Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Ni hiari yako kusikiliza chanzo cha habari au masimulizi mengine ya baadae.

Biblia iliyoanza kuripoti hilo tukio inasema Isaka ndiye aliyetolewa sadaka.

Waislamu wapambane na dini yao ambayo ina aya za mkato mkato na hazina mtiririko wa matukio.

Waislamu na qurani yao wameambiwa ishamaeli ndiye aliyetolewa sadaka wala hupaswi kuuliza.

Mungu wa kwenye Biblia alisha sema mara nyingi tu kuwa yeye ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambaye ndiye Israeli.

Na ametoa family tree ya mtiririko wa Manabii na watu aliowatumia katika mpango wake wa kumwabudu, na Ishamael hayupo kwenye hiyo family.

Achana na stori za kuunga unga, familia ya Wayahudi ni hii hapa.
Mathayo 1
2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;

3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;

4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;

5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;

6 Yese akamzaa mfalme Daudi; Daudi akamzaa Suleimani kwa yule mke wa uria;

7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;

8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;

9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;

10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;

11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.

12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;

13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;

14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;

15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;

16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
..............
Na nyie mnao mwona Ishmaeli kama ndio baba wa Uislamu naomba mnipe family tree yake hadi kuzaliwa Muhammadi.
Maana Mungu anatunza kumbukumbu za Manabii wake hadi wa mwisho.

Maswali mengine hayana mantiki, kweli ya mtu ni ile anayoiamini.

Kweli ya Wayahudi na Wakristo ni Isaka.

Kweli ya Waislamu ni Ishmaeli ambaye hawajui hata family tree yake.

Kila mtu ana kweli yake kutikana na kukiamini chanzo cha hiyo kweli.

Wayahudi na Wakristo tunamchukulia Muhammadi kama mtu mpotoshaji tu na kamwe hatumwamini kwa chochote anacho ongea
Wayahudi je wanamchukuliaje Yesu?
 
Wanabodi,
Leo ni sikukuu ya Eid El Haji, Iddi ya Kuchinja.

Leo ni siku ya Sikukuu ya Idd El Haj, ni iddi ya kuchinja, asubuhi nilikuwa naangalia matangazo ya mubashara ya Baraza la Iddi kupitia TBC, kutoka Msikiti wa Mfalme Mohammed VI wa Morroco, Bwakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, kumbe Msikiti Mkuu wa Bakwata, sasa umebadilishwa jina!, na kupewa jina la Mfalme wa Morroco!.

Mgeni rasmi kwenye Baraza la Iddi ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, ambaye ameandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ambaye amesilimishwa na kupewa jina la Aboubakar Chalamila!, na mawaziri akiwemo Waziri Mhe. Mohamed Mchengerwa. Baadhi ya watu maarufu niliowaona ni pamoja na Alhaj Sheikh Ali Nguruko, Alhaj Chande, Idda Azan, Shaweji Abdalah, Salum Mwalimu, Juma Simba Gadafi, Salum Abladaha "TRY Again", Katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mruma, Kadhi wa Dar es Salaam, Shamin Khan, mwenyekiti wa JUAKITA, pia kulikuwa na mabalozi wa Balozi wa Moroko, na wa Comoro.

Katika salam zake, Sheikh Aboubakar Chalamila alisema utulivu wa jiji la Dar es Salaam, unawategemea sana viongozi wa Dini.

Salaam za Waislamu, zimetolewa na Alhaj Sheikh Nuru Mruma, Katibu Mkuu wa Bakwata ambaye amewasisitiza Waislamu kudumisha amani na kuilinda amani. Wazazi watakiwa kulea watoto wao kwa tabia njema, kujenga taifa la kizazi cha watu wema ambao hawatapokea rushwa wala kufanya ufisadi.

Amesema kupanda miti na utunzaji wa mazingira ni ibada muhimu kwa Waismamu wote.

Pia amewataka Waislamu kujitokeza kwa wingi, kujiandikisha kwenye uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.
na wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kidemokrasia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Salaam za Mufti, zimetolewa na Kaimu Mufti Sheikh Ali Muhidin Mporogore, Mjumbe wa Baraza la Maulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Bwakwata. Aamezungumzia Watanzania tutafakari, sadaka ya kuchinja siku ya Iddi El Haj, ni iddi ya kuchinja. Zamani ilikuwa sio kuchinja tuu wanyama, bali walichinja hata binadamu ana akatolea mfano Sadaka ya Nabii Ibrahim kutaka kumtoa mwanae Ismail, kwa sadaka ya kuchinja.

