Uchaguzi 2020 Japo Magufuli atashinda lakini ilitakiwa ashindwe

Uchaguzi 2020 Japo Magufuli atashinda lakini ilitakiwa ashindwe

lanez

Member
Joined
Apr 18, 2019
Posts
78
Reaction score
163
Hapa ntajikita kujadili mambo ya (EI) yaani emotional intelligence. Bila shaka kila mtu atakubali kwamba Rais wetu ana tatizo la emotional intelligence, hivyo kusababisha kuonesha hisia zake hata sehemu ambayo haikustahili.

Rais Magufuli, ni mtu ambaye anajitoa kwa kiasi fulani, japo wapinzani wake wamekuwa wakimkosoa kwa mambo mengi sana. Kwa mtizamo wangu hayo husababishwa na (modality & methodology) anazotumia kutekeleza matamanio yake, huenda lengo lake likawa jema kabisa lakini kwa sababu anatofautina mtizamo na wapinzan wake basi hujikuta anapingwa sana. Rais Magufuli, anamini yupo sahihi kwa anayoyafanya huku akiungwa mkono na wananchi kwa kiasi fulani.

Licha ya harakati nying za Rais Magufuli, kuiletea Tanzania maendeleo, lakini imeonekana watanzani bado hawaelewi methodology & modality anazotumia. Hii imepelekea kuwepo kwa upinzan AMBAO haukutarajiwa kabisa. Hili limeonekana baada ya ujioa wa hasimu mkubwa wa Magufuli kwenye siasa za Tanzania ndugu Tundu Lissu. Kwa kiasi fulani ndgu TL ametia hamsha hamsha kweny siasa za Tanzania, mpaka kufikia wachambuzi wengi na waumini wengi wa demokrasia kuona sasa kutakuwa na upinzan wenye nguvu kuelekea uchaguzi wa October.

Lakini tujiulize, je Rais Magufuli anafurahia haya yanayoendelea kuonekana tangu ujio wa Tundu Lissu pale uwanja wa ndege mpak huko mikoani? Rais ni mtu anaye penda kujituma kwake, kuoneshwe kuthaminiwa, anataka ashukuliwe, apongezwe na kusifiwa, na hapa ndipo furaha yake ilipo. Lakini kwa kinachoendelea kuelekea uchaguzi wa October, Rais Magufuli ataona watanzani ni watu ambao hawana shukran wala hawastahili kufanyiwa jema lolote, hivyo hali hii kusababisha Magufuli kuwachukia baadhi ya watanzani wazi wazi kama alivyoonesha baadhi ya maeneo kweny kipindi cha uongozi wake.

Rais Magufuli, anasahau mambo ya demokrasia linapokuja swala la yeye kutopongezwa na kusifiwa kwa alichofanya. Kwa vile Rais ana tatizo la emotional intelligence (EI) basi tutegemee ubaguzi mkubwa, majibu mabaya kwa wananchi baada ya uchaguzi, kejeli na pengine kuongeza kibano zaidi kwenye mambo mbali mbali. Sasa ili kuepusha yote haya, ambayo yataacha makovu mengi baada ya yeye kuondoka 2025, ilitakiwa ashindwe kweny uchaguzi huu wa 2020.

Nimalizie kwa kuwashauri watu wa Public relations, kutoka ofisi ya Rais kumfanyia counseling Mh Rais, ili achukulie ushindani wa kisiasa kama njia ya kufikia maendeleo, maana licha ya kuahidi kumaliza upinzan ifikapo 2020, lakini bado kuna upinzan mkubwa tena imeonekana watu ndio wana moto zaidi ya 2015.
 
Rais Magufuli ni mwanademokrasia ndiyo maana alisikitishwa na kitendo cha Lissu kupigwa risasi na alimpelekea pole. Kielelezo ni alivyoruhusu mikutano ya vyama vya upinzani kwa sasa wakati wa kusaka wadhamini kwake anajua ni sehemu ya demokrasia, na aliishauambia ulimwengu kuhusu uchaguzi huru na haki. Aidha uwepo wa vyombo vingi vya habari na magazeti nk ambavyo vinavyomkosoa kila siku ni ushahidi wa demokrasia na pia vikao vyake na baadhi ya vyama vya siasa.

