Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218

Na infact Zanzibar kama visiwa vingine ingeshakuwa kama Dubai kitambo Sana ni vile Bara ndio wanaizuia..

Visiwa Maskini hapa Duniani ni Zanzibar na Commoros ila wakikaa peke yao Utalii wote ni Zanzibar.
Kwahiyo Madagascar na Comoro na wao wamekuwa Kama Dubai [emoji3][emoji3]

Wazanzibar nasemaga hamna akili
 
Haya ndo mambo ambayo Hangaya kayafanyia kazi! a.k.a kero za muungano yaani Tanzania bara inapata billion 540 na zanzibar wanapata karibia billion 220 huu ni upuuzi wa hali ya juu! Watanganyika mnachekelea tu!
Musilalamike kwani zamani mukizisomba zote zote kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano.
 
Nguruvi3 , kwanza lazma tukubaliane kuwa Muungano huu una viini macho flani. Una viini macho kwasababu, in reality Muungano ni kama ulikuwepo kabla ya tarehe 26 April 1964. Hili jambo wengi wetu Wabara kwa wazanzibari ni kama wanalipuuzia au kutolipa umuhimu. Kama Ikulu yetu ya Dar es salam ilijengwa na mzanzibari kama eneo la kiutawala la Zanzibar, kuamini Muungano ulianzia 1964 huo ni uvivu wa kufikiri. Kwa msingi huo hicho kinachoitwa mambo ya Zanzibar na mambo ya Tanganyika au ya Muungano ni kiini macho kwani in fact havipo. Ni sehemu ya viini macho vya Muungano. Zanzibar hana jambo lolote analoshughulika nalo yeye kama "nchi". Take it from me hana. Ndio maana no wonder huyohuyo mzanzibari anakuwa Waziri wa Maji huku wewe ukisema maji si suala la Muungano.

Usitishike na majina kama Rais, Waziri, sjui ardhi ya Zanzibar watu wa Bara hawaruhusiwi. Hayo ni maneno tu lakini Zanzibar kuna Wabara kibao wamenunua na kumiliki ardhi na mashamba kila kona na bila wasiwasi wowote. Kama ilivyo wapemba wakiwa Bara na watu wa Bara kuinjoy na kuwafanyia dhihaka lafudhi yao au kuwaita mdebwedo ndivyo hivyohivyo wapemba wanavyoinjoy na kuwafanyia dhihaka watu wa Bara kwa kuwaona hawajui kuongea vizuri au kuwaita machogo.

Turudi kwenye point. Mimi sijawahi kusikia nchi au taasisi ya Fedha ya kimataifa ikiikopesha Zanzibar huku ikijua kwamba hakuna nchi iitwayo Zanzibar. Zaidi nchi au taasisi hizo kuikopesha nchi ya Tanzania na huenda sehemu ya mkopo huo kutekeleza mradi ndani ya Zanzibar. Mimi ni mtanganyika lakini sioni shida kwenye hilo. Kama tumekubaliana Mzanzibari anaweza kuwa Amirijeshi Mkuu na ku dictate bajeti ya nchi ya matrilion itumike vipi, ujinga kuhoji Zanzibar kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 200.

Hili suala la population na geographical size ya Zanzibar, halina maana yoyote kwasababu if it is, then hata Bara projects ingekuwa zitekelezwe kwa misingi hiyo. Hatahivyo, kama tukiamini kuwa Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili, na kama hizo nchi zilikuwa na mamlaka kamili, the right ratio ni 50:50; no matter how large or population size. Mkilichukua jambo hilo na kulipeleka mahakama yoyote duniani, wazanzibari wanahaki ya kupata 50 yao. Yes, tulijua kama wao ni nchi ndogo wakati tunaungana.

Hili la mchango wa Zanzibar kwenye kulipa Deni au pato la Taifa pia halina mashiko. Ndio maana serikali inakusanya kodi kubwa zaidi Dar es Salaam lakini kodi hiyo hutawanywa hadi Sumbawanga wanakochangia kidogo. Ndivyo nchi inavyoongozwa.
Umeharisha
 
Mie naona Tanganyika ndio imechukua mgao mkubwa, zilitakiwa zigawiwe sawa kwa sawa. Ni Muungano wa nchi mbili.
Issue iko kwenye kulipa deni, Tanganyika na Zanzibar hawalipi sawa hata kama mgawo wa mkopo ungekuwa sawa sawa. Haki ya kukopa inapaswa iende sambamba na wajibu wa kulipa. Mchango wa Zanzibar kwenye pato la taifa hauzidi 5% hivyo Zanzibar tutalipa sio zaidi ya 5% tu ya mkopo mzima (lakini tumepewa zaidi ya 29% ya mkopo wote), wakati watanganyika watawajibika kulipa zaidi 95% ya mkopo wote.

Watanganyika amkeni sasa, mama anawatapeli kila siku.
 
Kwa mujibu wa gavana wa BoT marehemu Ndulu , Zanzibar haichangii katika muungano.
Kwa taarifa za TRA pesa hubaki Zanzibar, kama zinaletwa Dar twambie ni kiasi gani.