Hakuna ubishi kuhusu Wakristo na Waislamu, kuwa ni watoto wa Baba mmoja, Nabii Ibrahim hivyo huu ni uthibitisho wa Mungu wa Wakristo na Waislamu ni Mungu Mmoja, na sheria za dini hizi zote mbili Wakristu na Waislamu, ni sheria moja ile ile ya Musa, ila kuna watu wanafundishwa ukweli na kuna watu wanadanganywa!.

Hakuna ubishi kuwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail aliyezaa na mjakazi wa Kimisri, Hagir, na Isaka ni mtoto wa pili wa Ibrahim, aliyemzaa na mkewe Sarah.

Hakuna ubishi Ibrahim alitaka kumtoa mtoto wake Sadaka ya kuchinja.

Waislamu na Kitabu chao Kitukufu cha Quran Tukufu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Ismail.
Wakristo na Kitabu chao Kitakatifu cha Biblia Takatifu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Isaka.

Jee ukweli halisi ni upi?.
Hii maana yake
Kama tukio la Ibrahim kutaka kumchinja mwanae kumtoa sadaka ni tukio moja, then
1. Hii maana yake ni kuna watu wanadanganywa, haiwezekani kwa Waislamu mtoto huyo awe ni Ismail na kwa Wakristu mtoto huyo awe ni Isaka, hii maana yake kuna kitabu hapo kinasema kweli na kuna kitabu kinasema uongo!, jee ukweli ni upi?.

Umuhimu wa kuujua ukweli huu, unakupa fursa ya kujua ukweli ni upi, hivyo ufuate mafundisho yapi ambayo ndio mafundisho ya kweli!.

Bandiko hili linakutaka kwanza uwe open minded, kama wewe ni mfia dini, unaamini dini yako ni ya ukweli mtupu, bandiko hili halikufai.

Pili unatakiwa uwe na ngozi ngumu ya kuukubali ukweli halisi hata uwe mchungu vipi!, ikitokea ni dini yako unayoiamini kuwa ni dini ya kweli, kumbe ni dini ya uongo, uwe na uwezo wa kustahimili maana...

Nawatakia Waislamu wote,
Iddi Mubarak njema ya kuchinja.

Paskal
Pascal, huwezi kutumia masimulizi ya Abel na Cain au Isaac na Ismal kwamba Wakristo na Waislamu wanafuata automatically kwa Abel au Cain au kwa Isaac au Ismal respectively na kuanza ku'establish' dini ipi ni ya kweli kati ya hizo. It doesn't follow that way. Ukifanya hivyo, unakuwa umefany bad 'exegesis'/'hermeneutics' kama ambavyo pia watu wanalazimisha science iwe scienticism wanapolazimisha ku'prove' kuwepo kwa Mungu kwa kutumia science (yaani kutumia science ambayo inatumia experiment ku'prove' Mungu ambaye is beyond experiment/hawi controlled na laws of nature). It is impossible! Within one religion there could be elements of God and non-elements of God at the same time. Chukua Wakristo/Waislamu wawili: one could be for God and the other not. How would you explain that in relation to for example Abel or Cain au Isaac and Ismail? Even within one person there could be those two elements - kuna wakati mtu unaweza kujiona ni uzao wa Abel au Cain, au wa Isaac au Ismail. How would you explain it?
 
Hakuna kwenye Qur'an. ni porojo za watafsiri tu.

Mwenyezi Mungu atake kafara ya nini kwetu na yeye ni Muumba wa kila kitu?

Ukiona kuna "kafara" kwenye Qur'an basi chimba hapo utakuta hilo ni somo na zuio kwetu kwa watu ambao wanatoa kafara au walikuwa wanatowa kafara, Muumba wetu hahitaji kafara.

Vizuri
 
Achana naye huyo..
Kama hakuna Tukio la kafara then Dini ya Kiislam why Wanafanya Hija??
Kwahyo Nguzo ya Dini ya Kiislmu moja wapo Imekufa..

