Uchaguzi 2020 Japo inaniuma lakini kwa kuwa chama changu mmeendekeza sana ubabe sitawapa kura yangu

Uchaguzi 2020 Japo inaniuma lakini kwa kuwa chama changu mmeendekeza sana ubabe sitawapa kura yangu

Majibu ya hayo yote unayoniuliza yapo kwenye maelezo ya awali vinginevyo unahitaji nikupatie majibu yakukupendeza,
Msimamo wangu ni kutohama CCM maisha yangu yote lakini huu ndio uchaguzi wangu wa kwanza kutopigia kura raisi wa CCM.
siasa bora ni siasa yenye misingi yakidemokrasia,na demokrasia bora ni mimi kuchagua kwa kadiri ya matakwa yangu
Hapo juu ulieleza kwamba ulijiunga CCM 2019, sasa ni chaguzi gani "zote" ulizopigia CCM, au zile chaguzi za serikali za mitaa zilizofanyika kama maigizo?
Naona hauko serious mkuu 'gimmy's' na msimamo wako huo wa kuwa mwanachama wa maisha wa CCM. Magufuli kakutumbua?
 
Yamebaki masaa machache sana ili na mimi nikamuadhibu anayetuadhibu kwa madaraka ambayo tulimpatia wenyewe 2015,ametuazibu kwa miaka miatano lakini sasa tuseme basi,ninaimani kura yangu moja inatosha kabisa kubadilisha matokeo kesho.
Ninamuomba Mungu raisi ajaye asiwe na kiburi kama huyu wa sasa,asiwe mkabila,asipendelee kwao bali aongoze tanzania kama taifa moja,awe anapenda kushauriwa na athamini ushauri wa wengine,aheshimu viongozi waliomtangulia,akumbuke maendeleo ya vitu pasipo maendeleo ya watu ni kutesa wananchi.
Amina.
 
Mhindi akiwa na duka anasalimia majirani zake wote na kuwafanya wateja wake. Wenyewe wanasema “ every penny counts “ hapa ni kuwa “every vote counts”.
Mkuu, hata ikihesabiwa, huyo mshogeshaji (anayetaka wote muwe mashoga) utakayempigia atazidiwa kwa kura mamilioni, sasa tija iko wapi hapo? Ingekuwa kuna tight race kweli kura yako ingekuwa na tija.
 
Utakuwa umefanya jambo sahihi, kwa nyakati sahihi. Utakuwa mmojawapo katika historiamlll
Rais ni kama mzazi anapaswa kuwapa tumaini raia wote. Wapo wana ccm wengi wenye hekima hawapendezwi na kauli za mkuu za kibaguzi na dhihaka." Siwafichi" " Mtajuta" " Huwezi kunijibu hivyo wewe" ( Mama DED BK, kupoteza uteuzi kutotaja fungu kiasi barabara akihofia kuposha); " Niliahidi mafuriko" ..." Wa mabondeni wafurike... wauzieni nei kubwa" " siwezi mchagua DED nimpe gari,nyumba,mshahara halafu amtangaze mpinzani" " Hakuna fidia" .." Mtajuta" " Pesa zipo nakamua mafisadi na majizi"( wafanyabiashara).
Kuwapa kura ccm kwa sasa ni kuhalalisha dhulma, kwa sasa wamebanwa wanaanza kuamrisha hovyo polis na tume ya uchaguzi kutenda mambo ya hovyo...
MUNGU TUSAIDIE. HAKI HUINUA TAIFA
 
Back
Top Bottom