Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Serikali ya Japan imeipatia Tanzania mkopo wa shillingi billion 761.8 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo nchini!

Katika mkopo huo kisiwa cha Zanziba kimepewa mgao wa Tsh billion 218+


Kazi iendelee....View attachment 2107913
View attachment 2107914
SSH anajua anachofanya. Hata kama hamtamchagua 2025, ndoto za KUIENDELEZA nchi yake Zanzibar ALIKOZALIWA itakuwa imetimia. Na huko atakuwa shujaa mkubwa. Sisi kwa kuwa tumekubali acha mama ajenge nyumbani. East or West HOME is BEST!
 
ILA NACHOJUA DENI LITALIPWA NA HAOHAO WALIOKOPA!!

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Deni wanalipa serikali ya muungano na sio zanzibar yaani sisi watanganyika ni malofa wa kiwango cha juu sana watu milioni 1 wanapata pesa nyingi kiasi hicho. Watanganyima tuamkeni jamani kwa mwendo huu samia mpaka atoke madarakani zanzibar itakuwa kama singapore.
 
Huu ni ukiukaji mkubwa wa articles of union ambazo zinataka Zanzibar kupewa 4.5%
Ushawahi kuona articles of Union Iliyoandikwa ?
au unasema tu
Tulia wewe hapa ziliungana
two sovereignty states sio nchi na wilaya au wengi na kidogo.
Mkichoka vunjeni kwa Amani na utulivu
 
Pia ule mradi wa maji victoria kuleta shy tabora dodoma,
Shida watu wa bara tuna roho za kwanini sana,,, [emoji23][emoji23] yaani hatuna ustaarabu kabisa wala hikima, tumekaa kaa kama watindiga fulani,,,
Wakati tunavuta maji toka lake victoria , wazanzibar hawakulalamika,,, wao pia wanalipa kodi, [emoji851][emoji851]
Huu ni mkopo,naomba kujua kama Zanzibar watarudisha mkopo Huo au jukumu Zima litabebwa na Tanganyika chini ya mwamvuli wa JMT!
 
Deni wanalipa serikali ya muungano na sio zanzibar yaani sisi watanganyika ni malofa wa kiwango cha juu sana watu milioni 1 wanapata pesa nyingi kiasi hicho. Watanganyima tuamkeni jamani kwa mwendo huu samia mpaka atoke madarakani zanzibar itakuwa kama singapore.
Mi-5 tena 🙄
 
Tanzania na Zanzibar hapa sijaelewa kabisa
 
Upuuzi huu si w kuuchekea.watanganyika tunadilikeni.hapa linaongewa kimatani lakini mbeleni hawa jamaa na wanavyoipenda nchi yao!watalivua hili koti watuache na madeni kw watoto zetu.na wanao sema wakimbilie huko.wala hawatotambulika ni sawa na kwenda israel kuhiji na kurudi kwenu unawaachia kila kitu chao .wao wakija huku wanaondoka na vya kwetu
Hawa jamaa wabaguzi balaa
 
Kama kawaida, kila Raisi anakuja na mapuuza yake.
 
Hicho kizanzibar ambacho ukubwa wake ni sawa na mikoa3 ya Tz bara, why kila siku kinapokea misaada mikubwa lkn hakibadiriki?

Yaani miundombinu yao ya hovyo, huduma za kijamii hovyo, mipango miji hovyo, sas hizo pesa wanapelekaga wapi?

Hiyo zanzibar ilitosha kwa kuiwekewa robo bajeti ya Tz bara nakuifanya Zanzibar kuwa kama London [emoji23][emoji23][emoji23] au natania ndugu zangu???

Ukwel mchungu, bado kuna matumiz mabovu ya fedha na mikopo.

