Japo niridhike

We nae mchunguzi niliibania thanks lakini umenigusa imebidi nikupatie. Poa usijali

hahaha....asante kugawana ni kujali Dena.......uchunguzi kawaida yangu kabisa...sipendi kukurupuka....unanifurahisha sana
 
Kumsamehe amsamehe ila wanaume wakiambiwa ukweli masimango utakayopata utajuta kuzaliwa mie nakwambia ukweli.

Amwamwambie tu ukweli ili yaishe, mi nishawahi kuwa na rafk mumewe alikuwa anamnyanyasa sana kila siku ugomvi na kufukuzana mwanaume anawanawake nje akiulizwa ugomvi mpaka anamfukuza mkewe. Mkewe nae akapata wa kumfariji huko nje cku moja mumewe kama kawaida yake akagombana na mkewe na kumfukuza yule dada akamwambia jamaa wake wa nje akamwambia ucjali akampangia nyumba na kumnunulia full fanicha mwanaume kuja kuckia wacha roho imtange akamuomba msamaha mkewe na kibaya zaidi mke alirudi na mimba juu ikabidi waitoe wakaendelea na maisha na huyo mume kakoma hamfanyii tena visa mkewe kwani ashajua ukisema cha nini mwenzio anasema nitakipata lini. So amwambie tu ukweli na kama jamaa kajirudi kiukweli aachane na huyo jamaa kiustaarabu ila amwambie ukweli na amwambie kabisa kwamba alikuwa anasomesha na watoto wako wakati umeelemea kwa kimada, Hiyo itakuwa dawa kubwa nyamayao wala huyo mume hatorudia tena kufanya huo ujinga wake
 
Hebu mweleweshe huyo rafiki yako kwamba hawezi kuwa na mme na mfanyabiashara kwa pamoja....

nitamueleza.....lakini Roya naomba nikuulize, kwa maana hiyo mume yeye ndio anaweza kuwa na mke na hawara bila usumbufu wowote? ni haki yake?
 
mmmmm yaani this story looks so real....and like somebody said hapo juu hamna ndoa hapo....ni kwa ajili ya watoto hata umsamehe mtu...its now living for the kids. dawa yake huyo mume kaipatapata..serves him right, tell your friend to play her cards carefully. ama aombe talaka kabisa watoto si wanamjua baba yao? did they ever ask baba yuko wapi hiyo miaka miwili???
 


Mpotezee Luv....turudi kwenye mada.....
 
huyo mume ana kitu moyoni kwake na si kizuri nakwambia kuna msemo unasema "mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu" ndio una-apply hapo huyo jamaa ameachana na hawara anategemea mke wake atafanya hivyo ili maisha yaende vizuri lakini inaposhindikana kwa sababu ya mtu ni tatizo

i'm telling u Nyamayao najua unaongea kama unaona huyo jamaa amekomolewa ila angalia kwa upana sana ilo ni tatizo kubwa sana, mshauri rafiki yako either aachane na huyo mfanyabiashara au aombe talaka zaidi ya hapo kuna mmoja ktk hao wadau ataonja mauti kutokana na ilo tatizo

Materials si kitu ktk maisha huyo dada najua amefuata zaidi hela na mtu usitumie fedha kumnyanyasa m/ume mwenzio kwa kumchukua mkewe na kumjengea na kumnunulia magari na kulipa ada na matumizi mengine. Kumbuka huyo dada anamkomoa mmewe au ilikuwa ni njia ya kujitoa kwenye mateso ya ndoa ila kwa huyo mfanyabiashara na kwamba anaiba mke wa mtu tena kwa kutumia uwezo wake kifedha. Kwa m/ume yoyote hiyo ni dharirisho kubwa sana ndio maana naona hapo hakuna ndoa tena. Fikikria kwa mapana sana utaona tatizo kubwa lililopo hapo ndani na hicho kitendo cha mme kwenda na mkewe sehemu mfanyabiashara alipo ni dalili mbaya kuwa kuna mitego inawekwa ambayo siku ikipata prove im telling utaudhuria msiba. Najua kabisa jinsi w/ume wasivyo na moyo wa kuvumilia

Najua utasema kuwa mbona yeye alimfanyia mabaya mkewe lakini "two wrongs does not make it right" hivyo naona mwisho mbaya sana hapa na huyo mdada amefanya kosa kwa kulipiza kosa kwa kosa ambapo sasa mwenzake ametubu na kosa limebaki kwake

Huu uhusiano unatakiwa usitishwe kabisa au lah wahame huo mji na hiyo nyumba aliyojengewa huyo mama waiuze au wamrudishie huyo mfanyabiashara na je huyo mfanyabiashara ana mke? huoni kuwa mnazidi kuongeza tatizo kwenye familia nyingine ambayo nayo inaweza ikaleta tatizo jipya kama hili

Hii ni laana ya zinaa aaaagh what kind of life is this? ikinitokea mimi naua mtu i swear
 
Hivi ni wewe Nyamayao tumjuwae au tumebadilishiwa leo? Nyamayao nayemfahamu mkemea maovu wetu hapa hawezi kumuendekeza rafiki kama huyo.
 
