Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

Una ushahidi gani kama hizo habari za kesi ni za kweli?. Huko whatsapp wamejaa kila aina ya watu kuanzia matapeli mpaka watakatifu.
 
Tukiachana na ujinga, umaskini na maradhi adui mwingine mpya kwa watanzania ni vyombo vya habari vyenye jukumu la kuripoti matukio tu.
 
Nasubiri ufafanuzi wako wa Ibara zenye utata, ikizingatiwa kuwa IGA ndio utakuwa Mkataba mama (referal agreement) wakati wa kuandaa HGAs.

Je, wewe umefanikiwa kuona na kusoma MoU kati ya TPA na DP World, kwa maana "boss" wa TPA ameitetea sana DPW?
Nmetoka kumsikiliza lipumba akisoma vipengele muda si mrefu jambo tv, nimesikitika sana kwa kweli. Kuna sehemu unasema ukishaanza kutekelezwa hata ikifika kipindi cha renew serikali haina uwezo wa kukataa renew bila kibali cha UAE. Yani hiyo MoU ni ome sided inaomgelea majukumu ya TZ kwa DP world haiongelei majukumu ya DP world kwa TZ. Mkuu ukipata muda kaisikilize maana anao anasa vipmegele tatanishi. Pascal Mayalla
 
Mkuu leo nimeelewa na kusoma topic yako kwa umakini mkubwa sana

Swali langu najiuliza je Professor Palamagamba Kabudi si tuliambiwa kazi yake ni kumshauri mama yetu Samia kwenye kitengo cha mikataba ya kimataifa hakuyaona madhaifu haya au mkataba uliingia nchini ukiwa tayari una signature?

Au yupo ikulu tuu kusukuma Siku ziende ilhali uliyoyaongea naona kama yana Fact kwenye ubongo wangu!

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa
 
Na cha kushangaza zaidi, mama Samia wakati anamtoa kwenye uwaziri, Prof. Kabudi alisema atakuwa ndio baba wa mikataba,sasa Jana kwenye hoja hii hakusikika kusema chochote na kama alihusika,angalau angetetea lakini hakusema chochote,labda hakushirikishwa.
Wabunge wetu wao wanadhani watanzania wanapinga uwekezaji,No, kinacholalamikiwa ni vipengele vya mkataba vyenye utata na viko wazi, lakini wawakilishi wetu hawavioni,wanaishia kutoa matamko ya kutishia wanaokosoa mkataba.
 
Hilo Bunge la Magufuli ni hasara na mzigo kwa Taifa.

Ndio maana tunahitaji Katiba Mpya Leo kuliko juzi na jana.

Kukomesha ufisadi na kuondokana na huu utamaduni wa kifasadi ulioota mizizi zaidi ya miaka 40 sasa nchini, we need to RESET.
Mkataba unafanana na mingine, mfano wa Loliondo na Ile ya madini. Ni Lazima sasa tutoke hapa tulipokwama na kukwamishwa.
 
Conclusively ni kwamba tumepigwa na Wabunge wa CCM
 
Mimi sio mwanasiasa na kwanza siasa siipendi nilichokiona ilikuwa ni mipasho law wapinzani rejea mchango wa mbunge waitara,na press ya kibajaji
Nilidhani wangekuja na vipengele vp vitatuumiza na vipi tuvitoe wao wanaongea kama wapo najukwaani nilijikuta nawashangaa sana maana watakuja kuulizwa hata wao siku moja mkataba ulikuwa unasema nn utashangaa na wao hawajui
 
Conclusively ni kwamba tumepigwa na Wabunge wa CCM
Uliwahi kutegemea wafanye tofauti?

Wamefanya "walichoteuliwa" kukifanya na hayati Magufuli, na pia wamekamilisha kazi "waliyotumwa" na CCM. Wako pale kwa maslahi na malengo ya hao waliowaweka hapo.

Iko hivyo na itabaki hivyo Hadi pale tutakapobadilisha hilo - Katiba Mpya!
 
Mimi nilidhani pamoja na kuwa nchi Ina mfumo na vyombo vya kusaidia ulinzi maendeleo na kulinda maslahi yake, idara ya Usalama wa Taifa ingekuwa ndio chombo makini na nyeti kwa yote.

Hili jambo la bandari, idara inahusikaje hapo? Haina taarifa za kujibu mashaka? Haina stadi za kuchambua, kupima na kuainisha faida na madhara kwa miaka mingi ijayo?

Mbona hata waziri mwenye dhamana inaonekana kama kastukizwa kwa baadhi ya hoja?

Haipendezi jambo kubwa kama hili kupitishwa kwasababu mkuu kaona ni jema. Lipitishwe kwa sababu hoja zote za msingi kiusalama, kibiashara, kiuchumi na maslahi vyote vipo sawa.

Kama idara ya Usalama huwa inaingizwa kazini baada ya wakubwa kusaini, nahisi siyo salama. Au kama hiyo idara haikuwa na ijuacho kuhusu huyo mwekezaji kiasi cha kushindwa kupenyeza taarifa kwa wakuu, mantiki inaniongoza kuamini Kuna tatizo.

Hili ni funzo, Kuna rekebishika. Leo tumeanza na bandari. Mambo ya ufanisi kwetu ni kitendawili. Huenda mbele tutahitaji pia wawekezaji kwa kila kitu.

Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 
Una akili kubwa sana sema huwa inazongwa zongwa na uoga Mixer unafiki. Ndio maana unazunguka sana ili kutuambia Namba Moja ni Aidha hajielewi(Hana akili) kabisa au Ametishwa na anawaogopa sana Bwana Mananasi na Mchele wa Igunga. Na zaidi andiko lako hili ni kama unasema Hao watu wasipokuwepo Chini ya hili Jua letu, basi Tz inaweza kuwa nchi konki kinyama. Huyu bwana ni wakutandika Shabazz hadharani
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] idala yetu pia inaweza kuwa manipulated tuu mkuu ni watu wale Kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa waandishi wa magazeti wameahidiwa fedha iwapo watapigia Debe mkataba wa kuuza nchi!
These mercenaries are now busy spinning to facilitate the sale of our country kama Mangungo wa Mvomelo alivyouza kwa shanga enzi hizo za utumwa!
Nchi unaiuzaje kwa mfano?. Tulikuwa na TICTS, mbona nchi yetu bado tunayo?

Pale Airport kuna Swiss port na NAS, hawa DP World hawatakuwa wa kwanza kufanya biashara hapa nchini.

Uoga unatusumbua miaka yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…