Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Kwahawa wabongo wapenda pesa hata majopo yangekua mia wangelambishwa asali namwisho wangepitisha hatakama wameona madudu
 
Binafsi napenda sana kusoma mambo unayoandikaga. Wewe bwana Paschal una akili sana. Waafrika umaskini umetufanya tushindwe kufanya hata maamuzi sahihi.

Kwani kuna shida gani kama watu wangefikiria namna bora ya kuendesha bandari na hivyo ku neemeka kwa 100% na mapato yatokanayo na bandari? Najaribu tu kuwaza.
 
Unfortunately it's over now. Sie ni kichwa cha mwendawazimu, wazungu wameiba mpaka wanatuonea huruma wanarudisha kidogo kwa mlango wa 'misaada', sasa wachina na waarabu wamekuja kujifunzia wizi hapa kwetu.

Tungekuwa ni mwanamke basi ni wale akina dada wenye huruma kwelikweli, vijana wote wanaobalehe kijijini wanakwenda kujifunzia hapo.
 



Anne Kilango Malecela mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania anazungumza kwa kifupi

 
Huko we umeiona mikataba Yao??? Kwanza marekani waliikataa Do enzi za bush akiwa Rais kwa issue za usalama...

Na ujue watu hawapingi uwekezaji, wanaponga aina ya mkataba na vipengele vyake..

Huko kwenye hizo nchi perhaps ikiingia kama kampuni binafsi na sio kampuni ya serikali, na mkataba haukuinguwa btn governments,

Muhimu ni hatujasoma lkn tuna akili kuliko hao maprofesa

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Kama foundation ni mbaya namna hii,

Unafikiri kuna uwezekano wowote wa kuwa na mkataba mzuri??

NEVER.

achana kabisa na pesa za mafuta.

Kuna watu mpaka sasa tayari ni matajiri wakubwa tu.

Bandari ndio engine ya nchi tayari tumeshaigawa namna hiyo.

Hili jambo ni baya halihitaji woga wa coating statements.

Acha uitwe mpinzani ila ukweli usemwe na msemakweli ni mpenzi wa Mungu.

Binadamu anaweza kukuchukia kwa kusema ukweli ila ni binadamu tu lakini tunao wajibu wa kujenga mahusiano mazuri na Mungu.
 
Mkuu, pande mbili zikikubaliana si ndo zaingia mkataba na kutia saini au?

Naona kama wajaribu kueleza maana ya kukubaliana na maana ya mkataba.

DP World wamekubaliana ( baada ya mazungumzo na serikali ya Tanzania) na wakaamua kuingia mkataba wa uendeshaji wa bandari.

Kilotakiwa kujadiliwa wakati wa (consultation period) ni namna terms zitavotumika na kisha kukubaliana hizo terms au kuachana nazo na kuvunja mazungumzo kwa sababu mfano, kampuni haiwezi kuendesha bandari kwa kipindi cha miaka 99.

Nnavyoamini ni kuwa Serikali iliangalia uendeshaji na utendaji wa DPWorld katika nchi zingine za Afrika kama Rwanda, Algeria, South Afrika. Pia itakuwa imepata ripoti ya uendeshaji wa shughuli za bandari katika nchi zingine khasa zile za Ulaya kama Uingereza ambako DP World yaendesha shughuli zake katika bandari ya Southampton na bandari za nchi zingine kubwa tu.

Pia Serikali itakuwa iliangalia umiliki wa kampuni ya DP World ambayo ni kubwa na ipo dunia nzima, je hii inokuja Tanzania ni subsidiary company chini ya mwamvuli wa DP World? Je, yaendeshwa kuwa kutumia jina hilo lakini haina connection yoyote (kisheria) itoifanya kampuni hiyo kuwajibishwa pale itapokiuka "terms" za mkataba?

Je, nini "motive" ya DP World (hii ni kwa mazee wa TISS) kutaka kuendesha bandari nchini Tanzania, kiusalama iko sawa? Je, hakuna mkono wa mtu nyuma yake na mambo kama hayo. NImetumia neno "motive" kwasababu kijiografia nchi yetu ipo kistratejia zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki hivyo kutamanisha miamba ya dunia kama Marekani na Uchina kwamba nani achukue sehemu hii ya kimkakati.

Yaweza kutokea tukasikia DP World wameingia mkataba na wachina au wamarekani katika uendeshaji huohuo na siku kikinuka kumbe tayati mzigo wa silaha uliishaingizwa nchini na kuwa cleared nao tayari kuanza yale ya Sudan.

