Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Wayahudi je wanamchukuliaje Yesu?
 
Pascal, huwezi kutumia masimulizi ya Abel na Cain au Isaac na Ismal kwamba Wakristo na Waislamu wanafuata automatically kwa Abel au Cain au kwa Isaac au Ismal respectively na kuanza ku'establish' dini ipi ni ya kweli kati ya hizo. It doesn't follow that way. Ukifanya hivyo, unakuwa umefany bad 'exegesis'/'hermeneutics' kama ambavyo pia watu wanalazimisha science iwe scienticism wanapolazimisha ku'prove' kuwepo kwa Mungu kwa kutumia science (yaani kutumia science ambayo inatumia experiment ku'prove' Mungu ambaye is beyond experiment/hawi controlled na laws of nature). It is impossible! Within one religion there could be elements of God and non-elements of God at the same time. Chukua Wakristo/Waislamu wawili: one could be for God and the other not. How would you explain that in relation to for example Abel or Cain au Isaac and Ismail? Even within one person there could be those two elements - kuna wakati mtu unaweza kujiona ni uzao wa Abel au Cain, au wa Isaac au Ismail. How would you explain it?
 

Vizuri
 

Hapa Kuna mambo mapya najifunza
 
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّابِرِينَ

(ASS'AFFAT - 102)
Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.

Maswali
1. Hayo makamo ya kwenda na kurudi naye ni makamo gani?

2. Ameota usingizini, kwahiyo ndoto ni kitu cha kuelezea uhalisia wa maisha?

3. Huyo Mwanawe aliye mwotea ndoto ya kumchinja anaitwa nani ?

4. Ameota usingizini kuwa anamchinja, anamchinja sehemu gani?
Ni shingoni, kiunoni au katika govi lake ?

5. Hivi ni kwanini haisemi kuwa aliamuriwa na Mungu wake kuwa ameagizwa kumchinja huyo mtoto wake, anaficha nini ?

6. Nini kiliendelea baada ya hiyo ndoto, alitimiza ndoto yake ya kumchinja huyo Mwanae?

7. Ni kwanini hiyo Aya haina muendelezo wa hiyo ndoto na tukio lililo tokea ?

8. Mama wa huyo mtoto aliitwa nani ?

9. Hilo tukio la ndoto lilitokea wapi ?

10. Mtathibitishaje kuwa hiyo ndoto ilikuwa ni agizo la Mungu wake, wakati yeye mwotaji ndoto hajasema chochote ?

11. Mnaiaminije hiyo Aya wakati haielezi chochote zaidi ya kuota ndoto ya kuchinja kitu kisicho elezewa, alimchinja nani na alichinja nini ?

12. Kwanini mnaamini ndoto na kuyaweka maneno yenu kwenye hiyo ndoto, lengo lenu ni nini hasa ?

Bakini na ndoto zenu.
 
Wayahudi je wanamchukuliaje Yesu?
Uyahudi ni Dini na hawamwamini Yesu Kristo kama Nabii wao.
Bado wanamsubiri Masihi wao.

Ila wanamkubali kama Nabii wa Wakristo ndio maana wameweka Injiri ya Yesu kwenye Biblia yao.

Na pia Filamu za Matendo ya Yesu wao ndio Wana hati miliki nazo.

Na pia wametunza hadi leo kumbukumbu zote za Maisha ya Yesu.

Watalii wanaenda Israeli Hadi leo kushuhudia maeneo na mabaki ya Maisha ya Yesu.

Yesu alikuwa anaabudu pamoja nao katika dini yao ya Uyahudi.
 
🤣🤣🤣🤣🤣
Na Musa aliambiwa Atoe Jando kwa Ng'ombe pia Sio..
QURAN 2:67, QURAN 2:71
Kwahiyo Mkuu hapo Mwanzo ulikuwa Mchungaji wa imani ya Kikristo.

Halafu uka silimu na kuwa Mwislamu.

Halafu uka silimua na kuwa Myahudi

Na sasa hivi umeachana na hizo imani zote.

Hizi ni habari za kushangaza kwa kiasi chake

Ningekuwa wewe nisinge jadili maswala ya imani au dini ambazo niliachana nazo, maana hazina mashiko kwangu.
Ni kama kupoteza muda, kujadili maswala ambayo huyaamini.
 
