Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Katika dini zote mbili, Ukristo na Uislamu, imani kuhusu mtoto aliyetakiwa kutolewa sadaka na Nabii Ibrahim kama ishara ya utiifu kwa Mungu hutofautiana.

Katika Uislamu:

Waislamu wanaamini mtoto aliyetakiwa kutolewa sadaka alikuwa Ismail, mtoto wa Ibrahim na mjakazi wake Hajar.

Quran Tukufu inasimulia tukio hili katika Sura 37: 100-107, ikionyesha nia ya Ibrahim kumtoa mwanawe Ismail kama sadaka na kuingiliwa kwa Mungu kwa kumpa kondoo kuchukua nafasi ya Ismail.

Tukio hili linaonekana kama mfano wa utiifu wa hali ya juu kwa Mungu na imani thabiti.

Katika Ukristo:

Wakristo wanaamini mtoto aliyetakiwa kutolewa sadaka alikuwa Isaka, mtoto wa Ibrahim na mkewe Sara.

Biblia Takatifu inasimulia tukio hili katika Mwanzo 22: 1-18, ikionyesha nia ya Ibrahim kumtoa mwanawe Isaka kama sadaka na kuingiliwa kwa Mungu kwa kumpa kondoo kuchukua nafasi ya Isaka.

Japo hadithi ni moja ila napingana kwamba Mungu wa wakristo na Waislamu ni mmoja.

Nawasilisha mkuu
 
Sheria ya zamani kijakazi akikuzalia ni mtoto wako huyo. Haitwi mtoto wa nje.
 
Sheria ya zamani kijakazi akikuzalia ni mtoto wako huyo. Haitwi mtoto wa nje.
Sheria zote hizo wamezileta wao. Bado hata hiyo dini mtoto wa mwanamke ni wa mwanamke. Haiwezekani uamini tu kitu ambacho hakijatoka kwenye Roho. Sisi ni mfano wa visivyoonekana. Mifumo yetu hatujaianzisha sisi. Ilikuwepo siku Mungu ameweka misingi ya ulimwengu.
 
Nadhani kwa sababu ukweli upo na kuna wengine wanadanganywa hebu (ukweli uwekwe hapa kimaandiko) tuache porojo za fulani au encyclopedia kasema, kaandika.

Ukweli upo ki_evidence siyo kifikra.

Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.

Ukweli gani utakao upata hapo?
 
Ni hiari yako kusikiliza chanzo cha habari au masimulizi mengine ya baadae.

Biblia iliyoanza kuripoti hilo tukio inasema Isaka ndiye aliyetolewa sadaka.

Waislamu wapambane na dini yao ambayo ina aya za mkato mkato na hazina mtiririko wa matukio.

Waislamu na qurani yao wameambiwa ishamaeli ndiye aliyetolewa sadaka wala hupaswi kuuliza.

Mungu wa kwenye Biblia alisha sema mara nyingi tu kuwa yeye ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambaye ndiye Israeli.

Na ametoa family tree ya mtiririko wa Manabii na watu aliowatumia katika mpango wake wa kumwabudu, na Ishamael hayupo kwenye hiyo family.

Achana na stori za kuunga unga, familia ya Wayahudi ni hii hapa.
Mathayo 1
2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;

3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;

4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;

5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;

6 Yese akamzaa mfalme Daudi; Daudi akamzaa Suleimani kwa yule mke wa uria;

7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;

8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;

9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;

10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;

11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.

12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;

13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;

14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;

15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;

16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
..............
Na nyie mnao mwona Ishmaeli kama ndio baba wa Uislamu naomba mnipe family tree yake hadi kuzaliwa Muhammadi.
Maana Mungu anatunza kumbukumbu za Manabii wake hadi wa mwisho.

Maswali mengine hayana mantiki, kweli ya mtu ni ile anayoiamini.

Kweli ya Wayahudi na Wakristo ni Isaka.

Kweli ya Waislamu ni Ishmaeli ambaye hawajui hata family tree yake.

