Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Wapi imesemwa ni mtoto wa pekee wa Ibrahim na Sara?
Mwanzo 22:2

[2]Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
 
Kwa mujibu wa historia Ishmael na mama yake Hajir walikuwa wamekwisha fukuzwa kwenye nyumba ya Ibrahim Kwa maana hy mtoto wa pekee aliyekuwepo ni Isaka
Maandiko yenu yenyewe ndo yanasema Sara alikasirika kwa kuwa alimuona Ismail anamfanyia dhihaka Isaac ndo akaamuru wafukuzwe, sasa historia ipi hiyo inayoenda kinyume na maandiko yenu?
 
Mwanzo 22:2

[2]Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
Sasa anakuaje mwanawe wa pekee wakati yupo mkubwa wake? ... au kiswahili kimebadilika saivi kwamba pekee haimaanishi pekee tunayoijua?
 
Katika Historia ya Ibrahim alimpata Ishamil baada ya kufika Kaanani na si njiani, unakubalina na Hili?

Ibrahim Hadi Leo Waislam na Wakristo wote wanakubaliana kuwa Kaburi lake liko Hebron Israel?

Je unataka kusema Ibrahim alitembea kwenda Saudi Arabia kumtoa Sadaka mtoto wake?
 
Leta reference kukataa islam haitoki kwa Ismail ambaye n mtoto kutoka mgongo wa Ibrahim
 
Nimep Nimependa unavyosema ukweli.
Vitabu vya dini ndio muongozo sahihi wa dini husika.
Mambo ya nani kasema nje ya hivyo vitabu hayana mashiko.
 
Sasa anakuaje mwanawe wa pekee wakati yupo mkubwa wake? ... au kiswahili kimebadilika saivi kwamba pekee haimaanishi pekee tunayoijua?
mtoto wa pekee ni mtoto wa ahadi aliahidiwa na Mungu, baada ya kuona ahadi inachelewa mke wake(Sarah) akamshauri mumewe alale house girl, kwahiyo kwenye ndoa ya Ibrahim na Sara mtoto pekee ni Isaka. Lakini pia Maandiko yanasema Ibrahimu alimpenda Isaka kuliko huyo Ishmail, ndo maana Mungu akamwambia amtoe yule ampendaye
 
Unaongea kinyume na Mafundisho yenu, according to Quran, Ibrahim alimfukuza Hajiri na wakaenda Kusini yeye akabaki na mke wake
 
Je amri ya kumtoa sadaka ilitoka akiwa wote wawili watoto wakiwepo wameshazaliwa?
 
Wewe tubaki kwenye kufanya UCHAWA kwenye siasa. Haya mabo ya dini waachie werevu.

Judaism ni dini ya Wayuda. Yuda ni mtoto wa Yakobo. Hivyo, UKWELI unabaki pale pale kwamba Ibrahimu hakuwa Myahudi.

Ibrahim ni Myahudi kwa dini.
Mwebrania kwa taifa kutoka uhuru wa ukaldayo.

Wewe mwerevu tuambie Dini ya Ibrahim ilikuwa Dini gani? Mungu wake aliitwa nani?
 
Biblia haijaandika hiyo miaka.
Una Uhakika Mkuu? (Soma mwanzo 13:25)
Lets Talk Facts..

Tuanze na Mwanzo 16:15-16

Ibrahim/Abram alikuwa na Miaka 86 Alipomzaa Ishamael..

Baada ya Miaka 13 Mungu alifanya Agano na Abram agano la kwanza La kutahiriwa na kubadilishwa Jina kutoka Abram Kuwa Ibrahimu..

Mwanzo 17


Wakati wa Agano hili na wakati watoto wote wakitahiriwa na watu wote wa Ibrahimu..
Ishmaili alikuwa Mtoto pekee wa Ibrahimu akiwa na miaka 13 na Isaka akiwa bado hajazaliwa..

Ibrahimu alimpenda Sana Ishamael na ndo maana alimuambia Mungu kuwa Anaomba Ambariki Ishmaili..

Hapa chini utapata uone Ombi la Ibrahimu kwa Mungu na ukisoma kwenye aya ya 23 utapata miaka ya Ishamael


Kwahyo Ibrahimu alikuwa na Miaka 100 alipozaliwa Isaka hiyo inamaanisha Kuwa Ishmael alikuwa na Miaka 14

Sasa lini Amri ya Kuchinjwa Ilifanyika.?

Katika Theolojia Wanatheolojia Baadhi wanakubaliana kwamba Ibrahimu alipata Amri ya Kumchinjwa mwanae akiwa na Miaka 100 yaani Ibrahimu akiwa na miaka 100..

Sasa Do the maths Kipindi Ibrahimu akiwa Na miaka 100 Only Son aliyekuwepo Ni Ishmael na Baadae alizaliwa Isaka..
All you have to do ni kutafakari tu na Kuchambua utapata Ukweli
Pascal Mayalla
 
Tatizo kubwa hapa ni ku-mordernize mambo, enzi hizo kulikuwa na house girl? tumia neno sahihi kumuelezea hajra laikuwa ni nani!
 
Wewe tubaki kwenye kufanya UCHAWA kwenye siasa. Haya mabo ya dini waachie werevu.

Judaism ni dini ya Wayuda. Yuda ni mtoto wa Yakobo. Hivyo, UKWELI unabaki pale pale kwamba Ibrahimu hakuwa Myahudi.
Ibrahim hakuwa myahudi wala mkristo bali alikuwa ni muislam aliyejisalimisha kwa mola wake.
 

Hakuna sehemu Ishmael ametajwa kama alitolewa kafara.
Zaidi hapo namwona Isaack.

Tufanye tupo Mahakamani, na Ishmael ndiye alitaka kutolewa kafara,
Unaweza ukaeleza dhabihu hiyo ilifanyika wapi?

Maana kwa Isaka eneo limetajwa.

Embu nukuu Quran ikionyesha eneo hilo ambapo tukio lilitokea.

Mwandishi wa Quran aliandika uongo na niliwahi kueleza hili.
Mwandishi wa Quran hakuwahi kuishi Canaan, Israel au Palestine hivyo ingemuwia vigumu
 
Hebu ifanyie tarjama hiyo aya kwenda kwa kiswahili ili tuone kama aliyetolewa sadaka si Ismael?

Aya ipo wazi imeeleza mtiririko mzima toka ibrahim anapata mtoto wa kwanza kisha mtoto anakua kufika balehe, ibrahim anapata ndoto kuwa amtoe sadaka mwanae, anatekeleza ila Mungu anamlipa kwa kumpa kichinjo, kisha anapewa bishara kuwa atapata mtoto mwingine aitwae ishaq.
 

Tukio hilo linafanyika wapi au kwenye ndoto?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