Mpka leo bado wanahangaika na miradi ya maji??
Nonsense
 
Sawa tu, JPM alikuwa anakomba mboga ya taifa anapeleka chato
Bora yeye kuliko kupeleka kwa watu ambao wataitaji nchi yao.na wametulia sasa kwani wanavuna.litakapo baki jangwa ndio tutajua mbivu na mbichi
 
Kwani huu Muungano sisi tunaung'ang'ania una faida gani na sisi, kidhati kabisa mie sioni faida kwetu kwenye huu muungano, halafu kibaya zaidi ni sisi ndio tunafosi, wazanzibar wakitaka nchi yao inakuwa msala.
Huu muungano hauna faida yoyote zaidi tanganyika inachafuka jina kama imekiteka kisiwa kile.huu muungani ungerekebishwa tu.
Sawa sisi no ndugu tuache tushirikiane kama majirani tu tusiwe na mipaka ya ushirikiano kwa wananchi ila kila nchi ijiendeshe kea kujitegemea
Ila kimbembe kitakuwa kwa hawa jamaa zetu.hawatopenda kumuoma m bara kule hata akiuza duka roho zinawauma hatari
Labda mbara aende kuwa kibarua wa kulima ndo kidoogo watamwachia aisshi huklo
 
Machogo msiumie sana. Vunjeni tuu huo mnaouita muungano tubaki tuu kama nchi jirani. Zanzibar huru itaendelea tuu. Wazanzibari waliosambaa dunia nzima watarudi nyumbani kuijenga. Hata kuungana na Oman inawezekana maana kihistoria Zanzibar ilikuwa ni Oman. Nyie machogo kaeni na ubaguzi wenu, ukabila wenu, ukanda wenu na udini wenu huko bara.
 
Sisi Watanganyika Elimu zetu hazijatusaidia kabisa. Tunapenda kupotosha mambo for unnecessary. Kuna tofauti Kati ya mgawo fedha kwa Zanzibar na utekelezaji wa mradi wa Serikali ya Muungano ndani ya Zanzibar. Pesa zimeombwa kea specific projects na moja Kati ya projects hizo ni hiyo ya maji Zanzibar. Kuna shida gani kwa serikali ya Muungano kutekeleza mradi wa maji Zanzibar? Mbona kule Arusha umetekelezwa mradi wa Bilioni 500+? Mbona JPM alitekeleza mradi wa shule za kisasa kila Wilaya Zanzibar na Pemba?
Kuna SMZ yenye wizara ya maji na hilo si moja ya mambo ya muungano

Pili, Zanzibar walipewa uwezo wa kukopa nje, wafanye hivyo kwa kupitia SMZ
Aliyeongoza harakati hizo ni AG Maosud ambaye ni VP sasa na wenzake wa CUF.

Tatu, kama ni pesa za JMT zinagawanywa , Zanzibar wanachangiaje kurudisha deni hilo?

Nne, pesa zinazotolewa ni deni la Tanganyika ambako Arusha ni sehemu yake.
Pesa zinazopelekwa Arusha, Simiyu au Tandahimba zinalipwa na Tanganyika( JMT)

Tano, Simiyu na Njombe ni mikoa michanga sana isiyo na miundombinu ikiwemo maji. Mikoa ina maeneo makubwa na idadi kubwa kuliko Zanzibar.

Simiyu na Njombe zinaonekana katika kuchangia pato la Tanzania kule BoT.
Kwanini robo ya mkopo wa Tanzania iende Zanzibar kwa watu 1.2M ambao nusu wanaishi bara? Ni hesabu gani zinatumika au vigezo gani vinatumika

Sita, kwa miezi michache mikopo ya JMT kwa Zanzibar ambayo ni zaidi ya Bilioni 500. Watanganyika wanajiuliza, Zanzibar haikuweza kulipa 60B Tanesco, watawezaje 500B?

Saba, ni kiasi gani na kwa hesabu au mchanganuo gani Zanzibar inalipia madeni ya Taifa?
Kwanini kuna migao hatuonyeshwi wapi Zanzibar wanalipa na kuwajibika katika mikopo

Nane, zile kero 11 za muungano zimeishaje ikiwemo misaada, mikopo na madeni?
Nani alisimama kuyaangalia masilahi ya Tanganyika wakati wa kujadili kero hizo

JokaKuu
 
Back
Top Bottom