Sisi Watanganyika Elimu zetu hazijatusaidia kabisa. Tunapenda kupotosha mambo for unnecessary. Kuna tofauti Kati ya mgawo fedha kwa Zanzibar na utekelezaji wa mradi wa Serikali ya Muungano ndani ya Zanzibar. Pesa zimeombwa kea specific projects na moja Kati ya projects hizo ni hiyo ya maji Zanzibar. Kuna shida gani kwa serikali ya Muungano kutekeleza mradi wa maji Zanzibar? Mbona kule Arusha umetekelezwa mradi wa Bilioni 500+? Mbona JPM alitekeleza mradi wa shule za kisasa kila Wilaya Zanzibar na Pemba?
Kuna SMZ yenye wizara ya maji na hilo si moja ya mambo ya muungano
Pili, Zanzibar walipewa uwezo wa kukopa nje, wafanye hivyo kwa kupitia SMZ
Aliyeongoza harakati hizo ni AG Maosud ambaye ni VP sasa na wenzake wa CUF.
Tatu, kama ni pesa za JMT zinagawanywa , Zanzibar wanachangiaje kurudisha deni hilo?
Nne, pesa zinazotolewa ni deni la Tanganyika ambako Arusha ni sehemu yake.
Pesa zinazopelekwa Arusha, Simiyu au Tandahimba zinalipwa na Tanganyika( JMT)
Tano, Simiyu na Njombe ni mikoa michanga sana isiyo na miundombinu ikiwemo maji. Mikoa ina maeneo makubwa na idadi kubwa kuliko Zanzibar.
Simiyu na Njombe zinaonekana katika kuchangia pato la Tanzania kule BoT.
Kwanini robo ya mkopo wa Tanzania iende Zanzibar kwa watu 1.2M ambao nusu wanaishi bara? Ni hesabu gani zinatumika au vigezo gani vinatumika
Sita, kwa miezi michache mikopo ya JMT kwa Zanzibar ambayo ni zaidi ya Bilioni 500. Watanganyika wanajiuliza, Zanzibar haikuweza kulipa 60B Tanesco, watawezaje 500B?
Saba, ni kiasi gani na kwa hesabu au mchanganuo gani Zanzibar inalipia madeni ya Taifa?
Kwanini kuna migao hatuonyeshwi wapi Zanzibar wanalipa na kuwajibika katika mikopo
Nane, zile kero 11 za muungano zimeishaje ikiwemo misaada, mikopo na madeni?
Nani alisimama kuyaangalia masilahi ya Tanganyika wakati wa kujadili kero hizo
JokaKuu