Uchaguzi 2020 Japo inaniuma lakini kwa kuwa chama changu mmeendekeza sana ubabe sitawapa kura yangu

Pongezi kwako kwa uamzi huo.

Lakini nikuulize swali. Ulijiunga CCM 2019, nini kilikuvutia huko hasa hadi ujiunge na chama hicho?
Na unasema huhami CCM, kuna kitu gani hasa kinachokuvuta uwe na mapenzi makubwa kiasi hicho na chama ambacho kilishabadilika mara kadhaa katika miaka hii ya karibuni.
Kumbuka, sijakushawishi popote katika maswali yangu hayo ujiunge na chama kingine chochote cha siasa mbali ya hiyo CCM yako. Unayomipango ya kuweka ushawishi ndani ya chama ili kuleta mabadiliko unayoona yanafaa?
 
Mhindi akiwa na duka anasalimia majirani zake wote na kuwafanya wateja wake. Wenyewe wanasema “ every penny counts “ hapa ni kuwa “every vote counts”.
Ooh sababu kuna tume mpya..........kila mtu ajitoe akili tu ila baada ya uchaGuzi kila mtu ataondoka na 50 zake.....wale wenye kura nyingi na wale wenye urais.............
 
Tuendelee na kampeni hii kuanzia majumbani kuikataa ccm kwa ikatili na ubabe
 
Hata tukisema tutaiba utafanyaje?
Wee una ubavu wa kusema? Kusema na kutenda ni vitu viwili tofauti. Isije kuwa wewe ni mkereketwa mwenye T- shirt ya CCM iliyopauka Polepole hajui hata kama unaishi.
 
Nasisitiza sitahama CCM kwani chama kwangu ni imani,hii CCM ya Magufuli imekua chama cha kikundi fulani cha watu na mwenyekiti wao,CCM hii yenyewe inafikiri serikali na mamlaka ndio kila kitu kwao hili haliwezekani na si lakufumbia macho.
Kiongozi asiye na hekima hafai,kiongozi mwenye kiburi hafai kwangu.Yanayoendelea kwenye utawala huu yanaumiza watu hili si lakufumbia macho.
Nakumbuka siku moja Jakaya alizuia ubomolewaji wa jengo la Tanesco ubungo akawauliza swali Tanroad na naomba nimnukuu,"Hivi ikitokea jengo la kale la kihistoria likawa limejengwa sehemu ambayo ni kinyume cha sheria nalo mtalibomoa?"
Kwa asiye na akili anaweza fikiri Jakaya alibariki uvunjifu wa sheria la hasha bali alimaanisha kuna mambo yanahitaji hekima kwenye maamuzi jambo ambalo watawala wa sasa ni tatizo.
Ndugu yangu kero yangu kubwa ni mambo ya hovyo yanayoendela sasa,huu utawala unatesa sana wananchi.
Mfano;Mfanya biashara leo akichelewa kulipa kodi hata kwa siku moja baada ya muda kupita adhabu ni faini ya karibu 100% ya alichotakiwa kulipa hii sio haki na kwa bahati mbaya watala hawashauriki unataka tufanye nini labda.
Njia pekee ni sanduku la kura na kwa hakika kuanzia ndugu na familia huu ndio ushawishi wangu na si vinginevyo
Hivi unaacha kuajiri watu kwakisingizio cha kujenga miondombinu hili ni sawa?
 
Yoote haya Dr Mpango anajua, lkn anaogopa kumshauri yule nyapala maana alishasema hapangiwi chochote na yeyote!!!
 
kura moja ya mjiinga
 
Mkuu 'gimmy's' ninakubaliana na wewe kwa haya uliyoeleza hapa, lakini hujanishawishi kuhusu uzuri wa CCM iliokuwa nao uliokufanya ujiunge nayo mwaka 2019!
Hata kabla ya ujio wa Magufuli, CCM ilishakuwa mbovu.

Ukinieleza hapa kwamba nia yako ya kuwa ndani ya CCM ni kuirekebisha ili iwe chama imara kinachopigania maslahi ya waTanzania wote, na ukaainisha mambo yanayokuvutia na kuyaona ndani ya CCM hiyo, hapo nitaungana nawe moja kwa moja, na nitazidi kukupongeza kwa msimamo wako huu wa sasa, na juu ya hayo unayokusudia kuyapigania ndani ya chama chako.

Hapa hujanishawishi nielewe kwa nini wewe ni mwana CCM.
 
Majibu ya hayo yote unayoniuliza yapo kwenye maelezo ya awali vinginevyo unahitaji nikupatie majibu yakukupendeza,
Msimamo wangu ni kutohama CCM maisha yangu yote lakini huu ndio uchaguzi wangu wa kwanza kutopigia kura raisi wa CCM.
siasa bora ni siasa yenye misingi yakidemokrasia,na demokrasia bora ni mimi kuchagua kwa kadiri ya matakwa yangu
 
Kwanza: hongera kwa kujitambua.

Pili: kataa sisiem kwa nguvu zote kijana.

Tatu: Lingania vijana wenzako wa lumumba na watu wako wa karibu kadri uwezavyo kwani sisiem imekengeuka misingi yetu kama Taifa.
 
Wee una ubavu wa kusema? Kusema na kutenda ni vitu viwili tofauti. Isije kuwa wewe ni mkereketwa mwenye T- shirt ya CCM iliyopauka Polepole hajui hata kama unaishi.
Ajue asijue ila mimi najua Magufuli anaendelea 5 tena ....povu lako kafulia vyupi vya pipooz
 
Kitanuka....hao tume wenyewe wamebaki kumpa Hope Jpm lakini siku ya uchaguzi watamshangaza.
Kinuke watu wenyewe wanategemea hadi mzungu awapige busta ....kdg wazenj ila huku bara ma keyboard warrior kibao
 
Watampa wale wengine usijali
 
Bora mmoja wa wanachama ulivyoeleza hisia zako kuwa mambo yanakwenda ndivyo sivyo
 
Kwanza: hongera kwa kujitambua.

Pili: kataa sisiem kwa nguvu zote kijana.

Tatu: Lingania vijana wenzako wa lumumba na watu wako wa karibu kadri uwezavyo kwani sisiem imekengeuka misingi yetu kama Taifa.
Hapana,tatizo sio CCM bali ni mwenyekiti,bado CCM sina chama chakulinganisha nacho,mwenyekiti anaongoza nchi vibaya,mwenyekiti amejawa visasi,mwenyekiti hana sifa kabisa za kuwa kiongozi,
Nakumbuka marehemu Kingunge alisema kunawatu walipaswa kuwa wanyapara lakini sio kuongoza nchi kauli ambayo hua naikumbuka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…