Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Tatizo kubwa hapa ni ku-mordernize mambo, enzi hizo kulikuwa na house girl? tumia neno sahihi kumuelezea hajra laikuwa ni nani!
Mwanzo 16:1

[1]Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.

Now Sarai Abram's wife bare him no children: and she had an handmaid, an Egyptian, whose name was Hagar.
 
Sasa anakuaje mwanawe wa pekee wakati yupo mkubwa wake? ... au kiswahili kimebadilika saivi kwamba pekee haimaanishi pekee tunayoijua?
Kwa sababu Ishmael alikuwa mwana wa Ajiri. Wa Ibrahim alikuwa ni Isaka.
 
Katika Historia ya Ibrahim alimpata Ishamil baada ya kufika Kaanani na si njiani, unakubalina na Hili?
Nakubaliana Na wewe kabisa kulingana na Biblia 100%
Ibrahim Hadi Leo Waislam na Wakristo wote wanakubaliana kuwa Kaburi lake liko Hebron Israel?
Hebroni iko Ukinga wa magharibu mwa israel Eneo ambalo Ni Palestina Na sio Israel
Je unataka kusema Ibrahim alitembea kwenda Saudi Arabia kumtoa Sadaka mtoto wake?
Hakuna Mahali nimesema kuwa alienda mpaka Saudi arabia..

Ila Hata hivyo.Biblia inasema alitoka Nchi ya Kanaani mpaka nchi ya Moria kwenda kumtoa sadaka mwanae..
Screenshot_20240620_131917_Biblia Takatifu.jpg
 
Una Uhakika Mkuu? (Soma mwanzo 13:25)
Lets Talk Facts..

Tuanze na Mwanzo 16:15-16
View attachment 3021350

Ibrahim/Abram alikuwa na Miaka 86 Alipomzaa Ishamael..

Baada ya Miaka 13 Mungu alifanya Agano na Abram agano la kwanza La kutahiriwa na kubadilishwa Jina kutoka Abram Kuwa Ibrahimu..

Mwanzo 17
View attachment 3021358

Wakati wa Agano hili na wakati watoto wote wakitahiriwa na watu wote wa Ibrahimu..
Ishmaili alikuwa Mtoto pekee wa Ibrahimu akiwa na miaka 13 na Isaka akiwa bado hajazaliwa..

Ibrahimu alimpenda Sana Ishamael na ndo maana alimuambia Mungu kuwa Anaomba Ambariki Ishmaili..

Hapa chini utapata uone Ombi la Ibrahimu kwa Mungu na ukisoma kwenye aya ya 23 utapata miaka ya Ishamael
View attachment 3021364

Kwahyo Ibrahimu alikuwa na Miaka 100 alipozaliwa Isaka hiyo inamaanisha Kuwa Ishmael alikuwa na Miaka 14 View attachment 3021365

Sasa lini Amri ya Kuchinjwa Ilifanyika.?

Katika Theolojia Wanatheolojia Baadhi wanakubaliana kwamba Ibrahimu alipata Amri ya Kumchinjwa mwanae akiwa na Miaka 100 yaani Ibrahimu akiwa na miaka 100..

Sasa Do the maths Kipindi Ibrahimu akiwa Na miaka 100 Only Son aliyekuwepo Ni Ishmael na Baadae alizaliwa Isaka..

All you have to do ni kutafakari tu na Kuchambua utapata Ukweli
Halafu Biblia inajichanganya tena kuonesha kuwa Ismael aliondoshwa na mama yake pindi ni mchanga mtoto wa kubebwa mgongoni

Mwanzo 21:14-19
 
Swali kwa Mkristo yeyote yule:

Je ismael na Hagar waliondoka kupelekwa jangwani kabla au baada ya kuzaliwa kwa Isaka?
 
Mwanzo 16:3

Biblia inamtambua Hajar kuwa ni mke halali wa Ibrahim.