Je, ni katika msukumo wa Marekani kwamba mchina asipewe bandari yetu aiendeshe ili kuzuia ushawishi wake ukanda huu Afrika mashariki? Haya yote ni masuali ambayo yalipaswa angalau kuonekana yamepitiwa na viongozi na wawakilishi wetu bungeni.

Kiukweli, DP World nnoifahamu mimi kwa uzoefu wa bandari za South Afrika na Southampton ni waendeshaji wa kisasa wa shughuli za bandari. Wana mfumo wa kudhibiti malori yanokwenda pale kwa ajili ya kupakia makontena uitwao "Vehicle Booking System" ambao humkata dereva kujiandikisha na kupanga siku ya kwenda bandarini kuchukua mzigo.

Kisha wana mfumo wa kumpima dereva uitwao "Driver Awareness Assessment" kwamba ana uwezo wa kuendesha lori akiwa ndani ya terminals za bandarini ili asije kusababisha ajali au hata kuzamisha lori.

Pia wana maegesho ya magari ambayo hutoza ushuru kiasi na kutaka dereva ajisajili yeye na taarifa za gari kabla ya kwenda Bandarini na hutaka dereva kuorodhesha abiria kama anao.

Wana mfumo wa kutoa taarifa za ujio wa meli kila siku uitwao Daily Report Status ambao huwekwa katika tovuti yao mtandaoni hivyio kuwafanya wateja kupata habari zilizo "up-to-date".

Ni kweli kwamba bandari yetu haina ufanisi unotakiwa wa kiwango cha juu unoleta tija kubwa na mapato ya kutosha na bado bandarini pana wizi na wafanyakazi wengi waso waaminifu, hivyo ku-"force issue" kwa serikali kujaribu kutafuta mbia wa kuendesha bandari yetu.

Lakini tumewahi kuwa na kampuni za nje ziloendesha TANESCO, DAWASCO na hata mabenki yetu (NBC) hivyo muda wa kujitafakari na kuangali wapi twashindwa umekuwepo.

Nimeangalia kiini cha zogo lililopo kwamba watanzania wengi wamevumbwa na haya makubaliano na kisha Bunge letu kuja kufanya endorsement ya kitu hichi ambacho kina maslahi mapana ya taifa letu na pia kikiwa ni moja ya mali (assets) za nchi.

Lakini pia nimetoa angalizo kuhusu aina ya kampuni ya DP World kwamba kama ni ile "original" ambayo ipo duniani kote na ndo inokuja bandarini Daisaama basi kulihitaji ushauri na maoni kutoka kwa wananchi wa nchi hii au hata kwa wawakilishi wao Bungeni ambao wamepewa makabrasha wasome na kisha waunge mkono hoja.

Ila kama ni DP World ambayo ni "affiliate au subsidiary company" inotumia tu jina au mwamvuli wa DP, basi hilo itakuwa ni jambo la watanzania kujisikitikia na kuomba Mungu atuepushe na mabalaa zaidi huko mbele.

Hizi ni baadhi ya shughuli za kiutendaji ambazo DP World huzifanya bandarini na bila shaka watazileta hapa Tanzania.
 
Aina ya mkataba na vipengele vyake vyote vimejadiliwa kwa kina na Bunge siku nzima ya jana Jumamosi na penye wasiwasi pote pamejadiliwa.

Biashara ya bandari ni nyeti na hatujaanza kuifanya leo wala jana, kuingia kwa kina katika uchumi wa kati kunachochewa na hiyo bandari na nyingine zote kuwa za kisasa.

Jirani yetu wa kaskazini anaumia anapoona tunampiga bao la kisigino kwanza kumaliza treni ya SGR, pili kuingia ubia na DP World, haya yote ni mambo yanayokwenda kimkakati usidhani kuwa rais SSH alijiendea tu kule Dubai.
 
Wanasema jasiri aachi asili.... huyu ndiye wewe ninayekufahamu uncle....
Nimesoma kwakutulia na nimezidi kuelewa zaidi.
Jambo la msingi nyie wenzetu manguli wa sheria pazeni sauti kwanguvu msichoke, nyie ndio wa kutupa chakusema sisi ma layman ama ma bush lawyers.

Napata wasi wasi wangu kwa vipengere hivi ulivyoainisha ni je wanasheria wa serikali hawana uwezo ama wanashinikizwa au hawashirikishwi??

