Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" kuhusu jambo lolote lenye maslahi makubwa kwa taifa letu liwe ni la kisiasa, kiuchumi au kijamii.
Mada ya leo ni kuhusu makubaliano ya kiserikali, IGA ambapo Bunge letu tukufu, limeridhia kitutusa kwa kura ya gulio ya "ndiyo...!", makubaliano hayo ya IGA kati ya Serikali yetu na kampuni ya DPW ya Mwarabu wa Dubai, kutuendeshea Bandari zetu, naomba kuwapooza moyo na kuwafariji wana maslahi ya kweli ya taifa, kuwa hata baada ya kuridhiwa na yale matutusa ya Bunge letu, ikithibitika pasipo shaka kuwa kuna mambo bado hayajakaa sawa, makubaliano hayo yanarekebishwa kabla ya kuingia mkataba wa HGA na serikali yetu, hivyo Tanzania kufaidika na mwekezaji kufaidika kwa kufikia a win win situation, ili kazi nzuri ya Mama Samia iendelee bila madoadoa!.
Kupitisha kitutusa maana yake ni unapewa lidude, ndani yake kuna mambo ya ajabu yanayokwenda kinyume cha sheria zetu, halafu wewe unalipitisha lidude hilo vile vile lilivyo bila any reservations.
Hitimisho
Kwa vile Rais Samia ana nia njema ya dhati kuisaidia nchi yetu, wasaidizi wa rais na sisi Watanzania wengine wote tuna wajibu wa kumsaidia rais wetu na kulisaidia taifa letu na huu ndio uzalendo wa kweli.
Paskali.