Japan yaitangaza Tanzania kuwa Kitovu cha Uwekezaji, viwanda. Honda kujengwa nchini

Japan yaitangaza Tanzania kuwa Kitovu cha Uwekezaji, viwanda. Honda kujengwa nchini

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,813
10/08/20130
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  • Japan yatangaza sera mpya kwa Tanzania Sasa Tanzania kuwa nchi lengwa ya Japan
  • Japan itasaidia Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji katika Afrika
  • Kushiriki maboresho Reli ya Kati
  • Kusaidia kupanua na kuboresha Bandari ya Dar Es Salaam
  • Viwanda vya Japan kujengwa nchini kikiwemo cha kutengeneza pikipiki za Honda
  • Ni matokeo ya Ziara ya Rais Kikwete Japan
JAPAN imeamua kuanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania ambako nchi hiyo itaifanya Tanzania kuwa nchi lengwa ya Japan na kuiwezesha kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji katika Afrika kwa nia ya kuiwezesha kuwa na uchumi ulioimarika na wenye kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi.

Uamuzi huo wa Japan ni matunda ya mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Shinzo Abe yaliyofanyika Tokyo, Japan wakati Rais Kikwete alipotembelea nchi hiyo Juni, mwaka huu, 2013.

Uamuzi na msimamo mpya wa Japan umetangazwa rasmi leo, Jumamosi, Agosti 10, 2013 na Waziri wa
Uchumi, Biashara na Viwanda wa nchi hiyo, Mheshimiwa Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.

Kwa upande wa Tanzania, mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anashughulika na Uwekezaji na Uwezeshaji Mheshimiwa Mary Nagu, Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe.

Waziri Motegi amemwambia Rais Kikwete kuwa ametumwa na Waziri Mkuu Abe kufuatilia mazungumzo kati yao na kutangaza rasmi kuwa Japan imeiteua Tanzania kuwa nchi lengwa na kitovu cha uwekezaji wa Japan katika Afrika Mashariki na katika Afrika kwa jumla.

Waziri Motegi pia amemwambia Rais Kikwete kuwa pia amekuja Tanzania kutoa taarifa kuwa Japan iko tayari kushiriki katika kuboresha na kuifanya ya kisasa zaidi Reli ya Kati kwa kujenga njia ya kimataifa badala ya njia nyembamba ya sasa. Amesema kuwa Japan itatuma wataalam wake kuangalia jinsi gani ya kuanza kazi hiyo ya uboreshaji wa Reli hiyo.

Aidha, Mheshimiwa Motegi ametangaza kuwa Japan itashiriki katika upanuzi na uboreshaji wa Bandari ya Dar Es Salaam kwa kuifanya ya kisasa zaidi.

Waziri Motegi amesema kuwa katika azma ya Japan ya kuifanya Tanzania nchi ya mfano katika Afrika katika uwekezaji na uchumi ulioimarisha, amekuja na kundi la wafanya biashara wa Japan ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Tanzania kuona jinsi gani wanavyoweza kusaidiana katika kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.

Waziri pia amesema kuwa moja ya malengo ya uamuzi huo wa Japan ni kuhakikisha kuwa bidhaa ambazo kwa sasa zinanunuliwa moja kwa moja kutoka Japan zitazalishwa hapa nchini katika viwanda ambavyo vitajengwa na makampuni ya Japan.

Kwa kuanzia amesema kuwa makampuni mawili ya Honda na Panasonic yamekubali kujenga viwanda nchini kimoja kwa ajili ya kutengeneza pikipiki za Honda hapa hapa nchini na kingine kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya umeme.

"Huu ni mwanzo tu Mheshimiwa Rais kwa sababu kama nilivyosema kuwa tunataka Tanzania kuwa nchi mfano ya uwekezaji wa Japan katika eneo hili la dunia na namna hiyo kwa pamoja tutakuwa tumeshirikiana katika kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania," Mheshimiwa Motegi amemwambia Rais Kikwete.

Waziri huyo pia amesema kuwa baadhi ya makampuni ya Japan yana mipango ya kuwekeza katika kilimo, na hasa kilimo cha pamba, na kuanzisha viwanda vya nguo hapa hapa nchini.

Wakati wa mazungumzo yao mjini Tokyo, Rais Kikwete alimtaka Waziri Mkuu Abe kuwekeza zaidi katika Afrika akisisitiza kuwa Japan ni moja ya mataifa makubwa duniani ambayo yamefanikiwa kupata soko kubwa katika Afrika na hasa soko la magari.

