Wanabodi,
"Watakao Rudi Bungeni ni 'Wakijani' "
Haya sii maneno yangu, na sio maneno ya kuambiwa ni maneno yaliyotamkwa na ambayo nimeyasikia mwenyewe kwa masikio yangu mwenyewe!.
Japo maneno haya ni maneno machungu kumeza, kwasababu Tanzania ni ya Watanzania wote na siyo ya 'wakijani' tuu, lakini huo ndio ukweli wenyewe!, Watanzania woote katika Umoja wao, wamewakubali sana 'wakijani' na hili watalithibitisha tarehe 25 October, 2020. Mwenye masikio na asikie!.
Sisemi yamesemwa na nani na yamesemwa wapi, bali nawaomba tuu mniamini!.
Hongereni sana 'Wakijani'
Tulipokuwa tukiwaeleza humu kuhusu Watanzania tujifunze kuukubali ukweli hata uwe ni mchungu vipi kama ukweli huu
Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
Mlinibeza!.
Niliposema kuhusu hoja ya wabunge wasio wa kijani, wakitaka kurejea Bungeni 2020 ni lazima wajitambue
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
Pia mlinibeza humu.
Sasa leo Bunge limevunjwa rasmi, tegemeeni "the mass exodus" kwa wabunge wasio 'wakijani' watakao jitambua, they will do the needful, kwa ving'ang'anizi na wenye misimamo, ambao watashikilia msimamo kwa kusimama na wanachokiamini, hawa ni mashujaa!, watakufa kizungu na tai shingoni na kama ni meli au jahazi, hata likumbwe na tufani kubwa kiasi gani, wao watazama na meli yao au jahazi lao na watatamkwa mashujaa watakufa kishujaa!, hoja ya kati ya "waliojitambua" hai, na 'mashujaa' wafu, nani ni muhimu zaidi, ni debatable!.
Kwaheri ya kuonana hadi Novemba
2020... "ndani ya nyumba" panapo majaaliwa!.
Paskali