Kwa maoni yangu; wimbo huu siyo mzuri kabisa; ni wa kubabaisha sana labda ukiwa unategemea kunufaika kwa majina ya wasanii waliotumika nadhani ukilenga soko la Nigeria. Ni wimbo unaoonyesha kuwa ulichanganywachangwanya harakaharaka bile muelekeo wowote; hausogelei kabisa wimbo wa Nitamata Wapi, ambamo uimbaji wa Diamond unasikikia waziwazi. Hata hivyo ni vizuri pia kuelewa kuwa Diamond leo hii huku kwetu ameshaingia levo kubwa sana ambapo halazimiki tena kutunga muziki mzuri ili atambulike, ila anachohitaji ni kuendelea kuwa relevant tu. Wimbo kama huu pamoja na upungufu wake bado unamfanya awe relevant kuwa aliimba na P-Square. Na hata asipotunga wimbo mpya mwaka mzima ujao badala yake akawa anatoa picha za kuonyesha jinsi anavyokula maisha na mpenzi wake Zari hadi mama huyo atakapojifungua bado atakuwa yuko pale pale aking'ara tu. Kazi kubwa aliyofanya miaka mitano iliyopita sasa inamlipa leo hata asipofanya lolote tena.