Kinachomuudhi pengine ni lugha za matusi na uchochezi zinazoweza kuingilia uhuru binafsi wa watu, utu, heshima na kuvunja katiba na amani kwa kivuli cha demokrasia.Wale wenye kujipendekeza hilo analijua ndiyo maana alilikemea siku ya ufunguzi wa jengo la TAKUKURU Dodoma. Naomba tusipotoshe kuhusu haiba halisi nzuri ya Rais wetu kwa hoja mfu,tuseme ukweli bila ushabiki wa kisiasa.

Tufuatilie kwa makini rekodi yake ya huruma na kusamehe kwa hofu ya Mungu i.e Nape, Mkurugenzi Kibiti nk. Siyo mtu wa visasi. Tusipotoshe. Naelewa Kuongoza nchi kuna changamoto zake ila kiukweli ameweza sana kwenye maeneo mengi kwa ujasiri mkubwa yakiwemo ya nidhamu serikalini, miradi ya maendeleo, ukusanyaji kodi, kulinda raslimali za taifa, kurahisisha maisha ya watanzania kwa malengo ya muda mrefu i.e Angalia meli, elimu bure, mabarabara, umeme, afya.

Haya ni mambo makubwa yenye athari chanya kwa maisha ya wananchi .Wenye mitizamo finyu huangalia maendeleo haya bila kuyaunganisha na maisha ya kila siku ya wananchi na kupotosha kuwa ni ya vitu. Tumchague tena Magufuli mitano 5 Watanzania tusiyumbishwe kwa hili.
 
Hapa ntajikita kujadili mambo ya (EI) yaan emotional intelligence. Bila shaka kila mtu atakubali kwamba Rais wetu ana tatizo la emotional intelligence, hivyo kusababisha kuonesha hisia zake hata sehemu ambayo haikustahili...
Wewe ni Shabiki maandazi hata card ya kupiga kura huna
 
wapinzani wa kweli wa awamu hii ni wapenda :amani,maendeleo,haki,demokrasia na wale wote wenye akili zilizopevuka! Kodi za watanzania zinatumika kununua majogoo mitaani wakati hospitali hazina madawa,kodi zetu zinatumika hovyo....simply wapinzania wa awamu hii ni watanzania wenyewe ....tena walipa kodi!
 
wapinzani wa kweli wa awamu hii ni wapenda :amani,maendeleo,haki,demokrasia na wale wote wenye akili zilizopevuka!
kodi za watanzania zinatumika kununua majogoo mitaani wakati hospitali hazina madawa,kodi zetu zinatumika hovyo....simply wapinzania wa awamu hii ni watanzania wenyewe ....tena walipa kodi!
Safari hii tumchague mtanzania mwenzetu atakuwa na uchungu na watz
 
Pamoja na yote kwann yameshindwa kubadilisha kuboresha maisha ya watz,
 
Umeendakika story ndefu sijui ya nini, ukatishwe tamaa kuna mtu anamlazimisha kuwa kiongozi au Tz ni yeye tu ndiyo anaweza kuwa kiongozi, aondoke waingie wengine ambao hawahitaji kusifiwa kufanya kazi zao. Angekuwa halipwi hapo tungemsifu
 
wapinzani wa kweli wa awamu hii ni wapenda :amani,maendeleo,haki,demokrasia na wale wote wenye akili zilizopevuka!
kodi za watanzania zinatumika kununua majogoo mitaani wakati hospitali hazina madawa,kodi zetu zinatumika hovyo....simply wapinzania wa awamu hii ni watanzania wenyewe ....tena walipa kodi!
Huna akili wewe, kodi ya Tanzania over trillion kwa mwezi na jogoo mmoja tena wa laki, Bado hiyo laki imerudi kwa mwananchi, fikirisha ubongo wako vizuri.
 
Makomunist yeyeto huwa hayataki mtu yeyeto mtawaliwa awe maarufu kuliko anayekutawala, watz msifurike kwa Lisu msimpe umaarufu mnaumiza watu huku watakufa kwa Presha bado tunawahitaji
 
Suala la freedom of Expression linategemea matakwa ya Mtu au Katiba?

Rais aipende au aichukie Demokrasia sisi halituhusu. Hoja ni katiba inatakaje. Nchi haitawaliwi kwa Matakwa ya Magufuli. Na hapo ndipo anapokosea na kujijengea uadui usio na ulazima kwa wenyenchi.
 
Back
Top Bottom