Zanzibar hawana mchango katika muungano nani analipia gharama za muungano zikiwemo Wizara na Taasisi? Jibu ni rahisi, Tanganyika ndiyo inagharamia Muungano

Tanganyika imebaki JMT kwasababu Zanzibar ina kila kitu chake.
Zanzibar kuitumia JMT katika mafao tu, kuwajibika hawapo

Hiki ndicho kiini cha kuhoji, mikopo inalipwaje? Zanzibar wakichukua bilini 280 wanarudisha kwa utaratibu gani? Hakuna formula, deni ni la JMT ambalo ni Tanganyika, na inalipa

SMZ ilishindwa kulipa Tanesco Bilioni 60! Matokeo yake deni hilo likarudishwa kwa Wananchi wa Tanganyika na bila kujali ni CCM, Chadema,ACT au TLP wamelipa

Hakuna Wilaya , Tarafa, kata au kijiji cha Tanganyika kinacholipiwa umeme na JMT, iweje nchi ya Zanzibar ikiwa na kila kitu ilipiwe umeme !
Namuomba mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Siluhu Hassan awafikirie na kuwaangalia kwa jicho la huruma walimu wetu hasa wa shule za msingi. Nimegundua wanakazi ngumu sana tena sana kwa kweli.
Hapa naelimisha watu na madigirii yao lakini wapi.

Watu tunashindwa kuitofautisha Tanganyika na Tanzania halafu watu walivaa joho na mambwembwe kibao.

Hiyo habari ya umeme hawakushindwa kulipa isipokuwa walikuwa hawakubaliani na elements za VAT kwenye kuuziana umeme.
Na hoja ni kwamba final consumer yuko upande wa Pili kwanini walikuwa hawataki kuconsider input tax inayolipwa wakati wa mauziano au kama wanatreat as export kutokana na kila upande una Sheria zake za VAT basi hiyo ni Zero rated supply

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Haya ndo mambo ambayo Hangaya kayafanyia kazi! a.k.a kero za muungano yaani Tanzania bara inapata billion 540 na zanzibar wanapata karibia billion 220 huu ni upuuzi wa hali ya juu! Watanganyika mnachekelea tu!

Purely childish, something must be done sooner than later
 
Yanahudumiwa na Tanganyika kwa sababu mambo yote ya Tanganyika yamewekwa kwenye serikali ya muungano!! Hapo ndipo kiini macho kilipo!! Hata bajeti ya kujenga choo cha ofisi ya kata ni suala la muungano!! Hii ni kwa sababu hakuna serikali ya Tanganyika!!
Tanganyika haina kipato cha kuhudumia hayo mambo yaliyotajwa, kama unayafahamu hayo mapato ni vyema tukashea hapa.
Maana ni kweli hakuna Serikali ya Tanganyika lakini mapato ya Tanganyika yapo ambayo ni yale yote yasio ya Muungano.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Watu tunashindwa kuitofautisha Tanganyika na Tanzania halafu watu walivaa joho na mambwembwe kibao.
Tanganyika kwasasa ni JMT. Zanzibar ina serikali yake na taasisi zake nje ya zile za muungano
Ukiona Zanzibar inakumbatia JMT ujue kuna masilahi. Hutawasikia wakizungumzia Wizara ya Ulinzi, mambo ya ndani, mambo ya nje, Wizara na taasisi za muungano.
Kwa mantiki yoyote JMT imebaki kuwa Tanganyika na Rasimu ya Warioba ililiona jambo hilo
Hiyo habari ya umeme hawakushindwa kulipa isipokuwa walikuwa hawakubaliani na elements za VAT kwenye kuuziana umeme.
Na hoja ni kwamba final consumer yuko upande wa Pili kwanini walikuwa hawataki kuconsider input tax inayolipwa wakati wa mauziano au kama wanatreat as export kutokana na kila upande una Sheria zake za VAT basi hiyo ni Zero rated supply
Hata baada ya kuondolewa VAT Zanzibar haikulipa deni hilo , ''ilisamehewa '' kwa lugha ya JPM
Kusamehewa kuliingizwa katika JMT ambayo ni Tanganyika kwa uendeshaji na gharama.
Deni la Umeme uliotumika Zanzibar lililipwa na Watanganyika

Hakuna kijiji , kata au tarafa iliyowahi kusamehewa umeme Tanganyika

Ni kwa mantiki hiyo, hii mikopo italipwa na JMT na mzigo kuwa wa Mtanganyika.

Ikiwa tuna formula ya kugawana mbona hatuonyeshwi formula ya kulipia deni?
 
Mama anaupiga mwingi. Mpaka miaka minne iishe, Zanzibar itakuwa mbali sana kimaendeleo na madeni tutaachiwa kulipa Wadanganyika. Ndiyo maana ACT Zanzibar wametulia. Mdanganyika amka!
Tuliteseka sana ndani ya miaka mitano ya Magufuli.

Bora mama anaupiga mwingi na anafungua nchi.

Nchi yenyewe inayofunguliwa kumbe ni Zanzibar!!