Na kingine Muulize kwanini Mtume alikuwa Anachinja na alikuwa anachinja nini..
Hadithi/Sunna za Mtume zinaelekeza wao.kuchinja kwanini?

Hapa Kuna mambo mapya najifunza
 
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّابِرِينَ

(ASS'AFFAT - 102)
Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.

Maswali
1. Hayo makamo ya kwenda na kurudi naye ni makamo gani?

2. Ameota usingizini, kwahiyo ndoto ni kitu cha kuelezea uhalisia wa maisha?

3. Huyo Mwanawe aliye mwotea ndoto ya kumchinja anaitwa nani ?

4. Ameota usingizini kuwa anamchinja, anamchinja sehemu gani?
Ni shingoni, kiunoni au katika govi lake ?

5. Hivi ni kwanini haisemi kuwa aliamuriwa na Mungu wake kuwa ameagizwa kumchinja huyo mtoto wake, anaficha nini ?

6. Nini kiliendelea baada ya hiyo ndoto, alitimiza ndoto yake ya kumchinja huyo Mwanae?

7. Ni kwanini hiyo Aya haina muendelezo wa hiyo ndoto na tukio lililo tokea ?

8. Mama wa huyo mtoto aliitwa nani ?

9. Hilo tukio la ndoto lilitokea wapi ?

10. Mtathibitishaje kuwa hiyo ndoto ilikuwa ni agizo la Mungu wake, wakati yeye mwotaji ndoto hajasema chochote ?

11. Mnaiaminije hiyo Aya wakati haielezi chochote zaidi ya kuota ndoto ya kuchinja kitu kisicho elezewa, alimchinja nani na alichinja nini ?

12. Kwanini mnaamini ndoto na kuyaweka maneno yenu kwenye hiyo ndoto, lengo lenu ni nini hasa ?

Bakini na ndoto zenu.
 
Wayahudi je wanamchukuliaje Yesu?
Uyahudi ni Dini na hawamwamini Yesu Kristo kama Nabii wao.
Bado wanamsubiri Masihi wao.

Ila wanamkubali kama Nabii wa Wakristo ndio maana wameweka Injiri ya Yesu kwenye Biblia yao.

Na pia Filamu za Matendo ya Yesu wao ndio Wana hati miliki nazo.

Na pia wametunza hadi leo kumbukumbu zote za Maisha ya Yesu.

Watalii wanaenda Israeli Hadi leo kushuhudia maeneo na mabaki ya Maisha ya Yesu.

Yesu alikuwa anaabudu pamoja nao katika dini yao ya Uyahudi.
 
🤣🤣🤣🤣🤣
Na Musa aliambiwa Atoe Jando kwa Ng'ombe pia Sio..
QURAN 2:67, QURAN 2:71
Kwahiyo Mkuu hapo Mwanzo ulikuwa Mchungaji wa imani ya Kikristo.

Halafu uka silimu na kuwa Mwislamu.

Halafu uka silimua na kuwa Myahudi

Na sasa hivi umeachana na hizo imani zote.

Hizi ni habari za kushangaza kwa kiasi chake

Ningekuwa wewe nisinge jadili maswala ya imani au dini ambazo niliachana nazo, maana hazina mashiko kwangu.
Ni kama kupoteza muda, kujadili maswala ambayo huyaamini.
 
India kugombana na Waislam ni Matokeo yale niliyoyasema tangu Zamani ya Chuki za Kidini..
Waislam wanaamini kuwa Wana Mamlaka ya kuzuia watu wote Duniani kuabudi vingine isipokuwa Allah..

Na wanaaamini kwambwa wanaweza kutoa Adhabu kwa watu hao..

Hilo jambola vita kati yao halijaanza leo lilianza mara baada tu ya kuanza kwa dini ya Kiislmu..

Unajua Hinduism imeanza zamani kuliko.waislmu then why Hakukuwa na machafuko kabla??
Hapa unapotosha , chuki Za kidini Kati ya waislamu na Wahindu zilianzishwa na Muingereza . Hiyo dini ya kihindi ilikuwa haitwi hivyo ni wazungu ndiyo walitoa hilo jina. Wala siyo kwamba ni dini moja ni dini nyingi tofauti zinazoamini tofauti
 
Aisee Hivi Vitu Vipya Sana Elimu yangu ya Quran na Elimu ya Lugha ya Arabs sijawahi kukutana na hiki kitu nahisi Kila siku najifunza Shukrani sana..

