Nguruvi3 , kwanza lazma tukubaliane kuwa Muungano huu una viini macho flani. Una viini macho kwasababu, in reality Muungano ni kama ulikuwepo kabla ya tarehe 26 April 1964. Hili jambo wengi wetu Wabara kwa wazanzibari ni kama wanalipuuzia au kutolipa umuhimu. Kama Ikulu yetu ya Dar es salam ilijengwa na mzanzibari kama eneo la kiutawala la Zanzibar, kuamini Muungano ulianzia 1964 huo ni uvivu wa kufikiri. Kwa msingi huo hicho kinachoitwa mambo ya Zanzibar na mambo ya Tanganyika au ya Muungano ni kiini macho kwani in fact havipo. Ni sehemu ya viini macho vya Muungano. Zanzibar hana jambo lolote analoshughulika nalo yeye kama "nchi". Take it from me hana. Ndio maana no wonder huyohuyo mzanzibari anakuwa Waziri wa Maji huku wewe ukisema maji si suala la Muungano.
Usitishike na majina kama Rais, Waziri, sjui ardhi ya Zanzibar watu wa Bara hawaruhusiwi. Hayo ni maneno tu lakini Zanzibar kuna Wabara kibao wamenunua na kumiliki ardhi na mashamba kila kona na bila wasiwasi wowote. Kama ilivyo wapemba wakiwa Bara na watu wa Bara kuinjoy na kuwafanyia dhihaka lafudhi yao au kuwaita mdebwedo ndivyo hivyohivyo wapemba wanavyoinjoy na kuwafanyia dhihaka watu wa Bara kwa kuwaona hawajui kuongea vizuri au kuwaita machogo.
Turudi kwenye point. Mimi sijawahi kusikia nchi au taasisi ya Fedha ya kimataifa ikiikopesha Zanzibar huku ikijua kwamba hakuna nchi iitwayo Zanzibar. Zaidi nchi au taasisi hizo kuikopesha nchi ya Tanzania na huenda sehemu ya mkopo huo kutekeleza mradi ndani ya Zanzibar. Mimi ni mtanganyika lakini sioni shida kwenye hilo. Kama tumekubaliana Mzanzibari anaweza kuwa Amirijeshi Mkuu na ku dictate bajeti ya nchi ya matrilion itumike vipi, ujinga kuhoji Zanzibar kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 200.
Hili suala la population na geographical size ya Zanzibar, halina maana yoyote kwasababu if it is, then hata Bara projects ingekuwa zitekelezwe kwa misingi hiyo. Hatahivyo, kama tukiamini kuwa Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili, na kama hizo nchi zilikuwa na mamlaka kamili, the right ratio ni 50:50; no matter how large or population size. Mkilichukua jambo hilo na kulipeleka mahakama yoyote duniani, wazanzibari wanahaki ya kupata 50 yao. Yes, tulijua kama wao ni nchi ndogo wakati tunaungana.
Hili la mchango wa Zanzibar kwenye kulipa Deni au pato la Taifa pia halina mashiko. Ndio maana serikali inakusanya kodi kubwa zaidi Dar es Salaam lakini kodi hiyo hutawanywa hadi Sumbawanga wanakochangia kidogo. Ndivyo nchi inavyoongozwa.