gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,312
- 3,345
Ndugu zangu mimi ni CCM tangu udogo wangu na mwenye kadi hai kabisa nikiwa na maana kadi yangu nailipia kila mwaka.Nilijiunga CCM rasmi kwa maana yakuchukua kadi ya uanachama 2019 mara baada yakufika chuoni mwaka wa kwanza.
Nasisitiza sitahama chama changu kwa kuwa CCM naipenda toka moyoni ila nitakachofanya ni kuwaadhibu kwa kura viongozi kwa mwenendo usiofaa na sina sehemu nyingine yakuwaadhibu zaidi ya sanduku la kura.
Nafanya hivi kwakuwa nimekosa namna tofauti kwani viongozi hawataki kushauriwa wanahisi wao ni malaika lakini watambue awamu ya tano imetesa sana wananchi kuliko hata mkoloni.
Nasisitiza kutumiiza kwakigezo cha ndege, madaraja, umeme, maji nk sio sawa, hali ya maisha imekua ngumu sana huku mtaani.
Nakumbuka yupo mwananchi mmoja alidiriki kumwambia rais kwa uchungu,"mheshimiwa ruhusu pesa hali huku mtaani ni ngumu sana". Majibu ya rais ,"Asiyefanya kazi na asile". Hili sio jibu la kiongozi kwa mwananchi wake badala yake raisi alitakiwa kuwaza kwamba kuruhusu pesa sio kuwapa wananchi pesa mfukoni bali ruhusu ajira serikalini,ondoa kodi za hovyohovyo siku hizi faini imekuwa chanzo cha mapato kuliko hata VAT.
Yote kwa yote huu ni msimamo wangu na sitahama chama changu ila kwa mwaka huu kura mtanisamehe sitapiga kura CCM.
Wakati sisi tunapata tabu na tukiwaambia mnatujibu vibaya nyinyi mnaishi kwa raha na mnajisahau kuwa hio raha mnayoishi nyinyi chanzo ni sisi kuwapigia kura.
Kwa mwenye hofu na mimi juu ya mapenzi yangu kwa CCM apitie post zangu za nyuma.