Kila mtu ana kweli yake kutikana na kukiamini chanzo cha hiyo kweli.

Wayahudi na Wakristo tunamchukulia Muhammadi kama mtu mpotoshaji tu na kamwe hatumwamini kwa chochote anacho ongea
 
Kwa akili hizi ndio maana ukakaririshwa kuna mungu watatu na sasa najua kwanini wayahudi wanauchukia kristo
 
Una ushahidi wowote zaidi ya kukaririshwa? Mimi ni mkristo, illa sina haki ya kujiona ndio mwenye imani sahihi maana wote hizi imani
tumezikuta hapa duniani na hakuna mwenye ushahidi zaidi ya kutakiwa kuamini tu.
 
Una ushahidi wowote zaidi ya kukaririshwa? Mimi ni mkristo, illa sina haki ya kujiona ndio mwenye imani sahihi maana wote hizi imani
tumezikuta hapa duniani na hakuna mwenye ushahidi zaidi ya kutakiwa kuamini tu.
Ushahidi kuhusu nini ?
Naona upo hewani tu.
Sema hiyo nadharia.

Muhamadi anasema yeye ana dini yake na sisi tuna dini yetu.
Haabudu tunacho abudu wala hatuta abudu, anacho abudu yeye, sasa unataka mimi nimbishie?

Wewe ni Mkristo jina.
Biblia inasema Isaka ndiye aliyetolewa sadaka, kabla ya Muhamadi kuzaliwa na kabla ya Uislamu kuwepo.
Anakuja Muhammadi anasema aliyetolewa sadaka ni Ishmaeli.

Wewe na Ukristo wako utamwamini nani?
Mkristo Jina.
Manabii wa kwenye biblia wote wanakubaliana katika hoja zao.
Muhamadi ni nani hadi yeye tu ampinge Nabii Musa, Isaya, Yeremia, Yesu Kristo nk.
Yaani tusiwaamini manabii wote wa kwenye Bibli wanaokubaliana katika hoja moja.
Na tubaki tumwamini yeye tu.
Wayahudi na Wakristo tunamchukulia Muhammadi kuwa ni tapeli kama Mfalme Zumaridi wa Mwanza.
Huu ndio ukweli wetu.
 
HIZI NI HINTS ZA KUZINGATIA...

TUKIO LA KUCHINJA MTOTO IBRAHIM ALIAMRISHWA ALIKUWA NA WATOTO WANGAPI..?

JIBU BILA SHAKA NI JARIBU ALILOPEWA IBRAHIM NA MUNGU WAKE...KUMCHINJA MWANAE WA PEKEE...

NA TUNAJUA WAZI KUWA IBRAHIIM NA MKEWE SARA HAWAKUFANIKIWA KUPATA MTOTO MPAKA UZEENI... KUTOKANA NA HILO SARA AKAMUOMBA IBRAHIM ALALE NA KIJAKAZI WAKE HAJRA...NDIPO AKAPATA MTOTO WAKE WA KWANZA NA WA PEKEE AITWAYE ISMAAIIL...NA KUPITIA MTOTO HUYO MUNGU AKAMJARIBU IBRAHIM IMANI YAKE...NA JARIBU LA KWANZA KUWAHAMISHIA MTOTO NA MAMA YAKE JANGWANI...ALILIFANYA BILA KUJALI... AMRI YA PILI NI KUCHINJA...NA ALITEKELEZA AGIZO...ILA MUNGU AKAMUOKOA NA AKAMBADILISHIA MNYAMA...

KWA KUFAULU HUKO MITIHANI YAKE...MUNGU AKAMBARIKI NA KUMPATIA MTOTO MKE WAKE SARAH JAPO KATIKA HALI YA UZEE...NA MTOTO HUYO AKAWA ANAITWA IS-HAAQA...

