Japo Uchaguzi wa 2020 ni Uchaguzi halali, Ushindi wa Kishindo wa CCM ni halali? Wapinzani ni Wameshindwa Kihalali au Wamedhulumiwa kwa Figisu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Kwa maslahi ya taifa, leo naomba kuendesha somo kuhusu kitu kinachoitwa ubatili na haramu.

Ubatili ni kitu ama kilichofanyika kinyume cha sheria, taratibu na kanuni hivyo jambo likifanyika kwa ubatili jambo hilo linakuwa ni batili.

Haramu ni jambo ambalo limefanyika kinyume cha imani na sio lazima iwe ni kinyume cha sheria.

Huu ubatili na uharamu unafanyika katika nyanja nyingi za maisha yetu, kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Sasa ili batili iwe ni batili kweli, lazima batili hiyo ibatilishwe, batili isipobatilishwa inakuwa ni halali!. Vivyo hivyo kwa haramu, ili jambo fulani kuwa ni haramu, lazima haramu hiyo iharimishwe, haramu isipoharimishwa inakuwa ni halali.

Mada kuu ya bandiko hili ni maswali kuhusu uchaguzi mkuu uliopita wa 2020, kuna watu mpaka leo zaidi ya miaka miwili imepita, bado hawataki kukunali matokeo, bado wanaamini uchaguzi ule haukua huru na wa haki hivyo kwao matokeo ya uchaguzi huo sio halali na wengine hata kuuita ulikuwa sio uchaguzi bali ni uchafuzi na matokeo yake ni haramu, hivyo kuendelea kususa hadi leo, hawayatambui matokeo, hawamtambui rais, hawalitambui Bunge hadi kususia nafasi za viti maalum!, hivyo nina viswali kidogo kwako, kuwa japo uchaguzi wa 2020 ni Uchaguzi halali, kwa kanuni ya "the end justifys the means", aliyetangazwa mshindi ndie mshindi halali, jee ushindi wa kishindo wa CCM wa kukomba kila kitu ni ushindi halali au batili na haramu?. Wapinzani ni wameshindwa kihalali kwa kukataliwa na wananchi au ni wameshindwa kwa kudhulumiwa na kufanyiwa Figisu hivyo kushindwa kwao sio halali ni wameshindishwa kwa ubatili na haramu?.

Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili baada ya kusoma hoja hii ya mwana jf huyu
Pascal ana shida sana kuhalalisha haramu kuwa halali.
Mkuu WALOLA VUNZYA kwanza naomba kukiri post yako hii imenimotivate kupandisha bandiko linalojitemea, thanks for motivation.

Ili jambo lolote haramu liwe ni haramu kweli ni lazima liharimishwe, ukifanya jambo la haramu, lisipo harimishwa linakuwa ni halali, yaani kitendo cha kutoiharimisha haramu yoyote, kunakuwa ni kuihalalisha hiyo haramu inakuwa halali mpaka pale yule YEYE anapoingilia kati kwa karma ama kuibatilisha haramu hiyo ama kuiacha na hivyo kuibariki.

Kwa vile issues zs uhalali na uharamu ni issues ngumu kueleweka kirahisi, naomba nifungie darasa kabisa niwapige shule kwa kutoa mifano ila pia kwa vile humu tuna simple readers na deep readers, simple readers hawataki vitu virefu, wanataka vitu short, simple and clear, hawa wanaweza kuishia hapa na ku jump kwenye conclusion, wale ma deep readers, tuendelee.
Conclusion
Vivyo hivyo kwa haramu ya demokrasia na ubakwaji wa demokrasia, ili haramu iwe ni haramu kweli lazima haramu hiyo iharimishwe, haramu isipoharimishwa, na batili isipo batilishwa inageuka halal!.

Swali la kujiuliza kuhusu uchaguzi wa 2020 jee kuna mgombea yoyote aliyelalamika rasmi popote kuhusu uchaguzi huo?. Jibu ni hakuna!. Hivyo kwasababu hakuna mtu yoyote aliyelalamika popote, then kumehalalisha kila kilichofanyika kwa kuitumia ile kanuni ya "the end justifies the means" kwa hoja hizo, na kwa muktadha huo, Uchaguzi wa 2020 ni uchaguzi halali, na sio uchafuzi kama unavyodaiwa na baadhi ya walioshindwa!, CCM imeshinda ushindi wa kishindo kihalali, na wapinzani wamekataliwa na wananchi na kushindwa kihalali!, the winner takes it all!, the looser standing small.

Paskali
 
Paschall kumbuka kuuliza swali ambalo jibu unalo huo unakua ni zaidi ya ujuha au basi tukuulize na wewe kwakua ulikua sehemu ya uchaguzi (mugombea) mbinu alizotumia mwendazake zilikua halali? Kumbuka hata wewe bila kuponzwa na kile kiswali chako Leo ungekua bungeni kama Gwajima.
 
Sijawahi kushuhudia uchaguzi wa kipuuzi na wa hovyo, kama ule wa 2020! Yaani anashinda Juma, tena kwa kura nyingi tu! Halafu kwenye matokeo anatangazwa John! Aliyeshindwa vibaya.

Polisi na watendaji wa kata, haki ya nani mtaishi maisha magumu sana. Na aliyetoa amri ya kutangaza wagombea wa chama tawala pekee, alaaniwe milele!

Ile haikuwa demokrasia hata kidogo. Ule ulikuwa ni uhuni.
 
Hata uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2020 Trumph alidai kufanyiwa rafu, alidi kaibiwa kura na kambi ya Baiden.

Trumph alienda Mahakamani na alibwagwa, lkn hadi leo hajawahi kukubali kushindwa.

