Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Mwanzo 21:8-21

[8]Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.

[9]Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.

[10]Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.

[11]Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe.

[12]Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.

[13]Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.

[14]Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.

[15]Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.

[16]Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.

[17]Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.

[18]Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.

[19]Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.

[20]Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.

[21]Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
 
Ikiwa tutaegemea kwenye maandiko tu tukubaliane kutokukubaliana kwa kuwa kila imani imendika kikiwa kinatofautiana na kingine. Tunachopaswa ni kujadili content ya kilichoandikwa hapo ndo tutaelewa kipi kinasema ukweli na kipi ndani yake ukweli umepindishwa.

Kauli ya kusema mtoto wa pekee, Isaac ... hii unai-reconcile vipi na fact ya kuwa Isaac ni mtoto wa pili baada ya kuwa Ibrahim tayari alishakuwa na mtoto mwengine Ismail?
 
mtoto wa pekee kwenye ndoa ya Ibrahimu na Sarah, Maana baada ya Sara kufa Ibrahim alioa mwanamke mwingine naye akamzalia watoto wengine
 
Na Isaka ndiye mtoto wa Agano kwa watoto wote wa Ibrahimu
 
MUNGU WA WAKRISTO NA WA WAISLAMU NI MIUNGU MIWILI TOFAUTI KABISA. HAWAFANANI HATA KIDOGO. SIFA ZAO NI TOFAUTI NA HATA MBINGU ZAO NI TOFAUTI.
 
Mimi nina swali kwako Che Mittoga !

Kipindi Isaka anazaliwa Ishamael alikuwa na miaka mingapi?
Biblia haijaandika hiyo miaka.

Mimi nimeomba andiko linalo mtaja kwa jina Ismaeli kutolewa sadaka maana sijawahi kuliona popote.
Na nimeweka andiko la Mwanzo 22: likimtaja Isaka.
Kutokana na Biblia.
Ismaeli aliondoka nyumbani kwa Ibrahimu katika Mwanzo 21: kabla ya Mungu kumjaribu Ibrahimu amtoe sadaka Isaka.
Ina maana Ibrahimu aliambiwa hivyo wakati Ismaeli kesha ondoka na mama yake Hajiri kwa Ibrahimu.

Hivyo lingewekwa kwanza hilo andiko linalo mtaja Ismaeli kwa jina lake kutolewa sadaka ndio tuendelee kujadili hii mada.
La sivyo haitakuwa na mantiki.

Katika visa vya Biblia mtoto wa kwanza mala nyingi tu tunasoma anakosa urithi anaostahili.
Esau alikosa baraka kama mtoto wa kwanza na akapewa Yakobo mdogo wake, Nk.
 

Iweke hiyo aya hapa.
Ushahidi unaletwa mahakamani na sio mahakama kuufuata
 
What a contradiction! ... yani katika same story line Mungu awe upande wa Sara kutaka kumnyima urithi Ismail na kubariki kuwa afukuzwe yeye na mama yake lakini huko walikopotelewa akawatendee miujiza ya kuwaletea kisima cha maji palipokuwa hakuna maji ili kumuokoa huyo mtoto.

Something doesn't add up to this story, ila ukiwa open minded utagundua kuwa Mungu amewatukuza watoto wote wa Ibrahim hapo then nyinyi mnapata wapi biasness ya kumchagua Isaac na mkamkataa Ismail?

Ila sijaona mgao wa urithi hapo, au ndo kile kiriba cha maji walichopewa?
 
Nimesikiliza "qari" yaani msomaji, kasoma Surat Saffat aya ya 100 mpaka aya ya 105. Nimesikiliza na aliyepewa kutafsiri, hapo ndipo alipoboronga. Na yeye kwa kuwa anajuwa anahokisema akamsukumia mtafsiri mwengine aitwae Ibn kathir, akasema huyo mtafsiri ndiye kasema huyo mtoto ni "Ismail". Hayo Yanabaki kuwa ni maneno ya mtafsiri (commentator) na siyo ya Qur'an.

Maana yake nini hiyo? Maana yake hakuna katika hizo aya zilizosomwa alipotajwa Ismail.