Uamuzi huo wa Japan na ziara ya Mheshimiwa Motegi inakuja wiki na miezi michache baada ya Tanzania kuwa imepokea viongozi wa mataifa mengi yakiwemo mataifa makubwa ya Marekani na China na inathibitisha ni kiasi gani siasa na sera za Tanzania zinavyokubalika duniani.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

10 Agosti, 2013
 
Haka kanchi ketu kanautajiri mkubwa sana, hazina zimefulika madin aridhin, gesi pia misitu minene yenye wanyama wakila aina.

Haka kanchi ketu nikakimasikini sana kanafaa kuwa soko zuri kwa bidhaa za walioendelea kama japan, china nk

Naona amani yetu ipo mashakani .......... kila jomba wa ng'ambo anatulenga sisi tu mwee, kikwete naye na 10% anapokea

kila kitu kama scavenger wallah were in trouble for sure.
 
Namuonea huruma huyo waziri wa Japan kwa kushindwa kuelewa kuwa Kikwete ndio chanzo cha haya matatizo anayotaka kutatua...

Anaongelea kuboresha reli wakati mtoto wa Kikwete aitwaye Riziwani ndio kinara wa biashara ya usafirishaji mizigo kwa malori. Ubovu wa reli Ni mpango mkakati wa Kikwete kumtakatisha mwanaye na biashara ya malori ambayo pia mawaziri wengi pamoja na wahindi na waarabu rafiki zake Kikwete wanahusika.

Ukija kwenye upanuzi wa bandari mjapani hajaambiwa kuwa mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na wachina umekataza upanuzi wowote wa bandari ya Dar. Ngoja mjapani aje kikazi zaidi ndio atamjua Kikwete.

Labda atusaidie kupambana na biashara ya madawa ya kulevya...
 
[#hongera sana god bless tanzania] tuwe wazalendo ktk mambo nyeti yanayolenga kunyanyua taifa letu / not blah blah
 
Tunawakaribisha kwa moyo mmoja maendeleo kwanza mengine baadaye.
 
Good Move, Hawa super Giant wa Dunia wote wanaigombania Tanzania kama mpira wa kona, hofu yangu ni sera mbovu za CCM ikichagizwa na mifumo yao mibovu isiyokuwa ya uwazi utakavyoendelea kuididimiza nchi yetu... Wageni waje weenyeji waumie sasa iwe mwisho jamani...
Wao wanatuhitaji kuliko sisi tunavyowahitaji sijui kwanini haiwaingii akilini hawa mbulula wa CCM...Tukiweka kila kitu kwa uwazi Tanzania inaweza kuendelea ndani ya miaka mitano tu na si hizi takwimu za akina Ndulu za uchumi kukua kwa 1% wakati tuna kila kitu na vingine tumepewa sisi tu kama zawadi kutoka kwa mwenyeezi mungu...
 
Japan ni nchi iliyokua sana na imara kiuchumi na kidemocrasia.Sio vibaya kutusaidia lakin nafikiri hatujajianda kusaidiwa... Huo ujumbe ni sawa na kusema Tanzania ni koloni la kijapani kwanzia sasa.Acheni tripu zenu za kila siku......
 
...wamechelewa sana kugundua shamba la bibi...
 
Bila shaka hicho kiwanda kitajengwa Dar es salaam! Hahahaaaaaa, nchi hii bwana!
 
Sipendi kusikia neno "matokeo ya zaira ya Kikwete Japan" huo mpango umeletwa kutokana na ugunduzi wa gas uko Mtwara. Nchi za magharibi wameshaona deal lipo Tanganyika, ndio maana kila siku wanapigana vikumbo. JK na CCM yake have none to do with this at all
 
Karibu sana Wajapani, Tanzania ni nchi ya amani, tushirikiane kwa faida ya wote.
TANZANIA MBELE, AFRIKA MASHARIKI INAFUATA.
 
Upuuzi mtupu Ikulu ya nchi kushangilia misaada... Hivi ni lini na sisi tutaanza kujitegemea? Kila kukicha tunasaidiwa tu, hao wanaotusaidia wana huruma sana au ?
 
Upuuzi mtupu Ikulu ya nchi kushangilia misaada... Hivi ni lini na sisi tutaanza kujitegemea? Kila kukicha tunasaidiwa tu, hao wanaotusaidia wana huruma sana au ?

Cha kushangaza habari imekaa kishabiki utadhabi hao wajepu wanakuja kuggawa zawadi. Hawa maCCM kamwe hawawezi kuleta maendeleo, nillitegemea hao jamaa kuonekana kama partners WA kibiashara ambapo wote tutanufaika but hapa inaonekana na Ni msaada. Ikumbukwe pia serikali ya Japan haijengi viwanda bali Ni makampuni ya kijapani, kinachotakiwa Ni kiwekwa mazingira bora ya uwekezaji ili kampuni kutoka sio Tu Japan hata Korea, Kenya,Saudia, Finland ikija inayakuta na kuwekeza kwa manufaa ya wote
 
Back
Top Bottom