Jirani zetu wa kenya Raila alienda mahakamani baada ya kushindwa kwa debe, alibagwa lakini hadi leo hajayakubaali matokeo.

Tatizo la kutokukubali matokeo ya uchaguzi ni tatizo la dunia nzima, iwe imethibitishwa na vyombo vya sheria au la, hata wangeenda Mahakamani bado wasinge kubali.
 
Tukiendelea na katiba hii na Rais kupewa mamlaka za kuteua wasimamizi na waratibu wa uchaguzi watoke kwenye akili na mawazo yake Tanzania kamwe haiwezi kuwa na uchaguzi huru na wahaki. Magufuli alaaniwe huko alipo ametuharibia sana nchi kwa kujaza Wabunge kutoka CCM. 2020 hakukuwa na uchaguzi kulikuwa na uchafuzi. BABU TALE NA MWANA FA eti nao wabunge.
 
Bado mnaishia kulalama tu,mngethibitisha uharamu kwa kuchukua hatua, hivyo inabaki kuwa ule ulikuwa uchaguzi halali na ushindi wa kishindo kwa CCM,nimemuelewa sana ndugu" P ".

2025 mtaishia kulalama hivihivi tena bila kuchukua hatua za kisheria kuharamisha. mpaka siku mshinde nyie ndio utakuwa uchaguzi halali.
 
Unajua maana ya hamna aliyelala popote? Au hayo maelezo yako umeshindwa kuyaweka vizuri? Unasema unasikia watu wanalalamika halafu unasema hakuna aliyelalamika popote! Endelea kuomba watu waendelee na huu uoga, siku uoga ukiisha utaona waliokuwa wanalalamika popote wakijitokeza.
 
Ulitaka hatua gani zichukuliwe kama mchakato wote wa uchaguzi ulivurugwa! Kuionesha tu dunia kuhusu uhuni wote uliotokea, bado nayo ilikuwa ni hatua mojawapo.
 
We jamaa unaandika ujinga tu

ccm 2020 waliiba kura sasa hapo usichofahamu Ni Nini!?
Paskal wewe ni mwanasheria pia? Kama ni hivyo basi tafadhali "Consensus" kwenye andiko lako isomeke "consensual". Kupata majibu ya maswali yako inatakiwa urejee kwenye somo la falsafa. Hili somo, ili uweze kulielewa vizuri unatakiwa uelewe mambo ya msingi kwanza, kwa maana ya kuwa usirukie masuala ya Phd kama uelewa wa shahada za awali hujaumudu. Pengine na kigezo kingine, wale unaowaandikia kama unavyofanya humu ndani, unatakiwa, ama uwafikishe kwenye kiwango chako cha uelewa kama wewe unao uelewa au wao pia wawe wamefikia kiwango hicho kwa juhudi zao . Katika historia ya hivi karibuni, suala kama hili hujadiliwa kwenye kiwango cha juu cha somo la "jurisprudence". Kesi nyingi ambazo hutumika kufafanua mkanganyiko wa masuala unayoyasemea utazipata kwenye kesi za rufaa baada ya utawala wa Hitler kutokomezwa Ujerumani. Mahakama huzo za rufaa zilikuwa zinasikiliza rufaa za wahanga ambao walikutwa na hatia wakawa bado wako hai baada ya Vita Kuu ya Pili. Hawa waliokutwa na hatia wakati wa Hitler, mahakimu ama hawakufuata sheria za wakati wa Hitler au walitumia sheria ambazo hazikuwa halali katika kipimo cha misingi ya utu. Baada Mahakama za rufaa kupitia rufaa hizo na kutoa uamuzi wa rufaa ambao waliona ni sahihi, hizo mahakama zilirudi na kuamua kama mahakimu au majaji waliowatia hatiani hao wahanga ambao wameonekana kuwa hawajuwa na hatia hata wakati wa Hitler, je mahakimu na majaji nao wahukumiwe kwa makosa yao? Mahakama za juu nyingi zilikubaliana kuwa vuguvugu, ushabiki na vitisho ambavyo chama cha Hitler na serikali yake wakati huo vilisababisha mahakimu na majaji kutotenda haki kama nafasi na utulivu waliokuwa nao Mahakama za rufaa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kuisha na Hitler na Chama chake kupigwa marufuku. Mahakama za rufaa zikiona kuwa uwanja, mantiki na haki vilikuwa tofauti kwenye mazingira tofauti. Kwa ushauri wangu, si vema kuwadhakisha watoto wa chekechea majoho ya Phd na kuwaaminisha kuwa wamepata hiyo elimu wakati ndiyo kwanza wanaanza safari ya elimu.
 
wapuuz wa lumumba 2025 jiandaen
 
Kaka Pascal nimekuelewa,kuwa kila mchezo una kanuni za kuingia na kutoka.Uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni ambazo zinaeleza kila hatua ambayo mgombea anapaswa kufuata,kuanzia kuchukua fomu, kuirudisha,kuteuliwa,kugombea,kutangazwa mshindi na hatua za kuchukua endapo hujaridhika na matokeo.Sasa kama mgombea alishiriki kwa kujua kanuni na sheria za mchezo alafu anachagua vipengele vya kutekeleza,asaidiweje?
Naunga mkono hoja kuwa uchaguzi ulikuwa halali,na hauwezi kuwa batili kwa kanuni za nje ya mchezo(lawama) bali utakuwa batili kwa kuwa challenged na kanuni za mchezo husika(mchakato wa sheria za uchaguzi).
 
Wasimamizi na ded anayetangaza matokeo anaambiwa umepewa gari, posho, na mshahara, ikitangaza yeyote asiye Ccm kashinda, unafukuzwa kazi. Analazimika 2020 kutangaza Ccm kashinda hata kama ameshindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…