Kuna tatizo kwa mwanaume kumuoa mfanyakazi wake?
Mwanzo 16:1-2
[1]Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.

[2]Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
 
Mwanzo 16:1

[1]Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.

Now Sarai Abram's wife bare him no children: and she had an handmaid, an Egyptian, whose name was Hagar.
Na vipi Kuhusu Andiko hili Mkuu Daudi?

Mwanzo 16:3

"Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe.

And Sarai Abram's wife took Hagar her maid the Egyptian, after Abram had dwelt ten years in the land of Canaan,
and gave her to her husband Abram to be his wife."

Nikuulize kitu Daudi?
Unajua Hajri alitokea wapi alikuwa Princess wa Misri na alipewa ibrahimu kipindi kile farao alipoogopa mkono wa Mungu..

Baada ya kukaa miaka kumi kwa sheria ya Waebrania Ilimpasa Ibrahimu kumuachia huru ila mkewe sara alionelea kuwa Asimuache ila amuozeshe kwa Mumewe....

Kuna watoto wengi tu ambao wametoka kwa wamama ambao ni Vijakazi..

Mtoto wa Yakobo Dani Ni wa Bilha ambaye ni Kijakazi..
Mtoto wa Yakobo Naftari Ni wa Bilha ambaye ni kijakazi..
Mtoto wa Yakobo Gadi ni mtoto w zilpa ambaye ni kijakazi..
Mtoto wa Yakobo Asheri ni mtoto wa Zilpa ambaye ni kijakazi..

Katika Vijakazi wote wakeze Yakobo hakuna hata mmoka yakobo aliyekuwa amemuoa..

Soma mwanzo 29 mpka mwanzo 30
 
Mwanzo 16:3

Biblia inamtambua Hajar kuwa ni mke halali wa Ibrahim.

Kuna tatizo kwa mwanaume kumuoa mfanyakazi wake?
Mwanzo 16:5-6

[5]Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.

[6]Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.

STATUS YA HAJIRI BADO ALIKUWA KIJAKAZI
 
Halafu Biblia inajichanganya tena kuonesha kuwa Ismael aliondoshwa na mama yake pindi ni mchanga mtoto wa kubebwa mgongoni

Mwanzo 21:14-19
Yeah naelewa Kuna Kitu kinaitwa Documentary Hypothesis au kinafahamika zaidi kaka JEPD Theory ukisoma Utaelewa Kwanini Story unahisi Zinajichanganya..

Ni kwamba Theologically Torah iliandikwa kwa nyakati tofauti na Kwa Sources tofauti ila kwa bahati nzuri ama mbaya Sources zote zilichanganywa kwa pamoja hivyo kufanya Overlaping of Stories.. "JEPD Sources"

Hata Ukiangalia Story ya Yusufu kwenye Biblia tukitaka tuichambua Bila kufata JEPD theory kuna mahali itakuchanganya..

Kwamba walimtupa kwenye shimo au walimuuza?
Na story nyingi tu zimejirudia kwa mtizamo tofauti..
 
Na vipi Kuhusu Andiko hili Mkuu Daudi?

Mwanzo 16:3

"Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe.

And Sarai Abram's wife took Hagar her maid the Egyptian, after Abram had dwelt ten years in the land of Canaan,
and gave her to her husband Abram to be his wife."

Nikuulize kitu Daudi?
Unajua Hajri alitokea wapi alikuwa Princess wa Misri na alipewa ibrahimu kipindi kile farao alipoogopa mkono wa Mungu..

Baada ya kukaa miaka kumi kwa sheria ya Waebrania Ilimpasa Ibrahimu kumuachia huru ila mkewe sara alionelea kuwa Asimuache ila amuozeshe kwa Mumewe....

Kuna watoto wengi tu ambao wametoka kwa wamama ambao ni Vijakazi..