Ndiyo maana post ya juu huko nikasema yamepachikwa maneno kutoka nje ya Qur'an. Hata wewe ukiisikiliza aya inaposomwa hutosikia jina la Ismail, hilo utalisikia kutoka kwa "mtafsiri (commentator). Kayatowa wapi hayo aliyoongezea kama hayapo kwenye Qur'an? Hilo ndilo swali la kujiuliza.
 
hujaona baraka ya kumfanya kuwa uzao, sisi tunaamini uzao wa Ismaili ndio wote wakaao jangwani,
 
Iweke hiyo aya hapa.
Ushahidi unaletwa mahakamani na sio mahakama kuufuata
Sawa mahakama, mtoririko wa hizo aya ni huo hapo chini

99 - And [then] he said, "Indeed, I will go to [where I am ordered by] my Lord; He will guide me.

100- My Lord, grant me [a child] from among the righteous."

101 - So We gave him good tidings of a forbearing boy.

102 - And when he reached with him [the age of] exertion, he said, "O my son, indeed I have seen in a dream that I [must] sacrifice you, so see what you think." He said, "O my father, do as you are commanded. You will find me, if Allah wills, of the steadfast."

103 - And when they had both submitted and he put him down upon his forehead,

104 - We called to him, "O Abraham,

105 - You have fulfilled the vision." Indeed, We thus reward the doers of good.

106- Indeed, this was the clear trial.

107 - And We ransomed him with a great sacrifice,

108 - And We left for him [favorable mention] among later generations:

109 - "Peace upon Abraham."

110 - Indeed, We thus reward the doers of good.

111 - He was truly one of Our faithful servants.

112 - We ˹later˺ gave him good news of Isaac—a prophet, and one of the righteous.

113 - We blessed him and Isaac as well. Some of their descendants did good, while others clearly wronged themselves.
 
aliyetolewa sadaka ni Isaka na sio Ismaili, hata kwenye suala la urithi Ismali alipewa vichache lakini Isaka alipewa vyote
Kama vile ulikuwepo kama Mzee wa baraza wakati wanagawanya urithi! Kuwa Mswahili ( Mwafrika) Raha sana.
 
"Kayatowa wapi hayo aliyoongezea kama hayapo kwenye Qur'an? Hilo ndilo swali la kujiuliza"
 
hujaona baraka ya kumfanya kuwa uzao, sisi tunaamini uzao wa Ismaili ndio wote wakaao jangwani,
Mbona una generalize kiasi hicho kamanda? ... kumbukua kweye hilo jangwa palifanywa kisima na Mungu kwa ajili ya huyo mtoto (Ismail)! ... just for your information, hayo maji ndo yanaitwa maji ya "zamzam", mpaka leo yapo kuthibitisha kuwa Mungu aliagiza Ibrahim awapeleke pale kwa malengo maalum ya baadae. Hivi hii haikuoneshi wewe kuwa hii ilikuwa ni foundation ya future prophet to come in Ismail's generation?

Halafu pia ukisema uzao wa Ismail ndo wanaokaa jangwani does this include mpaka na sahara desert?
 
Ibrahim ni Muebrania kiasili lakini dini yake ni Myahudi na ndie muanzilishi wa dini ya wayahudi.

Mungu wa Ibrahim, isaka ma Yakobo ambaye ni Yahwe ndiye alimchagua Ibrahim kuanzisha dini ya Kiyahudi
Wewe tubaki kwenye kufanya UCHAWA kwenye siasa. Haya mabo ya dini waachie werevu.

Judaism ni dini ya Wayuda. Yuda ni mtoto wa Yakobo. Hivyo, UKWELI unabaki pale pale kwamba Ibrahimu hakuwa Myahudi.
 
"Kayatowa wapi hayo aliyoongezea kama hayapo kwenye Qur'an? Hilo ndilo swali la kujiuliza"
Aulizwe yeye mpotoshaji, msikilize vizuri "sheikh" aliyepewa kutafsiri, yeye kamsukumia "Ibn Kathir", anaelewa kuwa hapo kwenye aya hizo zilizosomwa halijatajwa jina la Ismail.

Hapo juu kidogo neno "sheikh" nimeliweka kwenye mabano kwa sababu naamini Sheikh wa kweli hawezi kuwa mpotoshaji na kupachika majina yasiyokuwepo kwenye aya zilizosomwa.

Hiyo ni tafsiri inayopogtosha na kubadilisha maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…