kuwa kibarua wa kulima ndo kidoogo watamwachia aisshi huklo