Ila nina maswali yanayokuja kichwani kwangu..
Nimesikiliza mpaka dakika ya 10..
  • Hili ni dhehebu Gani??
  • Kama ndyo maana Yake, Vipi Kuhsu Hijja na al Adha nazo ni Batili
  • Vipi kuhusu Kaaba (Maana inasemekana Ilijengwa na Ismaili na Ni kipindi ameenda kuchinjwa
  • Vipi kuhusu Nguzo ya Hija (miongoni mwa nguzo za waislamu
Yo've Enlight me ngoja nichunguze zaidi japo hapa naendelea kuangalia Video Inazidi kunishangaza vingi
Hilo ni darasa kubwa sana la kuielewa Qur'an na lugha iliyotumika, hata Waarabu wengi hawaielewi Qur'an

Nakushauri usiishie dakika kumi tu, sikiliza yote kwa kujifunza mapya. Kuna mengi sana ya kujifunza.
 
Naelewa Vizuri ila Kama Nimekunote mwanzoni Ulizungumza kuwa Ismaili sio mtoto wa ibrahimu..
So nimeconnect Dot..

Utanisamehe kama nilikuquote vbaya..
Kama ismaili sio mtoto wa Ibrahimu Na Kaaba ilijengwa na Ibrahimu na mwanaye ismaili then Kama ni uongo them means hivy9 vitu havikuwahi kuexists..
Najua kuhusu Hija pia
Hayapo hayo kwenye Qur'an, nasisitiza niliandika mwanzo huko, mimi natofautiana hata na Waislam wenzangu wengi kwenye hili la Ismail kuwa ni mtoto wa Ibrahim, sijuwi wamelisoma wapi, kwa kusisitiza, hata Sarah hayupo kabisa kwenye Qur'an sijuwi Waislam wamemtowa wapi?

Wewe badala ya kuuliza kuhusu makkah, mji ambao upo siku nyingi sana na inawezekana Ibrahim alipita au kuwepo hapo, kwanza inabidi upanguwe na kuelewa Ismail aliyetajwa kwenye Qur'an ni nani na kwanini ahusishwe na Ibrahim? Kwanini awe mtoto wa Ibrahim wakati Qur'an haina hilo? Sarah ni nani na katokea wapi wakati kwenye Qur'an hajatajwa?
 
Kwahiyo Mkuu hapo Mwanzo ulikuwa Mchungaji wa imani ya Kikristo.

Halafu uka silimu na kuwa Mwislamu.

Halafu uka silimua na kuwa Myahudi

Na sasa hivi umeachana na hizo imani zote.

Hizi ni habari za kushangaza kwa kiasi chake

Ningekuwa wewe nisinge jadili maswala ya imani au dini ambazo niliachana nazo, maana hazina mashiko kwangu.
Ni kama kupoteza muda, kujadili maswala ambayo huyaamini.
Hakuna Mahali nimesema Sijayaamini..
Maisha ni Mwalimu Sana mkuu...
Nilifanikiwa Kupita kote lakini Baada ya kujua vitu vingi amani Inakuwwpo..

Huwa napenda kujadili kwa sababu sipendi watu kupotoshwa na I take it as Second of My hobbies Mkuu..
Kuachana Na kitu haimaanishi hakina Mashiko kwako..inamaanisha hakina ushawishi Enough kukufanya Ukipe Matumaini..

Unafahamu Msemo unaosema..
"How Could I have Faith when there is no Hope"
 
Hapa unapotosha , chuki Za kidini Kati ya waislamu na Wahindu zilianzishwa na Muingereza . Hiyo dini ya kihindi ilikuwa haitwi hivyo ni wazungu ndiyo walitoa hilo jina. Wala siyo kwamba ni dini moja ni dini nyingi tofauti zinazoamini tofauti
Naelewa vizuri..
ILikuwa Ikiitwa Sanatana Dharma..
 
Achana na hizo mambo ndugu
Zilikuwa Ndoto tu. Na hajatajwa Ismaili hapo.
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّهُ مِنَ الصَّابِرِينَ

(ASS'AFFAT - 102)
Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.