Nyamayao mimi nachoshauri hapa ni bora huyo mwanamke asimwambie mume wake ila afanye jukumu la kuweza kuachana na huyo mfanyabiashara pole pole na kwa umakini wa hali ya juu, otherwise akimwambia you never now what reaction atakuwa nayo huyu mwanaume i believe na inferiority complex atakuwa nayo itakayosababisha kwa mwanaume either kujiua au kumfanyia kitu mbaya mke wake au huyo mfanyabiashara
 

Kweli kabisa yaani wanaume wanadhani cjui sisi tuna mioyo ya chuma kibaya zaidi hata ada ya watoto alikuwa halipi c kama asingekuwa huyo bwana wa nje watoto c wangekuwa wameacha shule? Muwe mnafikiria kabla ya kuamua huyo dada amwambie tu ukweli umuume mpaka akome na cku nyingine hawezi kurudia ujinga aliokuwa anaufanya we unazamia kwa hawara unasahau mpaka kulipa ada ya watoto pweeeeeee natamani mimi ndio ningekuwa huyo dada angenikomaje ningemuonyesha mpaka hiyo nyumba niliyonunuliwa then tuombane msamaha yaishe tuanze upya kama kweli amejirudi kiukweli
 

nimekuelewa maty, lakini kwa tunavyomjua mume nina mashaka kama atalichukulia hili suala ki rahic hivyo, mie nimehic na nimemshirikisha frnd wangu labda jamaa anataka kupata uhakika kutoka kwake na kitachofata mungu anajua, na hofu kubwa ni kwamba mfanyabiashara ana mtandao wa kutosha yacjetokea ambayo hatukutegemea chini ya jua, aambiwe kabisa na watoto anawasomesha/watunza ? jamani Maty...unajua kingine huyu frnd wangu ni very smart,hakujisahau/bweteke kwa miaka yote miwili, watoto hawamjui huyo mfanyabiashara, hata hawajawahi kuona sura yake, lakini mfanyabiashara anawajua watoto vzr, mama anatoka outing na watoto wanafurahia maisha mfanyabiashara anakamilisha kila kitu wanajiondokea, mume amewahoji watoto mpaka kawatishia sana watoto wamesema ukweli wao hawajawahi kumuona mtu baki ndani....mume anazidi kuwa njia panda.
 
nitamueleza.....lakini Roya naomba nikuulize, kwa maana hiyo mume yeye ndio anaweza kuwa na mke na hawara bila usumbufu wowote? ni haki yake?

Haki yake ya asili.....ila hapa huzungumzii kulipiza...
 
Nyamayao, huu msredi umeenda sana hata sijui kama kuna watu wameshakuuliza hili swali:

Huyo mfanyabiashara alikuwa anajua kama friend wako ni MKE WA MTU?

Hilo tu kwa sasa, mengine ntakuuliza badae.
 

ooh yeah....sema mama alikuwa anawadanganya ady anasafiri coz c alikuwa anakujaga labda mara moja kwa wiki au mara moja kwa week mbili, bac mama alikuwa anawaambia dady yupo safari nje ya nchi ili wacmwambie amcal waongee nae, walikuwa wanam mic day wao sana, lakini dady ndio hivyo tena.....mie nawauliza akiomba talaka na hili vuguvugu lililopo haita leta shida jumla? yaani huyu mume atoe talaka tu ili hali inajua mke wake ameshamsamehe? mke aanzie wapi kuomba talaka?
 
Nyamayao:

Kati yao wote hao hakuna aliyekwisha ambukizwa VVU?

- your friend
- your friend's man
- your friend's hawara
- your friend's hawara's wife
- your friend's hawala's wife' hawara

and the list goes on!

Kama yupo basi waendelee - Sinza Makaburi yanaonekana kujaa, Kisutu nadhani pia yamejaa - Kinondoni kule chini watu washanunua - labda waje mitaa ya huku Bunju kushika nafasi ya makaburi mapema!:rip:
 

Naheshimu kabisa mawazo yako NY,
Nilitaka kujua, huyu mfadhili warafikio ana mke/familia? Kama anaye basi hapo ni shughuli pevu!
 


Labda Bunju B. Kuanzia Tegeta mpaka Bunju A viwanja vya bustani za kuotesha binadamu zimejaa!
 
Nyamayao, huu msredi umeenda sana hata sijui kama kuna watu wameshakuuliza hili swali:

Huyo mfanyabiashara alikuwa anajua kama friend wako ni MKE WA MTU?

Hilo tu kwa sasa, mengine ntakuuliza badae.

Mjukuu yuko wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…