Hapa unapotosha , chuki Za kidini Kati ya waislamu na Wahindu zilianzishwa na Muingereza . Hiyo dini ya kihindi ilikuwa haitwi hivyo ni wazungu ndiyo walitoa hilo jina. Wala siyo kwamba ni dini moja ni dini nyingi tofauti zinazoamini tofauti
 
Hilo ni darasa kubwa sana la kuielewa Qur'an na lugha iliyotumika, hata Waarabu wengi hawaielewi Qur'an

Nakushauri usiishie dakika kumi tu, sikiliza yote kwa kujifunza mapya. Kuna mengi sana ya kujifunza.
 
Hayapo hayo kwenye Qur'an, nasisitiza niliandika mwanzo huko, mimi natofautiana hata na Waislam wenzangu wengi kwenye hili la Ismail kuwa ni mtoto wa Ibrahim, sijuwi wamelisoma wapi, kwa kusisitiza, hata Sarah hayupo kabisa kwenye Qur'an sijuwi Waislam wamemtowa wapi?

Wewe badala ya kuuliza kuhusu makkah, mji ambao upo siku nyingi sana na inawezekana Ibrahim alipita au kuwepo hapo, kwanza inabidi upanguwe na kuelewa Ismail aliyetajwa kwenye Qur'an ni nani na kwanini ahusishwe na Ibrahim? Kwanini awe mtoto wa Ibrahim wakati Qur'an haina hilo? Sarah ni nani na katokea wapi wakati kwenye Qur'an hajatajwa?
 
Hakuna Mahali nimesema Sijayaamini..
Maisha ni Mwalimu Sana mkuu...
Nilifanikiwa Kupita kote lakini Baada ya kujua vitu vingi amani Inakuwwpo..

Huwa napenda kujadili kwa sababu sipendi watu kupotoshwa na I take it as Second of My hobbies Mkuu..
Kuachana Na kitu haimaanishi hakina Mashiko kwako..inamaanisha hakina ushawishi Enough kukufanya Ukipe Matumaini..

Unafahamu Msemo unaosema..
"How Could I have Faith when there is no Hope"
 
Hapa unapotosha , chuki Za kidini Kati ya waislamu na Wahindu zilianzishwa na Muingereza . Hiyo dini ya kihindi ilikuwa haitwi hivyo ni wazungu ndiyo walitoa hilo jina. Wala siyo kwamba ni dini moja ni dini nyingi tofauti zinazoamini tofauti
Naelewa vizuri..
ILikuwa Ikiitwa Sanatana Dharma..
 
Sheikh hayo yooote ni marudio yaliyotwaliwa kutoka kwenye "KITABU'' na kumbuka hapo inaposemwa kitabu "ni kile walichopewa wale waliokuwepo kabla yenu''

Unafikili mtume alipata njozi moja? Hapana ni nyingi na zile zinazosomwa ndizo zilizojirudia mara kadhaa na ndizo zilizoandikwa kwenye Quran.

Kumbuka Biblia imekuwapo miaka mingi zaidi kuliko Quran
.
 
Huwa napenda kujadili kwa sababu sipendi watu kupotoshwa na I take it as Second of My hobbies Mkuu..
Mkuu DR Mambo Jambo , asante sana kwa michango yako kwenye bandiko hili, wewe na FaizaFoxy mmekuwa ni msaada mkubwa sana kwenye bandiko hili.

Mimi ni muumini muumini wa ukweli, pia sipendi watu wadanganywe, Mungu wa Wakristo na Waislamu ni Mungu mmoja, na sheria kwa dini zote mbili ni sheria moja ya Musa, ila dini zinapotosha sana, na kufanya editing maandiko matakatifu, au kutoa tafsriri potofu to suit their, needs.

Huu mjadala FaizaFoxy aliishaufunga siku nyingi aliposema kwenye Quran Tukufu, hakuna kuchinja binadamu wala Ismail hajatajwa.

Japo mimi ni Mkatoliki die hard, kuna vitu nimevisoma kwenye Bible, we are not doing right!, kuna lots and lots of things tunafanya, sheria ya Musa, ilikataza, wanamsingizia Yesu amekuja kutengua Torati, kitu ambacho sio kweli!.

Japp mimi ndie thread starter, nimejikuta mimi sasa ndio najifunza.
Asanteni wote kwa michango elimishi.

P
 
Andiko lefu Ila hujajibu Hoja u
Unayoongeleea wewe ni Mambo ya baada ya tukio la kichunjwa ,swali hapa nani alipaswa kuchinjwa Kama sadaka aakiwa ni mwana wa pekee wa Ibrahim
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…