Hicho kitabu hakipo serious hata kidogo.
Sheikh hayo yooote ni marudio yaliyotwaliwa kutoka kwenye "KITABU'' na kumbuka hapo inaposemwa kitabu "ni kile walichopewa wale waliokuwepo kabla yenu''

Unafikili mtume alipata njozi moja? Hapana ni nyingi na zile zinazosomwa ndizo zilizojirudia mara kadhaa na ndizo zilizoandikwa kwenye Quran.

Kumbuka Biblia imekuwapo miaka mingi zaidi kuliko Quran
.
 
Huwa napenda kujadili kwa sababu sipendi watu kupotoshwa na I take it as Second of My hobbies Mkuu..
Mkuu DR Mambo Jambo , asante sana kwa michango yako kwenye bandiko hili, wewe na FaizaFoxy mmekuwa ni msaada mkubwa sana kwenye bandiko hili.

Mimi ni muumini muumini wa ukweli, pia sipendi watu wadanganywe, Mungu wa Wakristo na Waislamu ni Mungu mmoja, na sheria kwa dini zote mbili ni sheria moja ya Musa, ila dini zinapotosha sana, na kufanya editing maandiko matakatifu, au kutoa tafsriri potofu to suit their, needs.

Huu mjadala FaizaFoxy aliishaufunga siku nyingi aliposema kwenye Quran Tukufu, hakuna kuchinja binadamu wala Ismail hajatajwa.

Japo mimi ni Mkatoliki die hard, kuna vitu nimevisoma kwenye Bible, we are not doing right!, kuna lots and lots of things tunafanya, sheria ya Musa, ilikataza, wanamsingizia Yesu amekuja kutengua Torati, kitu ambacho sio kweli!.

Japp mimi ndie thread starter, nimejikuta mimi sasa ndio najifunza.
Asanteni wote kwa michango elimishi.

P
 
Hasha, nisije nyimwa uzima wa milele Kwa hilo. Biblia imeelezea aliyetakiwa kuchinjwa. Haijaacha kitu lakini bado unabisha. Pia Mungu hapendi tubishane kumhusu. Anapenda tumuulize tukiwa na chochote. Hachoki kutusikiliza lakini kabla ya kumuendea lazima tumuamini.
Tukishaamini lazima tujue Kuna sadaka inapaswa kulipia kosa la wazazi wetu. Wao walitolewa mnyama akachinjwa ili wavishwe. Lakini aliahidi kuleta upatanisho maana Damu ya kondoo na mafahali haikutosha kufuta kosa bali ililifunika tu.
Torati yaeleza yote kuhusu siku iliyo ya upatanisho. Lakini tukitaka kwenda kwenye hekalu lake mbinguni je, hatuhitaji sadaka iliyo Bora kuliko Damu ya fahali na ngombe mnono? Akitaka aweza kujichukulia sadaka za wanyama wote ili ajiridhishe lakini hafanyi maana vyote japo vipo mikononi mwake si kitu kama mwanadamu aliyemuumba akampa pumzi yake ya uhai. Tuna thamani kuu machoni pake na ili atupatanishe naye alitoa sadaka ya kondoo kutoka mbinguni.
Sadaka ya Ibrahim aliyotoa badala ya mwanae kipenzi ilitoka wapi? Kuna mtu kauliza je, Mungu aliiba yule kondoo? Alimnunua? Kuna kitu ndani ya hiyo sadaka. Ilitoka Kwa Mungu Kwa ajili ya Mungu. Vivyo hivyo na Daudi alipotenda dhambi ya kuwahesabu Wana wa Israel aliambiwa akatoe sadaka juu ya madhabahu ambayo Baba yake Ibrahimu alijenga juu ya mlima Moria. Alipotenda Kwa Arauna Myebusi aligoma kutoa sadaka asiyoigharamikia.
Je Mungu Mtakatifu atajitolea sadaka iliyo duni? Au ataiba kondoo ili ampe Ibrahim? Ukijibu hayo mabishano yote yataisha.
Andiko lefu Ila hujajibu Hoja u
Unayoongeleea wewe ni Mambo ya baada ya tukio la kichunjwa ,swali hapa nani alipaswa kuchinjwa Kama sadaka aakiwa ni mwana wa pekee wa Ibrahim
 
Back
Top Bottom