HAPO IBRAAHIM AKAWA NA WATOTO WAWILI...NA WOTE WALIPEWA UNABII NA WAKABARIKIWA KIZAZI CHAO KUWA NA MANABII ..KAMA IFUATAVYO:-

1. ISMAAIYL - Katika kizazi chake mwishoni alipqtikana NABII NA MTUME MUHAMMAD ﷺ

2. IS-HAAQA - AKAPATA MTOTO AITWATE YAAQUUB AKAWA MTUME...NA YAAQUUB AKAZAA MTOTO YUUSUF(AKAWA NABII) NA NDUGU ZAKE 11 AMBAO NDIO WALIPELEKEA KUPATIKANA KIZAZI CHA WANA WA ISRAAIIL...
 
Kwanza waislamu watambue kwamba Ismail hakuwa ni ile ahadi akiyopewa Ibrahim na Mungu Mwenyezi- Ibrahim alizini baada ya kuona ahadi na Mungu inazidi kuchelewa na umri wa mkewe sarah umekwenda.

Mungu hakupendezwa na kitendo cha Ibrahim na ndipo alipomwagiza amuondoe nyumbani Ismail pamoja na mama yake.

Na ndiyo maana ukoo wa Ismail haupo kwa vitabu vitakatifu, ingawa ni kweli aliondoka na baraka za Ibrahim ila alikuwa mtoto wa zinaa.
 
Sidhani kama umeelewa hilo andiko!.
Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.

Ukweli gani utakao upata hapo?
 
We una akili sana maana unaangalia ndani ya boksi na nje ya boksi

Hata Yesu alisema haki zenu zipozidi haki za wandishi na mafatisayo hamtaingia kamwe katika ufarume wa mbinguni

Kama wewe ni mgalatia mda si mrefu utaujua ukweli
 
NABII MKUBWA WA MUNGU BABA WA IMANI HAWEZI ZINI...KAMA HUJUI SEMA UFAHAMISHWE...

KATIKA ZA UTUMWA...MTUMWA WA KIKE NI HALALI YA MWANAUME ANAYEMMILIKI TENA BILA NDOA...HIYO HUKMU ITASIMAMA HIVYO MPAKA MWISHO...MRADI UTUMWA TU UKIWEPO...

NDIO MAANA SULAIMAAN ALIKUWA NA VIJAKAZI WENGI NA AKAWAENDEA APENDAVYO...KWA SABABU SHERIA ILIMRUHUSU...TOFAUTI NA NYIE MNAOSINGIZIA MANABII WA MUNGU WATUKUFU UZINIFU...

ALLAAH ALIWATAKASA MANABII WAKE KUTOKANA NA UCHAFU KAMA HUO...

NB:-
Mtumwa - ni mtu anayepatikana kwa njia ya mateka wa vita...na unaweza kumnunua na kumuuza na kumtoa zawadi...na mwanamke mtumwa anaingiliwa na bwana wake bila ndoa...ni halali.

Ndio maana ilikuwa ni ngumu sana kuachia huru mtumwa...kwa sababu ulimpata kwa tabu...yaani ingekuwa sio wewe kushinda vita...ni wewe ndiye ungekuwa mtumwa.
 
Umeandika maelezo mengi hakuna chochote Cha maana zaidi ya Uongo mnao danganyana Kanisani

Kwa kuwa wewe ni mbumbu ngoja nikufundishe Ishmael ni nani

Mungu anamuahidi Ibrahim mtoto atakaye mrithi atatoka katika viuno vyake

Mwanzo 15:3
Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
Mwanzo 15:4
Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.

Ibrahim anamuingilia Hajiri na Hajiri anapata mimba na hatimaye Ibrahim anapata mrithi wake naye ni Ishmael

Mwanzo 16:2
Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
Mwanzo 16:4
Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.

Sasa wewe Ili usiwe mbumbu na msukule wa Wazungu toa andiko linalothibisha kuwa Isaka ametokana na viuno vya Ibrahim

Na ukitoa hilo andiko nakuwa mkristo Leo leo
 
Ibrahim hajawahi kuzini. Mnapata wapi hayo mafundisho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…