KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Pongezi kwako kwa uamzi huo.Yote kwa yote huu ni msimamo wangu na sitahama chama changu ila kwa mwaka huu kura mtanisamehe sitapiga kura CCM.
Wakati sisi tunapata tabu na tukiwaambia mnatujibu vibaya nyinyi mnaishi kwa raha na mnajisahau kuwa hio raha mnayoishi nyinyi chanzo ni sisi kuwapigia kura.
Kwa mwenye hofu na mimi juu ya mapenzi yangu kwa CCM apitie post zangu za nyuma.
Lakini nikuulize swali. Ulijiunga CCM 2019, nini kilikuvutia huko hasa hadi ujiunge na chama hicho?
Na unasema huhami CCM, kuna kitu gani hasa kinachokuvuta uwe na mapenzi makubwa kiasi hicho na chama ambacho kilishabadilika mara kadhaa katika miaka hii ya karibuni.
Kumbuka, sijakushawishi popote katika maswali yangu hayo ujiunge na chama kingine chochote cha siasa mbali ya hiyo CCM yako. Unayomipango ya kuweka ushawishi ndani ya chama ili kuleta mabadiliko unayoona yanafaa?