Mtoto wa Yakobo Dani Ni wa Bilha ambaye ni Kijakazi..
Mtoto wa Yakobo Naftari Ni wa Bilha ambaye ni kijakazi..
Mtoto wa Yakobo Gadi ni mtoto w zilpa ambaye ni kijakazi..
Mtoto wa Yakobo Asheri ni mtoto wa Zilpa ambaye ni kijakazi..

Katika Vijakazi wote wakeze Yakobo hakuna hata mmoka yakobo aliyekuwa amemuoa..

Soma mwanzo 29 mpka mwanzo 30
Asante kwa ufafanuzi ila tulikuwa tunatafuta status ya Hajir, pamoja na kuzaa na Ibrahimu lakini hakuwa mke bado alikuwa Kijakazi, ndo maana hata ilipotokea ugomvi aliyemfukuza ni Sarah sio Ibrahimu
 
Hebu ifanyie tarjama hiyo aya kwenda kwa kiswahili ili tuone kama aliyetolewa sadaka si Ismael?

Aya ipo wazi imeeleza mtiririko mzima toka ibrahim anapata mtoto wa kwanza kisha mtoto anakua kufika balehe, ibrahim anapata ndoto kuwa amtoe sadaka mwanae, anatekeleza ila Mungu anamlipa kwa kumpa kichinjo, kisha anapewa bishara kuwa atapata mtoto mwingine aitwae ishaq.
Hakuna neno "sadaka wala amtoe mwanae, umepotosha. Hilo neno sadaka na amtoe mwanae ni lipiu katika hizo aya zilizosomwa au nyingine yoyote kwenhye kisa cha Ibrahim?

Sadaka ya watu hutolewa na wachawi, Mwenyeezi Mungu hawezi kusema wala kuamrisha hayo.
 
Asante kwa ufafanuzi ila tulikuwa tunatafuta status ya Hajir, pamoja na kuzaa na Ibrahimu lakini hakuwa mke bado alikuwa Kijakazi, ndo maana hata ilipotokea ugomvi aliyemfukuza ni Sarah sio Ibrahimu
Umesoma Biblia ilivyoandika Kwenye Mwanzo 16:3
Kama umeelewa kuhusu Fungu hilo usingeandika hicho...
inasema kuwa "Sara alimpa kijakazi wake Awe mkewe na sio kijakazi tena.."

Sema kuna Tatizo kwenye Chuki iliingia Ambayo Neno kijakazi liliamua Kutumika kumshusha..
Nimekutolea Mfano kuna Vijakazi wengi walizaa kwanini Hawatamkwi kama vijakazi??
Na nimekupa Mfano wa watoto wa Yakobo..

Hata hivyo Hajri alikuwa ni Mke wa Ibrahimu na aliyemfukuza Hakuwa Sara ila ibrahimu
Soma Mwanzo 21:9-14
Screenshot_20240620_134553_Biblia Takatifu.jpg
 
Tunaifuata ila Yesu Kristu alipokuja alirekebisha baadhi kwa mfano ulaji wa nguruwe. Soma Agano Jipya kitabu cha Matendo ya Mitume Sura ya 10
Wapi yesu aliwahi kula nguruwe hata kwa bahati mbaya? Zaidi tunasoma aliyakemea mapepo yakakimbilia kwenye nguruwe na kutumbukia baharini
 
Nakubaliana Na wewe kabisa kulingana na Biblia 100%

Hebroni iko Ukinga wa magharibu mwa israel Eneo ambalo Ni Palestina Na sio Israel

Hakuna Mahali nimesema kuwa alienda mpaka Saudi arabia..

Ila Hata hivyo.Biblia inasema alitoka Nchi ya Kanaani mpaka nchi ya Moria kwenda kumtoa sadaka mwanae..
View attachment 3021397
Moria alipoenda ni Jerusalem ya Leo...

Eneo ambalo kuna ule msikiti wenye paa la Dhahabu Ndio kuna Jiwe linalosemekana Isaka alilala.

Pia Wasamaria wanaamini ni nje kidogo ya Jerusalem
 
Back
Top Bottom