Pamoja na hayo yoote je kitendo cha wabunge, waandishi wa habari na baadhi ya viongozi kupelekwa dubai kushangaa kwa gharama ya hio kampuni iliyojiserkalisha uoni kua ni aina ya RUSHWA, HONGO au PUMBAZO la kuahafifisha uhalisia??

Je wabonge wetu hawana uelewa kiasi cha kuto yaona hayo yote pamoja na kelele zilizopigwa??

Je na ikiwa kwa kelele zote zilizopigwa si rais wala bunge kushtuka na kujikita kwenye mipasho badala wa kuchambua MOU inayotiliwa shaka, je tutakua tunakosea tukitilia shaka USAFI, UZALENDO na nia njema ya rais kwa taifa hili???

Pia kwakua alihusika katika hatua za awali kwa swala hili je tukisema ni yeye ameileta kampuni hii kwa maslahi yake binafsi tutakua tumevunja katiba ya nchi??

Uncle ni saidie majibu ya kila kipengele plz
 

Mie nachokiwaza ni kwamba:

Katika hali ya kawaida tu ni mtu gani ambaye hapendi mafanikio yaende kwao?
Kwamba nami sitaki mafanikio yaende nyumbani?
Nitakuwa kichaa

Swali la msingi:
Japokuwa kuna mambo ya Muungano na yale yasiyo ya Muungano

Ikiwa kweli hao viongozi akiwemo huyo Rais na Mbarawa
wanaamini kuwa kwa kufanya hicho walichokifanya kitaongeza Mapato, ajira, ufanisi na ujuzi kwa wazawa na nchi kwa ujumla wake.

Je, kwanini na znz pia Bandari zake wasingeipatia hiyo Dubai?

kwanini wasingemwambia Rais Mwinyi kuwa tunahitaji znz watu wetu nao pia wapate ajira, ujuzi, ufanisi na mapato?

Ila kwa kuwa wanajua ukweli uliopo nyuma ya pazia ndiyo maana hawawezi shauri jambo kama hili znz

Hapa ndipo watu tunasema kuhusu uzanzibar na utanganyika!

ndani ya siku 1 unasaini mikataba 37 Dubai

Kweli Jambo la kheri msishauri na upande wenu wa znz wafanye hivyo ili nao wanufaike?
Nani hataki faida au manufaa yaende kwao?


hata sijui
Tulimkosea nini Mungu wetu
 
Nyie wanasheria uchwara mnachekesha, mkataba na makubalianono kitu kile kile. Mkataba ni makubaliano ya pande mbili au zaidi, yaweza kuwa written au verbal
 
Mkuu mbona unajifurahisha mwenyewe wakati ukweli unaujua.

Tanganyika kwanza Muungano hauna nafasi tena
 
Mtoa mada nadhani hajasoma katiba ya nchi ya Dubai na katiba ya shirikisho yaani UAE.

angesoma hii hizo katiba unge jua kama Dubai haina uwezo wa kuingia mkataba kama nchi au la.

kama ulivyo sema DPW imeingia mikataba na mataifa mengi katika bara la Afrika na ulaya katika kuendesha bandari....sasa kama hivyo ndivyo mbona unajichanganya ndg. mtoa mada?!!

Ukilinganisha Muungano wa UAE na Tanganyika na znz lazima utakosea, maana Dubai ni mornachy.

DPW kuwa na kesi mahakamani sio kigezo cha utapeli hata kidogo, hizo ni hoja za kuokoteza.

Serikali ya Tanzania haija kurupuka, imefnya due delligency kabla ya kukubaliana na DPW,
kama mtu wa kawaida tu anaweza kupata habari za DPW sembuse Serikali yenye vyombo lukuki!!!

tusiwapotoshe wananchi. tuweke facts tusitoe uzushi.
 
Siasa zile zile za vijiweni. Ufanisi wa bandari ikiwa na uwekezaji wa DP World huwezi kuulinganisha na huu tuliouzoea miaka yote.

Digital Port huwezi kuilinganisha na Port ya kizamani.


Hata smartphone sio sawa na kiswaswandu, lakini kwa kutumia Smartphone mtu hawezi kufanyia uhalifu??!!--- pick up your senses, DP world ametapakaa sehemu nyingi duniani katika shughuli za bandari lakini yeye ndiye anayeongoza kuwa na kesi nyingi kuhusiana ni migogoro ya mikataba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…