Sisi wa chato tuendelee kufuga kupe [emoji1787]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Idadi yao ni kama 4% tu ya watu wote, lakini wanajipa zaidi ya 28% ya pesa yote.

Na deni litalipwa na Tanganyika. Yaani hadi kufika 2025 wana wadanganyika mtaidai wenyewe serikali yenu ya Tanganyika.
Tuacheni kulalamika.

Magufuli alipokuwa anajenga bara mlimuona mjinga.

Nadhani tutaelewana kwa sasa!!

Na ole wenu mkanyage Zenji kimasihara sijui kuwekeza tutawa Zenji [emoji1787]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Tanganyika kwasasa ni JMT. Zanzibar ina serikali yake na taasisi zake nje ya zile za muungano
Ukiona Zanzibar inakumbatia JMT ujue kuna masilahi. Hutawasikia wakizungumzia Wizara ya Ulinzi, mambo ya ndani, mambo ya nje, Wizara na taasisi za muungano.
Kwa mantiki yoyote JMT imebaki kuwa Tanganyika na Rasimu ya Warioba ililiona jambo hilo

Hata baada ya kuondolewa VAT Zanzibar haikulipa deni hilo , ''ilisamehewa '' kwa lugha ya JPM
Kusamehewa kuliingizwa katika JMT ambayo ni Tanganyika kwa uendeshaji na gharama.
Deni la Umeme uliotumika Zanzibar lililipwa na Watanganyika

Hakuna kijiji , kata au tarafa iliyowahi kusamehewa umeme Tanganyika

Ni kwa mantiki hiyo, hii mikopo italipwa na JMT na mzigo kuwa wa Mtanganyika.

Ikiwa tuna formula ya kugawana mbona hatuonyeshwi formula ya kulipia deni?
Uuuuwwi.

Mwalimu hupenda asiache nyuma mwanafunzi hata mmoja kwenye darasa lake. Ikitokea wengine wako nyuma atafanya extra effort kuwapa special care kuhakikisha wote wapo ndani ya boti moja.
Ilisiposaidia hii mwisho huamua kuwa dump.
Na mimi nishafanya hayo kilichobaki ni kubwaga manyanga, sina tena jinsi. Maana sielewi kwamba huelewii au unafanya makusudi?

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Sote ni watanzania hebu tuacheni ubinafsi akipewa Zanzibar amepewa Tanzania akipewa tanganyika amepewa Tanzania. Tusipende kulalamaaa hovyo
 
Zanzibar haichangii chochote kwenye gharama za kuendesha muungano ambazo inatakiwa itoe gharama nusu kama inataka ipate faida zake nusu. Hawatoi hata mia. Wanajiona ni nchi kamili lakini hawataki kuwajibika kama nchi. Inapokuja kwenye Mikopo ya Tanzania wanajiona kama mkoa mmojawapo wa Tanzania. Wanaamini wana haki ya kupata mgao wao kama mikoa mingine, tena wapate zaidi kwa sababu wao ni nchi. Ila kwenye malipo ya deni ilipe tanzania kwa sababu wao ni kama wilaya ya TZ. Hizi ni Tabia za kimalaya kutaka kubebwa na kuhudumiwa na mwanaume wewe kazi yako ni kulalamika tu. Hata malaya kuna namna hulipia huduma hizo.
Bring back our Tanganyika!
 
Issue iko kwenye kulipa deni, Tanganyika na Zanzibar hawalipi sawa hata kama mgawo wa mkopo ungekuwa sawa sawa. Haki ya kukopa inapaswa iende sambamba na wajibu wa kulipa. Mchango wa Zanzibar kwenye pato la taifa hauzidi 5% hivyo Zanzibar tutalipa sio zaidi ya 5% tu ya mkopo mzima (lakini tumepewa zaidi ya 29% ya mkopo wote), wakati watanganyika watawajibika kulipa zaidi 95% ya mkopo wote.

Watanganyika amkeni sasa, mama anawatapeli kila siku.
Mkopo unalipwa na Tanzania, sio Zanzibar wala Tanganyika.
 
Zanzibar haichangii chochote kwenye gharama za kuendesha muungano ambazo inatakiwa itoe gharama nusu kama inataka ipate faida zake nusu. Hawatoi hata mia. Wanajiona ni nchi kamili lakini hawataki kuwajibika kama nchi. Inapokuja kwenye Mikopo ya Tanzania wanajiona kama mkoa mmojawapo wa Tanzania. Wanaamini wana haki ya kupata mgao wao kama mikoa mingine, tena wapate zaidi kwa sababu wao ni nchi. Ila kwenye malipo ya deni ilipe tanzania kwa sababu wao ni kama wilaya ya TZ. Hizi ni Tabia za kimalaya kutaka kubebwa na kuhudumiwa na mwanaume wewe kazi yako ni kulalamika tu. Hata malaya kuna namna hulipia huduma hizo.
Bring back our Tanganyika!
Ww mtanganyika unapiga kelele zanini? Deni linalipya na Tanzania nyie endeleeni kuificha Tanganyika yenu, mkoloni uchwara
 
Back
Top Bottom